Maombi rasmi kwa ajili ya Taifa kabla ya kulala

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,990
37,053
Mungu baba , Muumba mbingu na ardhi. Unayetujua sisi sote, mwenye nguvu na mamlaka yote.

Ninaomba toba na rehema kwaajili ya Tanzania na Watanzania.

Mungu tusamehe pale tulipochukiana na tukasahau Utanzania wetu kwasababu za kisiasa, kidini, kikabila na hata kwasababu za kipato.

Mungu ninaomba kutoka moyoni, utupe mioyo yenye kukuogopa wewe, na tujue kuwa wewe uko kila mahali, unaweza kila jambo na unayajua mambo yote hata yale tuliyoyashikilia sirini.

Eeeehhh Mungu ninaomba utupe moyo safi kama Watanzania na uzikemee roho zetu zinapotamani kuinuka huu yetu.

Ikiwa kuna Mtanzania yeyote alimwaga damu ya Mtanzania mwenzake(ndugu) eeehhh Mungu umkumbushe kutubu usiku huu, naye akitubu msamehe, naye akifanya moyo mgumu mvune haraka kwa mkono wako.

Amina.
 
Hapa mwishoni unapomtaka Mungu amvune mtu mwenye moyo mgumu ndio unaharibu sala. Omba amlainishe moyo au ampe neema ya kutubu. Mungu havuni waovu, huvuna walio wema kwani hao ndio huenda mbingun i.
 
Hapa mwishoni unapomtaka Mungu amvune mtu mwenye moyo mgumu ndio unaharibu sala. Omba amlainishe moyo au ampe neema ya kutubu. Mungu havuni waovu, huvuna walio wema kwani hao ndio huenda mbingun i.
Nimeandika amkumbushe kutubu, naye akipuuza basi amtwae. Yeye huvuna kisha mbele huchambua ngano na magugu
 
Eeh Mungu awalaani na kuwapiga kwa gadhabu yako kali wote waliotaka kumuu Lissu, waliomua Ben saanane, waliompoteza Azory na wote walioshiriki kumuua Aquilin, Baba uwalaani na kuwapatiliza wo na watoto wao na vizazi vyao laana ya milele waliomuua Katibu John wa hananasifu , Luena, kanguye. Uwapige na maradhi ya kudumu yasiyotibika waliomteka Roma, Mdude Nyangali na Neywa Mitego.

Baba sisi hatuna nguvu za kupambana nao bali wewe muumba wa vitu vyote ututete. Amina.
 
Back
Top Bottom