Rais Samia atakapostaafu Urais 2030 atakumbukwa sana na Watanzania kwa mema aliyolitendea Taifa letu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,326
9,748
Ndugu zangu watanzania,

Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu, Rais wetu Samia atakapokuwa anastaafu na kumaliza muda wake wa kulitumikia Taifa letu mwaka 2030, kwa hakika atakumbukwa sana na Watanzania kwa mema na makubwa aliyolitendea Taifa letu.

Naawaambieni ukweli watanzania wenzangu Rais Samia atakumbukwa na watu wa rika zote, Dini zote, vyama vyote vya siasa, makabila yote, kanda zote, jinsia zote na mikoa yote, nawaambie haya waziwazi na mtakuja mkumbuke maneno yangu, hata wanaompinga kwa sasa natambua watakuja kutamani arejee tena madarakani.

Kupata Samia mwingine mwenye mapenzi mema na Taifa, mwenye moyo wa upendo, huruma, ucha Mungu, hofu ya Mwenyezi Mungu, hekima, busara, usikivu, unyenyekevu, uungwana, utu, uzalendo ni shughuli, siyo jambo jepesi.

Wenye moyo kama alionao Rais Samia ni wachache ndugu zangu, wenye kifua na uwezo wa kukaa na mpinzani mezani au msikitini au kwenye dhifa ya kitaifa Ni wachache ndugu zangu, hawazaliwi kila siku.

Kupata Rais Samia mwingine mwenye kujua cheo ni dhamana, mwenye kujua uongozi unatoka kwa Mungu, mwenye kujua vyeo, mamlaka na madaraka ni vya kupita, mwenye kujuwa kuwa uongozi ni utumishi kwa watu ni wachache sana na itatubidi kuwa makini sana katika kumtafuta na kumpata Samia mwingine wa kuendeleza atakapo kuwa ameishia Rais Samia halisia.

Jiulizeni wangapi wenye uvumilivu na kifua alichonacho Rais Samia? Jiulizeni ni wangapi mmewashuhudia na tumewaona wakiwa wenye hasira kali na jaziba kali wakikosolewa au kuambiwa ukweli?

Kama wanakuwa wakali, wenye hasira, jazba, visasi na chuki kwa wakosoaji wao angali hawana madaraka na mamlaka ya Urais vipi siku wakipata Urais na kuwa na mamlaka yote ya Urais? Watawavumilia wapinzani wao? Watakubali wakosolewe? Jibu ni hapana ndugu zangu.

Kumpata Rais Samia mwingine mwenye uwezo wa kumyooshea kila mtu mkono wa heri na amani siyo jambo jepesi, inatupasa kumuomba Mwenyezi Mungu atuinulie mtu wa aina hiyo bila kujali umaarufu wake au familia yake au kipato chake ili aje aendeleze umoja na mshikamano wa Watanzania, upendo na umoja wakitaifa uliopo kwa sasa, uzalendo na utu kwa watu na Taifa letu.

Rais Samia atakumbukwa sana kwa alama za kiuongozi alizoziweka na kuziacha kila eneo na kila mahali. Atakumbukwa kwa kuwajali Watanzania na kulipenda kwa dhati Taifa letu. Atakumbukwa kwa kuliletea heshima Taifa letu, kuvutia wawekezaji na watalii kutoka katika kila pembe ya Dunia, kuleta na kujenga uchumi jumuishi unao mgusa kila mtanzania.

Atakumbukwa kwa kuiweka Tanzania katika jicho la ulimwengu katika nchi yenye amani na utulivu. Atakumbukwa kwa kuifaya Tanzania kuwa nchi ya ndoto kwa kila mtalii na muwekezaji.

Kikubwa Watanzania tuendelee kumwombea sana Rais wetu, tuendelee kumwomba Mungu amlinde, kumpigania na kumtetea Rais wetu, tumwombe Mungu amjalie maarifa na njia ya kuliongoza Taifa letu, ampatie wasaidizi wema wenye upendo na uzalendo kwa Taifa letu.

Nawapongeza viongozi wote kuanzia makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Baraza lote la Mawaziri pamoja na Wakuu wetu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kazi kubwa na ya kutukuka wanayoifanya katika kumsaidia Mh. Rais na kulitumikia Taifa letu kwa uzalendo mkubwa sana.

Nawapongeza Watanzania wenzangu kwa kuendelea kumwamini Mh. Rais na kumuunga mkono katika juhudi zake za kulijenga Taifa letu litakalokiwa bora na lenye kutiririsha fursa za kila aina.

Tuendelee kuwa bega kwa bega na Rais wetu na kusimama naye alipo. Asante kwa bunge letu kwa kuendelea kutoa ushauri chanya wa kumsaidia Mh Rais na serikali yake katika kesho iliyo njema kwa Taifa letu.

Kazi iendeleee, Rais ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Ndugu zangu watanzania,

Panapo Majaliwa ya Mwenyezi MUNGU Rais wetu mama Samia suluhu Hassani atakapokuwa anastaafu na kumaliza muda wake wa kulitumikia Taifa letu mwaka 2030, kwa hakika Atakumbukwa Sana na watanzania kwa mema na makubwa Aliyolitendea Taifa letu.

