Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Hakuna alichokosea, tuko kwenye maombolezo na shughuli zingine zinaendelea kama kawaida yeye kwenda mpira sidhani kama inahusiano wowote na maombolezo.

Jaribu kukosoa masuala ya msingi na ya tija kwa taifa letu.JK is doing good with his government bali wenye chuki binafsi ambao walidhani watakuwepo kwenye madaraka milele ndiyo wanaleta yote haya.

Mh. Rais wetu amesha tueleza tujihadhari na tuwaepuke watu wenye nia mbaya na nia ovo ya nchi yetu.
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?

Acholile kachola, "aliyekwenda amekwenda". Haina maana kuacha kuendelea na shughuli zako eti kwakuwa umefiwa.
Ndiyo maana kuna baadhi ya watu ( kabila) wakipata msiba J'tatu basi huendelea na shughuli zao mpaka weekend ndiyo mazishi yafanyike.
Aliyekwenda kaenda banaa.

R.I.P Mzee Kawawa.
 
Mwanakijiji
Nadhani unalako binafsi na JK, huu ukosoaji sasa umezidi na unakera.kama umekosa hoja bora utulie na usubiri pumba za CCM uziandikie.

kwa taarifa yako kuna watu muhim wanakufa hata huko ulaya sports inatumika kama njia moja wapo ya kujifariji, michezo si siasa, michezo ni njia moja wapo ya kujifariji.kama wewe unaona JK alikosea sijui ni wawapi wewe...naona tangu uweke picha ya JK yupo hospitali anaazindua machine pale muhimbili umekua hauna hoja.
 
kwani JK akienda uwanjani inamaanisha hakuna maombolezo ya kitaifa?
basi na mashule yafungwe kwa mpango huo.....acheni nyie watu afu bado mnajiita great thinkers.
 
Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo?

Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?

If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!

You really think this was a good business strategy?

Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:

Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?

wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!

Mkuu, umemaliza kabisa.

Sitegemei makubwa kutokana na dakika 90 za mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars na Ivory Coast katika kuitangaza nchi.

Biashara gani ambayo inatangazwa kwa kuonyeshwa kwenye TV za Taifa tu? Biashara gani hiyo ambayo ni mpaka Rais wa nchi ahudhurie ndipo inafanyika? Ni biashara gani hiyo muhimu kiasi kwamba kinachohitajika ni timu ya nchi changa kama yetu kuja na kucheza na timu yetu ndipo nchi itangazwe? C'mon guys, let's be serious.

Yaani tumefikia mahali ambapo tunaamini kuwa Rais akiwa mahali ndipo mambo yanafanyika? Sitaki kukubaliana na hili hata kidogo. Maana hata huko anakozunguka kila siku sioni anachorudi nacho nyumbani.

Uwanja wa Taifa (mpya) hauwezi kutangazwa ndani ya nchi. Kuna njia nyingi na nzuri zaidi za kuutangaza kama tunataka kufanya hivyo. Sijawahi kuona matangazo yoyote ya uwanja huo kwenye DSTv, CNN wala channels nyingine za kimataifa. Matumizi ya 7bil. inabidi yafanyiwe utafiti. Ni ya nini hasa kwa mchezo wa kirafiki? Au ni ya kumsherehesha Drogba?

Je, tulitumia kiasi gani wakati wa michuano ya kutafuta nafasi katika fainali za kombe la Afrika/Dunia? Je, tunajua vipaumbele kweli? Taifa Stars ingepewa pesa hizo hata mara moja kwa miezi mitatu, ingekuwa tofauti kabisa na ilivyo sasa. Na hapo ndipo tungekuwa tunaitangaza nchi.
 
Mwanakijiji
Nadhani unalako binafsi na JK, huu ukosoaji sasa umezidi na unakera.kama umekosa hoja bora utulie na usubiri pumba za CCM uziandikie.

kwa taarifa yako kuna watu muhim wanakufa hata huko ulaya sports inatumika kama njia moja wapo ya kujifariji, michezo si siasa, michezo ni njia moja wapo ya kujifariji.kama wewe unaona JK alikosea sijui ni wawapi wewe...naona tangu uweke picha ya JK yupo hospitali anaazindua machine pale muhimbili umekua hauna hoja.

onesha makosa ya hoja yangu acha kunishambulia. Waliohishiwa hoja wao huleta vioja!
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
he was right to go there....
 
