Maongezi na wazazi wangu jana usiku.

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,831
Walinikalisha kuniuliza kama nimeshapata mchumba au rafiki nisisite kumpeleka nyumbani. Nikawaambia sawa nikimpata ntamleta.
Nikawailiza mahari inakuwaje kulingana na mila zetu?
Wakanitajia, nikapiga hesabu nikaona mahari inafika kama milioni moja na laki 2.
Nikawaambia wazazi wangu kuwa, kwakuwa nina shamba kisarawe, nikipata mchumba wamwambie alete matofali ya kuanzia kwa ajili ya nyumba ambayo itakuwa yangu na mume wangu.
Baba yangu alipinga na kuongea maneno yote mabaya.
Je nilikosea nini?
Au aliona namzibia hela za bakuli la komoni?
 
:amen: Subiri hasira za baba yako zikiisha umuulize taratibu.... kwanini alikupinga ndio utajua, sidhani kama kuna yeyote humu Jamvini anayeweza kukupa jibu la uhakika!!!! Pole sana dada :welcome:
 
Hilo shamba ulinunua kwa pesa yako au ulipewa na baba yako?
Hebu ungea vizuri na mama yako akujulishe namna nzuri ya kuongea na mumewe.
Wakati mwingine wazazi wetu huwa wanahisi kwa sababu ya shule zetu tunawadharau na kuwaletea mambo ya utandawazi
 
ulichanganya vitu viwili hapo na babako ana haki ya kukasirika. ni kama ulimfanya kuwa mjinga na asiyejua thamani ya nyumba. kama pesa mahari ilitosha kujenga basi ni juu ya wazazi wako kuamua wakupe zawadi gani utakapoolewa. kumbuka mahari ni ya wazazi si ya wanandoa. na kimsingi haipaswi kuwa kubwa sana kwani ni kitu cha kuonyesha heshima na labda kukamlisha mila tu ili kusignify hiyari ya wazazi wa msichana kuruhusu na kubariki binti yao kuolewa. chimbuko la mahari na practice zake zaweza kuwa questionable lakini role ya mahali itaendelea kubaki kwa miaka mingi sana. mahakamani mahari yaweza kutumika kama ushahidi kuwa ndoa yenu inatambulika kimla. sasa nakushauri kawaombe msamaha wazazi wako na utakapopata mchumba fungeni ndoa na mambo ya nyumba na mengineyo mjipangie wenyewe
 
labda mzee anahisi kuwa unajibaba na wanalijuwa ila wewe hutaki kuwaeleza ukweli,pia kuhusu mnazi pombe ni kweli si unaelewa mdingi hapo ndo kimbilio lake sasa wewe wataka kuziba mrija wake ndio maana akatowa hayo aliyo yatowa

mapinduziiii daimaaaaaa:crying:
 
Ntaomba radhi leo usiku nikifika home, hope watanielewa.
ulichanganya vitu viwili hapo na babako ana haki ya kukasirika. Ni kama ulimfanya kuwa mjinga na asiyejua thamani ya nyumba. Kama pesa mahari ilitosha kujenga basi ni juu ya wazazi wako kuamua wakupe zawadi gani utakapoolewa. Kumbuka mahari ni ya wazazi si ya wanandoa. Na kimsingi haipaswi kuwa kubwa sana kwani ni kitu cha kuonyesha heshima na labda kukamlisha mila tu ili kusignify hiyari ya wazazi wa msichana kuruhusu na kubariki binti yao kuolewa. Chimbuko la mahari na practice zake zaweza kuwa questionable lakini role ya mahali itaendelea kubaki kwa miaka mingi sana. Mahakamani mahari yaweza kutumika kama ushahidi kuwa ndoa yenu inatambulika kimla. Sasa nakushauri kawaombe msamaha wazazi wako na utakapopata mchumba fungeni ndoa na mambo ya nyumba na mengineyo mjipangie wenyewe
 
Tatizo lako umezidisha u machi noo.
Bila shaka nyie ndio mnaoshinda kwenye mabotiki na masaluni makubwa wakati wazazi wenu wanavaa mguu mmoja rana na wa pili skuna kwa kukosa viatu.
Hebu weka heshima mbele na uhalisia pia.
 
Ntaomba radhi leo usiku nikifika home, hope watanielewa.

bila wasiwasi, watakuelewa na watakusamehe, na mito ya baraka na furaha itafunguliwa maishani mwako. utashangaa jinsi utakavyoijenga hiyo nyumba kirahisi hata kuliko ulivyotegemea
 
Jf kuna mengi na maoni ya kila namna.
Asante sana kwa ushauri mpendwa, ubarikiwe.
tatizo lako umezidisha u machi noo.
Bila shaka nyie ndio mnaoshinda kwenye mabotiki na masaluni makubwa wakati wazazi wenu wanavaa mguu mmoja rana na wa pili skuna kwa kukosa viatu.
Hebu weka heshima mbele na uhalisia pia.
 