Naawaambieni ukweli watanzania wenzangu Rais Samia Atakumbukwa na watu wa Rika zote,Dini zote,vyama vyote vya siasa, makabila yote,Kanda zote,jinsia zote na Mikoa yote ,nawaambie haya waziwazi na mtakuja mkumbuke maneno yangu,hata wanaompinga kwa Sasa Natambua watakuja kutamani arejee Tena madarakani.

Kupata Samia mwingine mwenye mapenzi mema na Taifa,mwenye moyo wa upendo ,huruma,ucha Mungu,hofu ya Mwenyezi MUNGU,hekima ,busara,usikivu, unyenyekevu,uungwana,utu,uzalendo Ni shughuli ,siyo Jambo jepesi ,wenye moyo Kama alionao Rais Samia ni wachache ndugu zangu,wenye kifua na uwezo wa kukaa na mpinzani mezani au msikitini au kwenye dhifa ya kitaifa Ni wachache ndugu zangu, hawazaliwi kila siku.

Kupata Rais Samia mwingine mwenye kujuwa cheo Ni dhamana,mwenye kujuwa uongozi unatoka kwa Mungu,mwenye kujuwa vyeo ,mamlaka na madaraka Ni vya kupita, mwenye kujuwa kuwa uongozi Ni utumishi kwa watu Ni wachache Sana na itatubidi kuwa makini Sana katika kumtafuta na kumpata Samia mwingine wa kuendeleza atakapo kuwa ameishia Rais Samia halisia.

Jiulizeni wangapi wenye uvumilivu na kifua alichonacho Rais Samia? Jiulizeni Ni wangapi mumewashuhudia na tumewaona wakiwa wenye hasira Kali na jaziba Kali wakikosolewa au kuambiwa ukweli? Kama wanakuwa wakali ,wenye hasira ,jazba ,visasi na chuki kwa wakosoaji wao angali hawana madaraka na mamlaka ya Urais vipi siku wakipata Urais na kuwa na mamlaka yote ya Urais? Watawavumilia wapinzani wao? Watakubali wakosolewe? Jibu Ni hapana ndugu zangu.

Kumpata Rais Samia mwingine mwenye uwezo wa kumyooshea kila mtu mkono wa heri na amani siyo Jambo jepesi ,inatupasa kumuomba Mwenyezi MUNGU atuinulie mtu wa Aina hiyo bila kujari umaarufu wake au familia yake au kipato chake ili aje aendeleze umoja na mshikamano wa watanzania,upendo na umoja wakitaifa uliopo kwa Sasa, uzalendo na utu kwa watu na Taifa letu.

Rais Samia Atakumbukwa Sana kwa Alama za kiuongozi alizoziweka na kuziacha kila eneo na kila mahali,Atakumbukwa kwa kuwajali watanzania na kulipenda kwa dhati Taifa letu, Atakumbukwa kwa kuliletea heshima Taifa letu,kuvutia wawekezaji na watalii kutoka katika kila pembe ya Dunia, kuleta na kujenga uchumi jumuishi unao mgusa kila mtanzania,Atakumbukwa kwa kuiweka Tanzania katika jicho la ulimwengu katika nchi yenye amani na utulivu,Atakumbukwa kwa kuifaya Tanzania kuwa nchi ya Ndoto kwa kila mtalii na muwekezaji.

Kikubwa watanzania Tuendelee kumwombea Sana Rais wetu, Tuendelee kumwomba Mungu amlinde ,kumpigania na kumtetea Rais wetu,tumwombe Mungu amjalie maarifa na njia ya kuliongoza Taifa letu,ampatie wasaidizi wema,wenye upendo na uzalendo kwa Taifa letu.nawapongeza viongozi wote kuanzia makamu wa Rais ,Waziri mkuu,Baraza lote la mawaziri pamoja na wakuu wetu wa vyombo vya Ulinzi na usalama kwa kazi kubwa na ya kutukuka wanayoifanya katika kumsaidia mh Rais na kulitumikia Taifa letu kwa uzalendo mkubwa Sana.

Nawapongeza watanzania wenzangu kwa Kuendelea kumwamini mh Rais na kumuunga mkono katika juhudi zake za kulijenga Taifa letu litakalokiwa Bora na lenye kutiririsha fursa za kila aina, Tuendelee kuwa bega kwa bega na Rais wetu na kusimama naye Alipo. Asante kwa bunge letu kwa Kuendelea kutoa ushauri chanya wa kumsaidia mh Rais na serikali yake katika kesho iliyo njema kwa Taifa letu.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Lucus msambwanda unawaaibisha watu wa nyanda za juu kusini kwa kitangaza njaa hadharani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda ndio rafiki wakwelii nazani muda utaongea kuliko ww ulivyoandikaa hapaa...


Ngoja tuonee mwisho wa picha hili la mama SAMIAA...
 
Back
Top Bottom