Inaonyesha wengi humu aidha hamjui maana ya msiba wa kitaifa au ndio ule msemo wa ukipenda chongo huona kengeza. Hivi mfano ile landslide/ mudslide ya Brazil iliyoclaim 60 human lives imeitangazwa kuwa ni msiba wa kitaifa na will be mourned in 3 days, unataka kuniambia rais wa Brazil kwenda kuangalia mechi kipindi hicho ni sahihi? Hivi mlikuwa wapi wakati wa msiba wa mwalimu? Harusi ziliahirishwa, mechi kama hizi hata kuchezwa ilikuwa hakuna,baa zilikuwa kimyaaaa! Mnataka kuniambia leo hii God forbid Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini akifa, after say 2 days Zuma anaweza kwenda kuangalia mpira.

Anywayz maybe Kawawa was not that important, lakini je kulikuwa na haja gani kutangaza msiba wa kitaifa?

Tuacheni ushabiki, hapa mkulu amechemka tena big tyme.
 
Msiba wa Kawawa kwa kiasi kikubwa umekuwa tofauti sana na msiba ule wa Mwalimu. Kwenye msiba wa Mwalimu zilitangazwa siku 30 za maombolezo ya kitaifa na kwa kweli katika kipindi hicho uliweza kufeel kweli tupo kwenye Maombolezo. Nakumbuka hata ukitizama redio na televisheni za hapa nchini ulikuwa unapata feeling kwamba tunaomboleza.

Sio nia yangu kuingia kwenye mjadala wa nani ni zaidi kati ya Mwalimu na Kawawa (naamini hili lipo wazi mno). Lakini kwa hakika kwa jinsi msiba ulivyoendeshwa na namna tunavyoomboleza hizi siku saba nasita kuamini kwamba tumemtendea/tunamtendea Kawawa anavyostahili.

Nimejaribu kupitia hii thread lakini bado sijapata kinagaubaga majibu ya maswali haya:
- Rais wa Tanzania anapotangaza siku kadhaa kuwa ni za maombolezo ya kitaifa maana yake ni nini? Au kwa kifupi, Maombolezo ya kitaifa ni nini? Je tuna sheria au taratibu inayoongoza jambo hili?
- Mambo gani Rais anaweza kufanya au hawezi kufanya katika kipindi hicho (kisheria au kimaadili)?
 
Vizuri. Hoja yako ingekuwa na nguvu na wala tusingebishana kama aliyekufa hakuwa Kawawa. Unachosema ni kweli kwenye misiba yetu ya kawaida. Kawawa kwa Kikwete alikuwa ni karibu zaidi na ndugu. Vinginevyo nini kilichomfanya kutangazia taifa msiba wa kitaifa? Na kama suala la msiba wa Kawawa ni swala la familia na familia ndiyo wanatakiwa kuombeleza ni kitu gani kiliwafanya serikali kusimamia msiba na mazishi badala ya kwenda kutoa pole tu na kuondoka zao msibani? Ni kitu gani kilimgusa Kikwete kwenda asubuhi na mapema kwenda kumuona mtu asiye ndugu yake akiwa hospitali tena yeye na mkewe? Unless.. unless Kawawa hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe.. you tell me. Kwanini serikali imejihusisha kwa karibu kuanzia ugonjwa, kuaga, mazishi na hata kututangazia maombolezo? !
Mzee Mwanakijiji, Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa hili, hata kama rais ungekuwa wewe, ungewajibika kuyafanya yote hayo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Hii ya kwenye asubuhi na mapema, ni humane side ya JK. Lazima tukubali JK ni mtu wa watu, anajichanganya sana, tena nadhani urais ni kikwazo kwake otherwise angeendelea kuripoti Msondo pale Amana, kujiwe cha Saigon etc.
Hata hivyo, hili la kuwa mtu wa watu, sio excuse ya madhaifu yake judgment, kwenye issues ndogondogo tusizikuze, hakuna ubishi JK ni mtu wa avarage inteligence, hatuna sababu ya kumvua nguo hata kwenye issues zinazohitaji average common sense.
Ni nadharia ya ajabu kufikiri kuwa tutaitangaza nchi kwa mechi ya Ivory Coast! Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!! Kama lengo ni kutangaza nchi kuna njia nyingine rahisi zaidi na wala hazimuhitaji rais kuitangaza. Yaani miaka minne yote ya safari zote na kukutana na kila aina ya watu huko majuu bado hajaitangaza Tanzania na kuiuza nchi ndio ije leo kwenye mechi ya Ivory Coast?

