Maoni Ushauri na Mapendekezo kwa mabasi ya mwendo kasi (DART): Nini changamoto, nini umefurahia?

Pdidy ktk ubora wako wa kufichua maovu. Ahsante kwa taarifa bila shaka wahusika wataifanyia kazi.
 
Hawa Mwendokasi nashindwa kuwaelewa!! Hadi sasa wanashindwa kuendesha haya mabasi kisasa; Hata tu kuwa na basic requirement (Timetable Wameshindwa!!) Hawa polisi kwenye juctions nawashauri wazingatie kusimamia matumizi bora ya barabara na waache interference!!
 
basi nimecheka sana, ikifika usiku mabasi ya dart yanakua kama daladala, utakuta akitoka mbezi kwa sababu no usiku basis basis linakua tupu,akipita vituo vya kati basis anaita kimara kimara, hapo hutumii kadi unaingia unampa konda 500 , maisha yanaenda, nadhani baada ya miezi 6 zitakua vurugu tupu na huu usafiri.
 
Zaidi ya 60% ya kengere/alarm ndani ya haya mabasi hazifanyi kazi, kwa wale abiri wanaoshuka vituo vya katikati kama Shekilango, Urafiki n.k wanapata shida ya kupitishwa kwenye vituo maana ukibonyeza zile switch hazifanyi kazi na wakati mwingine waweza usijue kama imelia au la!
Kuna wakati dreva anawauliza abiria kama kuna wa kushuka aseme, lakini hakumbuki kuwa mtu aliye nyuma hawezi kusikia. Na wanapokuwa wanatoka kituo cha mwanzo wanasema kuwa wanasimama vituo vyote na badala yake hawafanyi hivyo.
Nashauri sana abiria wanaoshuka njiani muwajali hasahasa mida ya asubuhi. Na si vyema kutotengeneza hizo switch za alarm, tengenezeni acheni ubabaishaji
 
Hivi kuna haja gani kuweka mabasi nane morroco? Matokeo yake mabasi hayo ni nadra sana kujaza hata level seat. Kwa nini yasiwe mawili yakawa yanashusha abiria jangwani au magomeni ambapo mabasi ya route zao?
Mkiendelea kuiga huo mfumo wa route za daladala zs Sumatra mtasababisha tuendelee kuchekwa na majirani maana biashara itawashinda.
 
Jambo lingine ni matumizi ya kadi. Kadi ziwe na kifurushi vya wiki au mwezi. Hii itasaidia mgeni anayetembelea Dar kwa muda mfupi naye atumie kadi. Nchi za watu kadi ya za muda mfupi ni ghali ikilinganishwa na za muda mrefu. Ni kawaida sana kukuta mtu anatembelea mji kwa siku NNE ila anaona ni hasara kununua kadi ya mwezi kuliko kununua kadi ya mwezi. Hiyo ndivyo wenzenu wanapata faida siyo nyie mnaovizia 250/= za watu kinyemela.
 
Hayo magari siku za jmos na jpili yanakuwa ya shida sana hasa Kimara terminal unaweza kukaa hapo zaidi ya saa nzima unasubiri gari
 
Mimi nikiwa kama abiria wa DART maomba kuonyeshwa kukerwa kwangu na huduma zenu kwa wiki hii.

Kuna mpango mmeanzisha wa kusimama kila kituo hata lama gari limejaa.

Mgano sasa hivi nipo kwenye gari namba A-032 kutoka Kimara kwenda Gerezani
Dereva lasema kapewa maagizo ya kusimama kila kituo hata kama gari limejaa na hakuna abiria anayeshuka.

Kuna umuhimu hani wa kufanya hivyo, uharaka tuliambiwa?
 
Mimi nikiwa kama abiria wa DART maomba kuonyeshwa kukerwa kwangu na huduma zenu kwa wiki hii.

Kuna mpango mmeanzisha wa kusimama kila kituo hata lama gari limejaa.

Mgano sasa hivi nipo kwenye gari namba A-032 kutoka Kimara kwenda Gerezani
Dereva lasema kapewa maagizo ya kusimama kila kituo hata kama gari limejaa na hakuna abiria anayeshuka.

Kuna umuhimu hani wa kufanya hivyo, uharaka tuliambiwa?
Hivi kwa utaratibu uliopo sasa, DEREVA ANAJUWAJE KWAMBA KITUO KIFUATACHO KUNA MTU ANASHUKA? AU ANAPANDA KUELEKEA LINAKOKWENDA BASI HUSIKA? MAANA MKIFIKA SEHEMU KAMA MOROCO HOTEL HUWEZI JUWA WALIOKO KITUONI WANAKWENDA KIMARA AU GEREZANI AU KIVUKONI
 
Back
Top Bottom