Maombi: Dini mbalimbali, kabila tofauti ndani ya Tanzania, tuungane kwa umoja kuomba Mungu atuepushe na ugonjwa wa Corona

Mr Big

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
479
922
Wakuu nawasalim,

Ni dhahiri kwa sasa kila pande ya dunia ugonjwa wa corona madhara yake yamekuwa makubwa zaidi na kila nchi inajaribu kupambana kwa uwezo wake wote ilimradi tu kuuondoa au kupunguza madhara ya huu ugonjwa.

Idadi ya vifo ni vingi zaidi, licha yakuwa taarifa zinazotolewa na baadhi ya serikali za nchi husika zinajaribu kuficha idadi kamili ya vifo.

In general hadi sasa ugonjwa huu haujapata Tiba, japokuwa jitihada mbali mbali bado zinaendelea kufanywa na wataalam wa mataifa husika kupatikana kwa dawa au kinga. Sina hakika kama Tanzania nayo inafanya utafiti wa dawa kwa virus hivi!!

Tanzania
Kwa upande wetu kama taifa, leo mheshimiwa Waziri wa Afya, amethibitisha wazi Tanzania haina uwezo wakupambana na ugonjwa huu pale endapo utaingia.

Tukitazama mataifa makubwa yanavyohangaika kupambana na huu ugonjwa tunaona wazi kwa uhalisia africa kiukwel hatuna huo uwezo wakuhimili mikikimikiki ya huu ugonjwa.

Je, msaada wetu na tegemeo letu kwasasa liko wapi?

Ni vyema kwa wakati huu baada ya kupokea taarifa hizi za serikali, kuthibitisha wazi kuwa taifa halina uwezo kupambana na ugonjwa huu wa Covic19.

Nadhani ni jambo jema kwa Viongozi wa dini mbali mbali, wananchi wote wa Taifa la Tanzania, uandaliwe mkutano mkubwa kwa ajiri ya maombi utakaoshirikisha Taifa zima ili kuomba rehema, Mungu atuepushe na huu ugonjwa.

Kwakuwa tukae tukifahamu Africa ina matatizo mengi sana, endapo ugonjwa huu utaingia basi africa itakuwa imepata pigo kubwa sana ambalo halijawahi kushuhudiwa katika dunia. Vifo vitakuwa vingi zaidi yawezakuwa mara mbili au zaid ya maafa wenzetu wanayoyapata.

Lakini naamini wazi Mungu yupo, na sote tunatambua kwake yeye hakuna linaloshindikana. Tukisimama kwa pamoja kwa kumaanisha basi huu ugonjwa tutabaki kuusikia tu.

Corona virus symptoms.jpeg

Nawasilisha
 
Hakika Mungu wetu wa kweli muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake ni jibu, 🙏✅
 
Back
Top Bottom