If this was a business strategy.. then it is the most ill-thought business strategy ever! And if I had a chance to know who came up with this idea I would parade him in public and do something better left unmentioned!

You really think this was a good business strategy?

Nitakuambia kitu kingine, kama suala lilikuwa ni kutangaza uwanja kuna njia nyingine za kuutangaza.. otherwise.. nijibie swali hili:

Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?

wakati hata kona zinakabwa kama hazipigwi moja kwa moja!

Kwa hili, 'You really think this was a good business strategy?' nakiri sio eneo langu la kujidai lakini lazima tukubali kuwa kwenye bussiness strategies, Tanzania bado tuko nyuma, kazi ya kupromote use ya uwanja wa taifa kwa kombe la dunia, we are late, but better late than never.

'Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?'. Tutayapima mafanikio ya mpango huu pamoja na kujustfy its 7 Billion budget wakati wa kufanya mrejesho baada ya fainali, pia mtapatiwa hesabu za faida ya bilioni 7 mara 70 itakayozalishwa!.

'Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!!' - kwa hili nakuunga mkono, tutengeneze kina Bayi, Nyambui na Shahanga wengi kadri tuwezavyo. Miaka ya 70, tulikuwa ni sisi machampioni, Kenya wameibuka na kutuacha kama ilivyo kwenye lugha ya Kiswahili.

JK anafanya makosa mengi tuu kwa sababu hana watu wa kumwambia ukweli, waliomzunguka wengi ni wapambe, kazi yao ni kutoa nyimbo za sifa na mapambio, ila JK japo kiburi na madharau, pia kisirisiri ni msikivu, ndio maana kuna mahali nilikuambia Mwanakijiji, kama bado hujatafutwa, basi the time is near, utatafutwa simply because your too critique but sometimes constractive.
Niliwahi kusema, unawasidia sana hawa, laiti kama ungekubali kusaidia na upande wa pili kama ulivyoahidi kwenye 'Change' basi safari ndio imeanza!.

Mzee Mwanakijiji, you are Great!, sometimes hivi vitu vidogovidogo viache vipite isijeonekana its a crusade against!. Tupunguze malalamiko, turudi kwenye kupanga strategies, tufanye actions, tusonge mbele!.
 
Mzee Mwanakijiji, Kawawa ni mmoja wa waasisi wa taifa hili, hata kama rais ungekuwa wewe, ungewajibika kuyafanya yote hayo kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni. Hii ya kwenye asubuhi na mapema, ni humane side ya JK. Lazima tukubali JK ni mtu wa watu, anajichanganya sana, tena nadhani urais ni kikwazo kwake otherwise angeendelea kuripoti Msondo pale Amana, kujiwe cha Saigon etc.
Hata hivyo, hili la kuwa mtu wa watu, sio excuse ya madhaifu yake judgment, kwenye issues ndogondogo tusizikuze, hakuna ubishi JK ni mtu wa avarage inteligence, hatuna sababu ya kumvua nguo hata kwenye issues zinazohitaji average common sense.

Umesema vizuri hapo mwisho; sasa kama yeye anapenda kujichanganyachanganya na urais ni kikwazo ni bora tuendelee kupiga kelele asigombee.. the nation can not take another five years of his unleadership..(if thats a word).

Kwa hili, 'You really think this was a good business strategy?' nakiri sio eneo langu la kujidai lakini lazima tukubali kuwa kwenye bussiness strategies, Tanzania bado tuko nyuma, kazi ya kupromote use ya uwanja wa taifa kwa kombe la dunia, we are late, but better late than never.

This is not even near "late".. ni kupoteza fedha believe me.. kwani tulipowafunga Togo tulifanya nini?

'Tunapimaje mafanikio ya mpango huu wa biashara na kujua kuwa umezaa matunda?'. Tutayapima mafanikio ya mpango huu pamoja na kujustfy its 7 Billion budget wakati wa kufanya mrejesho baada ya fainali, pia mtapatiwa hesabu za faida ya bilioni 7 mara 70 itakayozalishwa!.

well.. waanze kutuambia kwanza mafanikio ya bilioni 21 za "Kikwete"..na halafu watupe faida ya stimulus package of 1.6 trillioni ~

'Nitasuggest njia nyepesi.. support riadha!!!' - kwa hili nakuunga mkono, tutengeneze kina Bayi, Nyambui na Shahanga wengi kadri tuwezavyo. Miaka ya 70, tulikuwa ni sisi machampioni, Kenya wameibuka na kutuacha kama ilivyo kwenye lugha ya Kiswahili.

sasa kama mimi nawewe tunaweza kuona hili huyo JK hawezi kuliona. Hivi bilioni 7 zingeingizwa kwenye riadha zingeenda mbali kiasi gani kuitangaza nchi?

