MAONI:. Ndoa ,,, Waislam vs Wakristo

Status
Not open for further replies.
Msifungwe nira na wasioamini. Biblia inasema wazi ktk kitabu cha Mathayo. Pia Yesu alitamka hadharani mchana kweupe kuwa Nuru na giza haviwezi kukaa pamoja. Sasa iweje mkristo ukaoe muislam? Me mpk naoa na kuruka ruka kwangu kote nilikuwa sigegedi wala kutongoza demu asiye wa dini yangu.
 

And the vice versa is true
 

Mbona Mzee Makamba kamuo Mkristo na kila mtu yupo na dini yake ile ile na mzee Makamba ni muumini mzuri tuu...

Muumini mzuri anamjua M'mungu peke yake. Wewe unamjuaje mtu ni muumini mzuri??!!!
 

Msijidanganye wakristo wa sasa si ahalul kitab.. ahalul kitab ni wale wanaoamini agano la kale.. kwani life style yao haipishani sana na waislam mfano maamrisho ya kutokula kitimoto etcl..
 
Hapo nadhani amekujibu kulingana na mafundisho ya kiislamu, kwa hiyo ukitaka na kujadili sheria ya ndoa au sijui familia ya Tanzania utachanganya mambo sana. au bidodo?

Kabisa mkuu, hawa watu hawaendi na maneno matukufu bali wanatizama nini nafsi inataka
 
Last edited by a moderator:

:becky:
Mkuu hiyo mifano yako Kiboko dah!! Punguza kuhukumu bwana, huenda Allah(sw) akawajaalia kheri hao unaowaona wewe si waislamu au huenda wakawa na thamani zaidi kwa Mungu kuliko wewe.
 

Mkuu unachanganya mambo hapa. Mafundisho ya kiislamu ni jambo moja na kile kinachotokea duniani kwa sasa ni kitu kingine. Hapo juu bidodo ameongelea msimamo au taratibu za dini ya kiislamu sio vile wewe, nchi au watu wanavyoishi au kufanya. Na hili ni tatizo kubwa sana kwa sasa watu wanapenda kuchanganya kile wanachofanya waislamu na mafundisho ya kiislamu.

Tukija kwenye suala la nchi kuwa tajiri au la, sijui unaongelea nchi gani lakini Saudi Arabia ni nchi tajiri na sijasema hii ndiyo nchi hasa inayofuata uislamu ila ukienda Saudi kwa kiasi kikubwa utakuta wanafuata taratibu za kiislamu.

Halafu mkuu wewe ulishawahi kusema mahali kuwa hata kufunga ulishaacha kwa miaka kumi sasa na wala huna mpango wa kufunga. Sidhani kama msimamo huu unakuweza kukupa haki ya kusimama mahali na kuusemea uislamu.

Allah(sw) akuongoze umrejee na ujue thamani ya dini yako bi-idhinihi.
 
Last edited by a moderator:

Hiyo kukaa nae kwa muda inaitwaje na katika uislam inaushahidi au ni maneno yako? Tusaidie
 

Umemaliza kila kitu. kilichobaki ni kika mwenye akili atajijibu kulingana na swali la ndoa zinazoonekana mitaani kuhusu pande hizi mbili
 
Ahlul kitabu sasa hv hawapo kwani ahlul kitabu hawasemi kuwa yesu ni Mungu nw kuna washirikina

Thats my point wakristo wa agano jipya si watu wakitabu waliozungumziwa kwenye quran tukufu na haturuhusiwi kuoa.. nakumbuka mdogo wangu wa kike alinitumia msg maana aliona aibu hata kunipigia simu akaniuliza "kaka hivi ikatokea mkristo kabadili dini na ataka kumuoa muislam nini maoni yako " ?

Kwanza nilijua yeye so alikuwa akitaka baraka tu za kaka.. nilimjibu kwa ufupi ran as far as u can kwa hao wanaobadili kwa ajili ya ndoa.. uislam ni total submition towards Allah..

I hv seen some cases mtu anabadili kwq ajili ya kuoa akiingia ndani ya ndoa pombe kama kawaida, kusali wala hasali, kitimoto, kila siku mwanamke kupigwa ndani ya ndoa vyo hivo ni kinyume na utaratibu wa dini..

