Investigation Unit
Senior Member
- Nov 26, 2023
- 164
- 223
Moja kwa Moja kwenye mada,
Hapana Nakonde Zambia hali ni mbaya, Ugonjwa wa Kimeta unapukutisha watu na mifugo,
Watu wanaopenda kulà nyama na wanaoishi mikoa ya Rukwa,Mbeya na Songwe kuweni makini sana na ugonjwa huu unaua tena kwa kasi zaidi ya Korona.
Ukila nyama ya mnyama mwenye ugonjwa huu na wewe utakuwa katika hatari ya kupata ugonjwa huu.
Dalili za huu ugonjwa mtu anakuwa kama kamwagiwa maji ya moto na anaanza kuvuka ngozi hakika huu ugonjwa ni wahatari sana.
Kulingana na WHO, kesi 26 kati ya 60 zinazoshukiwa nchini Zambia zinatokana na "ulaji wa nyama iliyochukuliwa kutoka kwa mizoga ya viboko, ngo'mbe na Mbuzi.
Shirika hilo limeonya juu ya hatari "kubwa" ya ugonjwa wa Kimeta kuenea katika nchi jirani hasa Tanzania, kutokana na "mienendo ya mara kwa mara (ya kuvuka mpaka) ya watu na wanyama."
Kando na Zambia, Kenya, Malawi, Uganda na Zimbabwe pia zimerekodi visa vya Kimeta mwaka huu, na jumla ya vifo 20 na visa vingine 1,100 vinavyoshukiwa.
Naziomba mamlaka za Tanzania hasa Waziri wa mifugo na yule wa Afya kuhakikisha anachukua tahadhari zote kupambana na ugonjwa hasa katika mikoa ya pembezoni na iliyo mipakani mwa Tanzania na Zambia,
Ugonjwa huu hauna tiba thabiti mpaka sasa ila unatokomezwa kwa kuwapa chanjo mifugo kama kitimoto, ngo'mbe, Mbuzi, Punda etc
#Kila mmoja chukua tahadhari maisha ni mali yako sio ya Serikali.
Mungu ibariki Tanzania na walaji wote wa nyama.
Cc: Waziri Ummy Mwalimu,
Waziri Ulega
Waziri Mkuu,