JK anafanya makosa mengi tuu kwa sababu hana watu wa kumwambia ukweli, waliomzunguka wengi ni wapambe, kazi yao ni kutoa nyimbo za sifa na mapambio, ila JK japo kiburi na madharau, pia kisirisiri ni msikivu, ndio maana kuna mahali nilikuambia Mwanakijiji, kama bado hujatafutwa, basi the time is near, utatafutwa simply because your too critique but sometimes constractive.

tatizo la mtu kama mimi nitaambiwa nataka kuchukua kibarua cha mtu!.. kwa sababu ushauri wangu wa kwanza utakuwa ni kufukuza watu wengi kweli!! So it is not to their interest to approach me unless they want real change that will lead us into a real path of prosperity.

Niliwahi kusema, unawasidia sana hawa, laiti kama ungekubali kusaidia na upande wa pili kama ulivyoahidi kwenye 'Change' basi safari ndio imeanza!.

LOL

Mzee Mwanakijiji, you are Great!, sometimes hivi vitu vidogovidogo viache vipite isijeonekana its a crusade against!. Tupunguze malalamiko, turudi kwenye kupanga strategies, tufanye actions, tusonge mbele!.

mzee hiki kwangu ni kitu kidogo sana.. tatizo lake ni implication yake. Sehemu yake ya pili ambayo kwangu ni muhimu zaidi ninamalizia kuandika sasa kwa ajili ya Tanzania Daima la J'tano.
 
sometimes naamini kabisa washauri wa JK wanampotosha makusudi...
 
Mimi nilishikwa na butwaa mkuu na kujiuliza huyu bwana kweli msanii wa bagamoyo;
kwa hali hii ata akifa nani watu wanaangalia mbele kuna nini
kazi kweli
 
Halafu waziri wake huyuhuyu rais wao
ati anatangaa uma wanataka kuleta brazil kwa billion 7
hapo zingine ziikajengee bandari ya bagamoyo loh ccm ile
 
JK , hawezi kusubiri kuja kusimuliwa eti Drogba alipiga bao pale, lazima aende akashuhudie.

Kama anaweza kufunga safari kwenda kupiga picha na Boys 2 men , la drogba ulitaka afanye nini zaidi?Sijui hata kama alikumbuka kufunga kitambaa cheusi....
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?

MwanaKijiji,
Lord have mercy! If this is indicative of your new-year resolutions for 2010 and the direction you are planning to lead your dutiful and loyal JF subjects, this could prove to be a long and arduous year for the rest of us! It is a bad omen, to state the obvious, for someone of your stature to choose such a solemn event and awkward moment to take potshots at the President. You are strength and credibility as a political observer and commentators that you have rightfully earned is enhanced when you focus on giving impartial and unbiased views about the prevailing political climate in Tanzania. Hitting below the belt, unfortunately, has the opposite effect.

I was hoping you would continue your “trademark” incisive remarks in this forum and also praying that you will maintain your lucid and insightful contributions on the bread and butter issues that most Tanzanians care about, such as the war on corruption in government and your virtually unparalleled and unmitigated passion for good governance and transparency. I am now seriously worried that I may not get the answers to my prayers.

The notion that life has to come to a screeching halt when the nation is mourning is as disingenuous as it is ridiculous. A minute of silence was observed at the soccer game in honor of the late Vice President and that should be plenty considering that we are still observing a 7 day mourning period. I don’t expect the late Kawawa’s widow or children to go to the ballgame any time soon or even after the traditional 40-day mourning period since, as you know, the family will bear the heavy burden and weight of the pain and grief for many months and year to come. But the President cannot allow the luxury of nursing grief (important as it is) to incapacitate or render him helpless. He is the leader of nation after all and has important and essential duties to fulfill. He has to keep going.

We know this is an election year and so to expect the unexpected is sage advice and a necessary skill to help endure the journey. Every weapon available in the political arsenal can and will be used against politicians especially the President. But to take a swipe at him (or any other government leader for that matter) for attending an international soccer match knowing that he was fully involved in most if not all the key activities surrounding the late Vice Presidents funeral, is just beyond the pale. When you make these types of comments, you run a much greater risk of slipping into irrelevance as we enter this election year.
 