Nashukuru alinielewa kaka yake now she's happy married kwa kijana wa kiislam
 

Mi nakuelewa sana mkuu, nimeishi kwenye hizo nchi pia. Ukiusoma vizuri uislamu utaelewa kwa nini pamoja na hayo unayosema lakini M'mungu anawaamrisha kumtii kwa kadri ya uwezo wao. M'mungu mwenyewe amesema katika Qur'an kuwa binadamu ni viumbe dhaifu sana na wenye mapungufu, kwa hiyo kukosea ni kitu kinachotarajiwa ila kila unapokosea ni vyema kuomba msamaha na kutubia. Kifupi ni kwamba perfectionism kwenye uislamu ni suala la mtu kukubali ubinadamu, kumtambua M'mungu na kuomba msamaha kila anapokwenda tofauti, sio kuwa malaika.

Kitu kingine kuwa muislamu ni hiari mkuu, kama unaona yale yanayosemwa katika uislamu ni mambo ya kizamani na hayawezekani, unaweza kuacha tu huo uislamu. Kwanza sina hakika sana kama unaweza kuendelea kujiita muislamu maana ushapingana na aya ya M'mungu inayosema kuwa wanaume ni viongozi wa wanawake katika Qur'an (Bahati siikumbuki hiyo sura wala namba ya aya, ila kama ni muhimu nitaitafuta nikuwekee).

Kingine unaongelea kuhusu masuala ya elimu kama vile uislamu unakataza kumsomesha mtoto wa kike. FYI kutafuta elimu ni excuse pekee inayomruhusu mtoto wa kike kwenda kinyume na amri za mume au baba yake. Yaani kama baba/mume anasema hakuna kupata elimu, mtume amemruhusu mtoto wa kike kwenda kinyume katika hili na kuelekea katika njia ya kutafuta elimu. Sasa sijui unaongelea vitu gani hapa.
 
Naomba kufahamu , ni kwanini Waislam hawako tayari dada/mabinti zao kuolewa na Wkristo wakati wao wanaoa dada zetu(WAKRISTO) ,,

Taqfadhali maoni.

NO OFFENCE PLEASE.

Sisi binadamu tuna hulka ya kujipendelea ktk kila hali,iwe ya kijinsia,kidini,kikabila,kirangi na kadhalika..Ndo maana utakuta kila mahali watu wanazungumzia pande fulani (UBINAFSI).Suala la kufunga ndoa ni lazima wote mke na mume wawe dini moja kwa wakati huo ndo ndoa itafungwa na kutambulika ktk dhehebu husika.Haijalishi kama ulikua mfuasi wa dini husika tokea kitambo au mpagani au umebadili dini; Hiyo ni kwa mkristo na muislam wa Tanzania japokua hapa duniani kuna dini nyingi tu ambazo TZ hazijafika,zikifika tutazijadili.

Tanzania wanawake wengi wanabadili dini na kufuata dini za waume zao (Wanawake wa kikristo kubadili kua waislam na Wanawake wa kiislam kubadili kuwa wakristo) haijalishi kama ukristo au uislam wao ni wa kweli au wa jina ila wanabadilisha dini kwa maelfu kila mwaka.Haya mambo yanatokea sehemu mbali mbali.Kimsingi mtu hafungwi na imani ya aina fulani,vitabu vya dini vinatoa mafunzo ila havilazimishi mtu,Sema sisi watu ndo tunapenda kulazimisha wenzetu tuwe watu wa dini fulani.Ukiwa mwislam lazima upende watu wote wasio waislam wawe waislam na ukiwa mkristo unapenda watu wote wasio wakristo wawe wakristo.Ukiwa mjinga mjinga wa kupokea tu vitu bila kutafakari utaona unaishi kwa shida sana hapa duniani.

Blogger
yawezekana umependa kuongelea upande mmoja au huna taarifa za kutosha kuhusu watu wanaobadili dini na kuolewa na mtu wa dini nyingine,VIZURI UENDELEE KUFANYA UCHUNGUZI ILI UJIRIDHISHE ZAIDI.
 

Huo ujinga unausema wewe, hakuna mahala katika Uislaam paliposema "mwanaume ndio mwenye sauti zaidi nyumbani" sijui hilo umelitoa wapi?
 
