Maombi ya Rais Samia Yajibiwa, Tanzania Yachaguliwa Kuwa Makao Makao Sekretarieti ya Baraza la Michezo Afrika Kanda ya IV

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana anayofuraha kuwajulisha Watanzania kuwa kikao cha Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya IV Nazi ya Mawaziri kimeichagua Tanzania kuwa Mako Makuu ya Sekretarieti ya Baraza hilo.

Aidha, wajumbe wa mkutano wameazimia kuwa mkutano ujao utafanyika hapa nchini huko Zanzibar mnamo mwezi Aprili 2024 ikiwa ni mkutano wa pili wa Baraza hilo.

Hayo yote yamewezekana kutokana na utayari wa nchi yetu kuanzia Viongozi Wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia salamu zake alizowasilisha wakati wa mkutano kwa njia ya mtandao kwa wajumbe wa mkutano pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyewaomba kura wajumbe hao wakati wa mkutano huo.

Pia mkutano huo umefanya marekebisho ya Katiba yake ili kuongeza ufanisi kwa kuboresha kukuza na kuendeleza michezo miongoni mwa nchi wanachama ambazo ni Comoro, Djibouti Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Mauritius, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Seychelles na Uganda.

Screenshot 2023-05-05 at 21.48.50.png
 
Back
Top Bottom