Msiba wa Kawawa kwa kiasi kikubwa umekuwa tofauti sana na msiba ule wa Mwalimu. Kwenye msiba wa Mwalimu zilitangazwa siku 30 za maombolezo ya kitaifa na kwa kweli katika kipindi hicho uliweza kufeel kweli tupo kwenye Maombolezo. Nakumbuka hata ukitizama redio na televisheni za hapa nchini ulikuwa unapata feeling kwamba tunaomboleza.

Sio nia yangu kuingia kwenye mjadala wa nani ni zaidi kati ya Mwalimu na Kawawa (naamini hili lipo wazi mno). Lakini kwa hakika kwa jinsi msiba ulivyoendeshwa na namna tunavyoomboleza hizi siku saba nasita kuamini kwamba tumemtendea/tunamtendea Kawawa anavyostahili.

Nimejaribu kupitia hii thread lakini bado sijapata kinagaubaga majibu ya maswali haya:
- Rais wa Tanzania anapotangaza siku kadhaa kuwa ni za maombolezo ya kitaifa maana yake ni nini? Au kwa kifupi, Maombolezo ya kitaifa ni nini? Je tuna sheria au taratibu inayoongoza jambo hili?
- Mambo gani Rais anaweza kufanya au hawezi kufanya katika kipindi hicho (kisheria au kimaadili)?

Hata 1984 Sokoine alipokufa maombolezo yalikuwa mwezi mzima (30 days). Kipindi kile ulikuwa huruhusiwi hata kupiga muziki kwa nguvu nyumbani kwako, kuna watu nasikia walikuwa arrested kwa hili. Nakumbuka hata Mdisco, cinema vyote vilipigwa marufuku. That time nilikuwa form one, nakumbuka disco letu lliliahirishwa kwa sababu hiyo.

Those were the days. Sasa mambo yamebadilika ila la Mh. kwenda kwenye mpira inawezekana ikawa little bit too much. May be wenye picha watuletee inawezekana alienda pale ili apige picha na akina Drogba!
 
Msiba wa Kawawa kwa kiasi kikubwa umekuwa tofauti sana na msiba ule wa Mwalimu. Kwenye msiba wa Mwalimu zilitangazwa siku 30 za maombolezo ya kitaifa na kwa kweli katika kipindi hicho uliweza kufeel kweli tupo kwenye Maombolezo. Nakumbuka hata ukitizama redio na televisheni za hapa nchini ulikuwa unapata feeling kwamba tunaomboleza.

Sio nia yangu kuingia kwenye mjadala wa nani ni zaidi kati ya Mwalimu na Kawawa (naamini hili lipo wazi mno). Lakini kwa hakika kwa jinsi msiba ulivyoendeshwa na namna tunavyoomboleza hizi siku saba nasita kuamini kwamba tumemtendea/tunamtendea Kawawa anavyostahili.

Nimejaribu kupitia hii thread lakini bado sijapata kinagaubaga majibu ya maswali haya:
- Rais wa Tanzania anapotangaza siku kadhaa kuwa ni za maombolezo ya kitaifa maana yake ni nini? Au kwa kifupi, Maombolezo ya kitaifa ni nini? Je tuna sheria au taratibu inayoongoza jambo hili?
- Mambo gani Rais anaweza kufanya au hawezi kufanya katika kipindi hicho (kisheria au kimaadili)?

SMU,

Uchambuzi wako ni mzuri na maswali uliyouliza ni ya msingi sana.
iNAONEKANA kama vile maombolezo yameisha. Tusipokuwa waangalifu mzee wetu huyu atasahaulika mapema sana. Kuna mtu amependekeza TBC pia iwe inatoa sehemu ya hotuba zake kila wiki kama wafanyavyo kwa Mwalimu kupitia kipindi cha Wosia wa Baba. Kwa upande wa Mzee Kawawa wanaweza kukiita kipindi hicho kwa jina la NASAHA ZA SIMBA WA VITA. Naamini TANAPA watakuwa tayari kukithamini.
 
Ninavyojua muungwana yuko mapumzikoni, na kama mwananchi na mpenda michezo kuna ubaya gani naye kwenda kuangalia mechi? Hakuwa mgeni rasmi, bali alienda kama mpenzi yeyote wa michezo, japo kwa vile ni kiongozi (taratibu zingine za kutawala lazima zifuatwe). Mbana Obama anakula ice cream na wanawe jamani kwao ?
 
Back
Top Bottom