Maoni: Safu ya Baraza la Mawaziri haiakisi maendeleo, inaakisi nchi kumilikiwa na familia fulani zinazoamini bila wao hakuna Tanzania

Shida ni tishio kwa mzoga gang kwa kuwa alikuwa mfuasi wa Magu,waliondolewa wote ni wafuasi wa magu kindakindaki wao wamegoma kwenda na mama wa kaya, kaawacha akidhani ndio anaondoa kadhia kumbe kadhia ndio kwanza imeanza, hivi Kingu,Bulembo, Zungu pamoja na kuimba mapambio wee hawajapewa uwaziri ama kweli CCM ina wenyewe na wenyewe ni wenye baba zao, akina January,Nape,Ridhiwani( huyu ndio ajira ya kwanza rasmi kila kitu analetewa mezani kuanzia ubunge na sasa uwaziri)
Wewe nimetumia hela zangu nyingi sana kukuelimisha , lakini una bichwa gumu sana , haya sasa kiko wapi ?
 
Tangu nchi ibaki na Rais mstafu mmoja (Achana na mzee wetu ambaye hajiwezi kwa lolote), haina kabisa tofauti na nchi ya kifalme.

Hii nchi ni ya familia.
Hata Magu alilipa fadhila Kwa familia.Hii nchi ina wenyewe sisi wengine tunakula wanavyotumegea 😃😃.

Kuwa chawa acha kulia Lia kama mtoto.
 
Masauni ni wa znz pia
naona huu mwaka spika nae atoke tu znz
Waziri mkuu nae znz!

Hivi akina Kabudi, Mkuvi na wengine hata Majaliwa
si wajitoe ccm?
Kweli hii nchi imekuwa genge sasa!

Siku bwana yule akitangulizwa na yeye kwa Baba
hakika nchi yetu itapiga hatua kubwa!

Upinzani hii ndiyo nafasi pekee ya kuingia Ikulu
huenda Mungu amejibu maombi yenu
Cha msingi mleteni mtu sahihi!
Kinachofata nae si atanyooshwa tu😅 kwani sindio mtindo wao CCM huko!
 
On my view:

Magufuli alifanikiwa sana kwenye uchaguzi kutokana na ufanisi kila kona kutokana na mawaziri aliokuwa nao.

Ushindi wa CCM 2025 utakuwa determined sana na perfomance ya hili baraza.
Mkuu una uhakika tutafika 2025 kabla Hangaya hajalivurugua tena hili baraza????
 
Nimeona mkeka wa baraza jipya la Mawaziri, unajiuliza uchaguzi umeisha au bado tupo Kwenye kampeni? Watu waliopo Kwenye baraza la Mawaziri ni watoto wa familia zilezile zinazoelekea kustaafu au zilizostaafu.

Hakuna ufanisi, ubunifu wala mikakati ndani ya baraza bali wamewekwa watu wakumsaidia Mhe. Rais kupiga kampeni kuelekea uchaguzi ujao.

Baraza la Mawaziri kwa kipindi hiki halipaswi kujazwa watu wa propaganda, inahitaji watu wakufikiri kuhusu maendeleo ya nchi yetu.

Baraza la sasa limerejesha fadhila Kwa timu Jk baada ya miaka mitano ya mateso. Naiona Tanzania maskini huko tuendako
Baraza la mchongo. Yaani kelele zile zote ndio kaja na hivi vituko
 
Sasa tuibue hoja ya katiba mpya tushirikiane wananchi wote bila kujali vyama vyetu iwe mvua au jua katiba mpya lazima ipatikane
Unadhani rahisi kiasi gani ndugu yangu,hapa nikuomba nakusali Tu,watanzania hatuna ujasiri huo walidai lolote,nawao wanafanya hivi kwavile washajua watanzania hatuyawezi mabadiriko
 
Wewe nimetumia hela zangu nyingi sana kukuelimisha , lakini una bichwa gumu sana , haya sasa kiko wapi ?
Hah hah naona umefurahiii, hawa sisi tunao tu subiri. Huku ofisini kwenu pamekuwa mahame ya mbuzi nasikia mnapangisha vyumba nakuja kuchukua chumba kimoja mwana CCM mie nisie bebwa kwa kutumia baba.
 
Nilijua utaitaja Ujerumani na ni kwa sababu inaipa misaada CHADEMA kwa ajili ya kufanyia uchochezi na kutukana mitandaoni.
Nyinyi kila mtu akikosoa tayari anakuwa ni Chadema, haya na wewe ni nani anaekulipa kuja kushangilia mitandaoni??
 
Hivi hata hauoni aibu kuongea hizi pumba??
Huoni wewe ndiyo pumba? Mimi nimeuliza hao wateule wana shida gani hadi wakose sifa?

Unachotakiwa ni kujibu sio kuandika kiroja ambacho hakina fact yoyote.
 
Back
Top Bottom