Mahari ni kama zawadi tu wanayopewa wazazi walea chema,nafikiri baba ana haki ya kukasirika,mahari apewe baba na mama.
Hayo ya nyumba yawe kati yako na mwenzi wako Nazjaz, na si lazima wakati wa uchumba hata mkishafunga ndoa.
Waombe msamaha,wanakupenda watakuelewa!:smile-big:
 
Kwani utamaduni/mila mnazofuata hapo nyumbani zikoje? Kwa baadhi ya dini, mahari ni mali ya binti, na kwa mambo ya kikabila, kwa makabila mengi ninavyojua mimi, mahari wanapewa wazazi au wajomba. Sasa pima mwenyewe jinsi mlivyo hapo home kwenu.
 
Mahari ni kama zawadi tu wanayopewa wazazi walea chema,nafikiri baba ana haki ya kukasirika,mahari apewe baba na mama.
Hayo ya nyumba yawe kati yako na mwenzi wako Nazjaz, na si lazima wakati wa uchumba hata mkishafunga ndoa.
Waombe msamaha,wanakupenda watakuelewa!
Mimi binti yangu hata Uji aliokunywa kufikia alipo muoaji atacontribute
 
ehhh mi sielew apa....

mdada mleta sredi anataka apewe mahari ya matofali, faza anataka mahari yawe katika mfumo wa noti mpya zilizotoka karibuni. nazani utakuwa umeelewa? sihitaji malipo ni sadaka tu kukuelewesha.
 
Walinikalisha kuniuliza kama nimeshapata mchumba au rafiki nisisite kumpeleka nyumbani. Nikawaambia sawa nikimpata ntamleta.
Nikawailiza mahari inakuwaje kulingana na mila zetu?
Wakanitajia, nikapiga hesabu nikaona mahari inafika kama milioni moja na laki 2.
Nikawaambia wazazi wangu kuwa, kwakuwa nina shamba kisarawe, nikipata mchumba wamwambie alete matofali ya kuanzia kwa ajili ya nyumba ambayo itakuwa yangu na mume wangu.
Baba yangu alipinga na kuongea maneno yote mabaya.
Je nilikosea nini?
Au aliona namzibia hela za bakuli la komoni?
unataka akose pombe yake ya mnazi?
 
hivi kihalali mahari anapanga nani? na nihalali apewe mzazi wakati anaekwnda kuemeka ni binti ebu nipeni mwongozo kuhusu mtoa mada apo kuna mwingiliana wa kimasilai
 
Walinikalisha kuniuliza kama nimeshapata mchumba au rafiki nisisite kumpeleka nyumbani. Nikawaambia sawa nikimpata ntamleta.
Nikawailiza mahari inakuwaje kulingana na mila zetu?
Wakanitajia, nikapiga hesabu nikaona mahari inafika kama milioni moja na laki 2.
Nikawaambia wazazi wangu kuwa, kwakuwa nina shamba kisarawe, nikipata mchumba wamwambie alete matofali ya kuanzia kwa ajili ya nyumba ambayo itakuwa yangu na mume wangu.
Baba yangu alipinga na kuongea maneno yote mabaya.
Je nilikosea nini?
Au aliona namzibia hela za bakuli la komoni?

Nazjaz sorry kama nitakukwaza kwa maoni yangu haya! Kwanza ulivyo jieleza katika thread yako inaonyesha ujui thamani ya Wazazi na umeonyesha kiburi kikubwa mbele yao, kama hiyo inshu ni serious kwa upande wako au its just idea kuongeza idadi ya post sijui.Kwa kweli sikufurahi kabisa na hiyo Red Finishing statement hapo juu.Kwa Thamani ya Mzazi kwa hakika siwezi kumpresent hivyo hadharani..OK any way huyo ni wewe,labda kwa Ushauri tu,Mahari inategemea na jamii uliyopo,kuna jamii ambayo Mahari ni kama Shukran kwa Wazazi,lakini pia kuna jamii ambazo mahari ni haki ya Binti anayeolewa..sasa basi kama wewe upo katika jamii ya kwanza Mahari si haki yako na kama upo katika jamii hii ya pili ni kweli mahari ni haki yako lakini haukutumia Busara hata moja mbele ya Wazazi wako katika kuwakilisha Ombi lako la mahari zaidi ya kuonyesha kiburi...Tumia busara nenda kawaombe msamaha wazazi kama ulibishana nao katika hilo.
 
Walinikalisha kuniuliza kama nimeshapata mchumba au rafiki nisisite kumpeleka nyumbani. Nikawaambia sawa nikimpata ntamleta.
Nikawailiza mahari inakuwaje kulingana na mila zetu?
Wakanitajia, nikapiga hesabu nikaona mahari inafika kama milioni moja na laki 2.
Nikawaambia wazazi wangu kuwa, kwakuwa nina shamba kisarawe, nikipata mchumba wamwambie alete matofali ya kuanzia kwa ajili ya nyumba ambayo itakuwa yangu na mume wangu.
Baba yangu alipinga na kuongea maneno yote mabaya.
Je nilikosea nini?
Au aliona namzibia hela za bakuli la komoni?

Unataka kumkosesha ulaji, kuwa na mtoto wa kike ni dili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom