Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,293
- 18,870
Ninajaribu kuangalia maisha ndani ya familia ambapo baba wa kaya anaagiza kuwa nyama itakuwa inaliwa siku ya sikukuu tu kutokana na hali ngumu ya kipato, siku nyingine zote watakula kauzu. Halafu baba huyo huyo anakuwa ananunua nusu kilo ya nyama kila siku kwa ajili yake tu: watoto na mama wanakula kauzu, je hiyo ni sahihi? Ingawa jambo hilo inafanyika katika baadhi ya kaya zetu, siyo jambo jema na linajenga tabia mbaya kwa watoto kuwa wanafiki na waongo. Kikwete ni kiongozi wa kaya, na kwenye hili la maombolezo ya kitaifa alitakiwa aonyeshe mfano siyo kuagiza wengine waomboleze yeye asherehekee. Kuna mambo ambayo anaweza kuendelea nayo wakati wa maombolezo lakini siyo hili kwenda kushangilia timu ya taifa wakati anaomboleza; huko ni kulinafikia taifa kuwa anaomboleza huku kumbe hana taimu na maombolezo hayo; ni afadhali angesema kuwa Taifa litaomboleza kwa siku tatu tu ingeeleweka.
Nikirudi nyuma, nakumbuka kuwa rais huyu huyu aliwahi kukatisha mkutano na watanzania huko uingereza bila kujibu maswali kusudi eti akatazame mpira, halafu baadaye akapanga safari nyingine ya kurudi uingereza ili akajibu maswali aliyokwepa!!