KiIslaam hakuna ndoa hapo ni zinaa tu, huyo unaezini nae ni "pangu patupu" haelewi ndee wala sikio kuhusu Uislaam.

FaizaFoxy:Nakubaliana na wewe kwa 100% kua kwa muislam hiyo si ndoa ni zinaa,Ila kwa mkristo hiyo ni ndoa halali na ina baraka na wataishi vizuri tu.Na pia mwanamke wa kikristo akibadili dini aolewe na muislam ni hivyo hivyo,wakristo watasema hiyo ni zinaa hakuna ndoa wakati huku kwenye Uislam ndoa hiyo ni halali na ina baraka tele na wataishi vizuri tu.Tumeshakua tofauti ni kawaida kusema kua ndoa ya upande mwingine ni ZINAA.Kinachotakiwa mtu binafsi uendeleze juhudi za kuelimisha watu kuhusu imani yako waijue na waifuate.
 
Mjasiria, Salaam Aleikum, Ahsante kwa maoni yako. Nimekuelewa. Swali langu ni hili: Kwa nini wewe ni Mwislamu zaidi yangu kwa kuwa unafunga na mimi sifungi? Dini ni sharia si ndio? Sasa kama wewe hufuati masharti ya dini yako, kwa nini uwaambie wengine kwamba wamepotea na warudi kwenye mwanga wakati wewe mwenyewe huwezi kufuata masharti ya dini yako. Kama nilivyosema mwanzo, hamna binadamu anayeweza kufata masharti YOTE ya dini yake. kwa hivyo kama wewe unafunga na mimi sifungi , lakini wewe hufuati sharia law Tanzania na unampeleka mkeo apewe dawa ya kuzuia mimba au kufunga kizazi basi kwa nini wewe uwe Muislamu bora zaidi wakati umeshavunja sharia ya Uislamu ya kutoingilia mambo ya Mungu? Umenipata? Katika maisha ya leo, narudia, hasa maisha ya karni hii, ni vigumu kujiita Mdini wakati huwezi kufuata sharia za dini. Hata Saudi Arabia yenyewe, watoto wa kiume wengi wanabatiliwa kwa kuwa wasichana wanafungiwa na hawana ruhusa kukutana na wanaume ambao sio ndugu zao na hamna ruhusa kutembea na mwanamme na mwanamke kama sio ndugu yako au jamaa yako. Hi ni sharia ya Kiislamu, je wewe unaishi namna hivi? Je, unapokea riba katika benki? Unatoa sadaka kamili kama inavyosema dini kila mwaka? Humtongozi mwanamke kazini au kuongea nae? Je, unakubali kukatwa mkono ukikamatwa na wizi? Kabla ya kunitenga na kuniambia mimi sio mwislamu kamili kwa kuwa sifungi, wewe pia jiangalia nafsi yako na toa jibu kamili kama wewe pia unafuata sharia ZOTE za dini yako, sio kuchambua chambua tu. Narudia, dini na maisha ya kisasa hayalingani, kama yangelingana basi tusiongetumia vidonge vya kuzuia mimba au wote tungeishi katika sharia za dini zetu ya karne ya 15. Sijui wewe, lakini mimi sitaki kuishi chini ya sharia za dini kama kanuni ya nchi kwa sababu zimepitwa na wakati wake ndio maana kuna binadamu wachache mno wanaoweza kusimama na kusema wanafuata aamri yoye ya dini zao.
 

Bangu-silo sijiui wewe ni dini gani ila ninavyojua mimi ni kwamba dini nyingi zinasisitiza kufundisha na kueneza imani yao ktk hali ya nidhamu;shawishi watu waamini mafunzo ya imani yako.Suala la kutoa elimu ya imani yako lisiwe la kuchagua/kubagua watu wa aina fulani,fundisha mtu yoyote ambaye sio wa dini yako ili wajue na ikiwezekana wajiunge.Una haki ya kuwa na mwanamke yeyote ilimradi kama mmependana na kukubaliana kufuata masharti ya dini husika (kwa suala la ndoa) ila suala la kugegeda bila ndoa hiyo ni ZINAA haikubaliki katika mafunzo ya dini yoyote,ni DHAMBI.
 

Kwa kweli umemalizia maelezo yako kwa hekima sana....Allah ndie anayejua zaidi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…