Mjasiria, Salaam Aleikum, Ahsante kwa maoni yako. Nimekuelewa. Swali langu ni hili: Kwa nini wewe ni Mwislamu zaidi yangu kwa kuwa unafunga na mimi sifungi? Dini ni sharia si ndio? Sasa kama wewe hufuati masharti ya dini yako, kwa nini uwaambie wengine kwamba wamepotea na warudi kwenye mwanga wakati wewe mwenyewe huwezi kufuata masharti ya dini yako. Kama nilivyosema mwanzo, hamna binadamu anayeweza kufata masharti YOTE ya dini yake. kwa hivyo kama wewe unafunga na mimi sifungi , lakini wewe hufuati sharia law Tanzania na unampeleka mkeo apewe dawa ya kuzuia mimba au kufunga kizazi basi kwa nini wewe uwe Muislamu bora zaidi wakati umeshavunja sharia ya Uislamu ya kutoingilia mambo ya Mungu? Umenipata? Katika maisha ya leo, narudia, hasa maisha ya karni hii, ni vigumu kujiita Mdini wakati huwezi kufuata sharia za dini. Hata Saudi Arabia yenyewe, watoto wa kiume wengi wanabatiliwa kwa kuwa wasichana wanafungiwa na hawana ruhusa kukutana na wanaume ambao sio ndugu zao na hamna ruhusa kutembea na mwanamme na mwanamke kama sio ndugu yako au jamaa yako. Hi ni sharia ya Kiislamu, je wewe unaishi namna hivi? Je, unapokea riba katika benki? Unatoa sadaka kamili kama inavyosema dini kila mwaka? Humtongozi mwanamke kazini au kuongea nae? Je, unakubali kukatwa mkono ukikamatwa na wizi? Kabla ya kunitenga na kuniambia mimi sio mwislamu kamili kwa kuwa sifungi, wewe pia jiangalia nafsi yako na toa jibu kamili kama wewe pia unafuata sharia ZOTE za dini yako, sio kuchambua chambua tu. Narudia, dini na maisha ya kisasa hayalingani, kama yangelingana basi tusiongetumia vidonge vya kuzuia mimba au wote tungeishi katika sharia za dini zetu ya karne ya 15. Sijui wewe, lakini mimi sitaki kuishi chini ya sharia za dini kama kanuni ya nchi kwa sababu zimepitwa na wakati wake ndio maana kuna binadamu wachache mno wanaoweza kusimama na kusema wanafuata aamri yoye ya dini zao.
Waalaykum msalaam. Kwanza mkuu mimi sijasema kuwa mimi ni muislamu kuliko wewe. Nilichosema mimi ni kuwa, kwa wewe kutangaza hadharani kuwa hujafunga kwa miaka 10 kwa kuwa tu umeamua hivyo (Kumbuka hukutoa sababu yeyote ya msingi). Zaidi ya hapo ukaongeza kuwa huna mpango wa kufunga kabisa, hapa kwa mujibu wa taratibu na sheria za kiislamu sidhani (makusudi kabisa nimetumia neno sidhani, hata ukirudi kwenye ile posti yangu ya kwanza ndilo neno nililotumia) kama unaweza kusimama mahali na kuusemea uislamu. Hii ni kwa sababu japokuwa uislamu una mambo mengi, lakini funga ni nguzo ya tatu ya uislamu na funga ni moja ya ibada ambayo imesisitizwa sana katika uislamu na ghadhabu anazopata M'mungu kwa mtu kuacha kufunga kwa makusudi ni kubwa mno. Hivyo basi mtu anayeacha kufunga bila sababu ana walakini sana na imani yake juu ya uislamu wake. Kumbuka kuwa si mimi nayehukumu hapa, nilichofanya mimi ni kukupa tu msimamo wa uislamu juu ya kuacha kufunga bila sababu. Unaweza ku-google hapo kwa maelezo zaidi juu ya kuacha funga. Kumbuka pia kwenye uislamu dhambi hazilingani, kwa mfano kuua si sawa na kumtukana mtu.
Halafu mkuu kuwa kwangu muislamu mbaya hakuwezi kuhalalisha wewe kuwa mbaya vilevile. Pili dini si sharia peke yake. sharia ni sehemu ya dini. Uislamu ni mfumo wa maisha wenye kila kitu. Kuhusu vijana wa Saudi, hapo kuna mkorogo wa mambo mengi na sidhani kama hapa ni mahali pake. Duniani leo kuna matatizo mengi sana ambayo kama tukianza kuyajadili hapa hatuwezi kumaliza. Nafikiri ni busara zaidi tuendelee kubaki kwenye mada husika japokuwa kwa kiasi fulani naona kama tunatoka.
Mkuu kwa nini unanisemea mambo ambayo huna uhakika nayo. Maana umeshasema nampeleka mke wangu akapewe dawa ya mimba, nakula riba wakati hata hunijui. Tufanye basi labda nafanya hayo mambo. Lakini kama umesoma vizuri pale juu nimekwambia kwamba Allah(sw) anatambua watu tunafanya makosa na ndiyo maana milango iko wazi kwa waumini kutubia na kuomba msamaha. Hicho ndicho kinachotufanya sisi binadamu. Ndiyo maana kuna hadi aya, Allah(sw) anasema, "Kama mngalikuwa ninyi binadamu hamfanyi makosa, basi ningeliwaondoa na kuwaleta wengine wanaokosea na kuomba msamaha" (Siyo tafsiri rasmi,
bidodo kama unaweza tusaidie na hii tafadhali). Kwa hiyo basi naweza kuwa nafanya hayo lakini nina nafasi ya kutubu na kutaka maghfira.
Kuhusu suala la sheria za dini kupitwa na wakati, dini ni hiari na uislamu haujapitwa na wakati. Huwezi kudai wewe ni muislam halafu wakati huo huo unaukataa huo uislamu. Huu ni mkanganyiko wa aina yake, nimesema hapo kuwa unaweza kuacha uislamu kama huridhiki, ni hiari si lazima.
Mkuu binadamu hatujakamilika na tunabadilika, mimi siwezi kujiona bora kuliko yeyote. Hata kama mimi ni bora kuliko wewe sasa hivi kitu ambacho siwezi kujua wala kuwa na uhakika nacho, lakini nitajuaje kama wewe kesho utakuwa bora kuliko mimi. Allah(sw) anatuambia ni kwa rehma zake tu mtu anaweza kumtii na kufuata haki, si ujanja wetu. Na ukifikiria kwa makini, hii kitu ina maana sana, maana mtu hajichagulii anachoamini. Ni kama vile mtu anajikuta tu anaamini kitu fulani. yaani hatuna udhibiti kabisa wa imani zetu na ndio maana sisi waislamu tunatakiwa kumshukuru Allah(sw) kwa neema hii kubwa ya kuwa waislamu
Allah(sw) atuongoze sote katika nuru na njia ya haki....Amin.