Manyara: RC Munyeti apiga marufuku umoja wa watu wa Kilimanjaro mkoani kwake

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,425
RC wa Manyara, Alexander Mnyeti amefuta kikundi cha watu wa Kilimanjaro waishio Manyara. Wiki chache zilizopita alikifuta kikundi cha watu wa mkoa wa Mara waishio Manyara. Amesema ataendelea kuvifuta vikundi/vyama vyote vya watu kutoka mikoa mingine waishio Manyara kwa sababu havina faida kwa mkoa huo na vinaendekeza ukabila. Ameshauri viundwe vikundi vya jamii za watu wa Manyara kama Wairaq, Wafyomi, Wamassai etc.


Swali : Kwa kadri ya kumbukumbu ya mwanaJF unayesoma uzi huu , vikundi kama hivi vya kuzikana viliwahi kuleta madhara yoyote mahali popote ?

MAONI YA WADAU



Mwaka 2007, Prof. Rwekaza Simpho Mukandala, alifuta vyama kama hivi UDSM. Miongoni mwa vyama hivyo ni KAGERA UNIVERSITY STUDENTS ASSOCIATION (KAUSA) kilikuwa kikubwa mno nami nilikuwa kiongozi.


Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu umoja huu una msaada sana sitasahau kipindi flani nilipata matatizo nikiwa mkoa flani nikaja kusaidiwa na Umoja Wa watu wanaoishi ule mkoa....tuchukulie vitu positively wazee sio kila kitu tunawaza mabaya tu
Mnafanya umoja kimagroup sasa , au kimtaa, mpak inafikia hatua ya chama kinarun mkoa mzima na mnaitisha kikao cha mkoa , si hatar hyo...alaf manyara sio far from Kilimanjaro , ni useles kutengeneza chama cha namna hiyo tena Kwa ukubwa huo , angalau ingekuwa Songea au katavi huko hapo inaweza ikamake sense , japo bado ni very dangerous
 
Angefatilia zaidi asili na lengo la hivyo vyama, kwa haraka haraka wachaga wametapakaa sana Tanzania, na katika taratibu za mazishi ni lazima wazikwe makwao hapo kuna gharama ambazo wanachama wanachangia kwenye hivyo vyama kupunguza makali kwa wafiwa.

Kuwezesha kusafirisha miili ya marehemu, sidhani kama vyama vya wachaga vina ajenda nyingine tofauti na kuzikana.
Huku dodoma kuna kimoja kinaitwa UWAKA hichi kililenga kanda ya kaskazini kote ila yeyote anaweza kujiunga, na shuhughuli kubwa ni kuzikana.
 
Umewahi ku experience madhara yoyote ya vikundi vya namna hii ?
 
Mkuu umoja huu una msaada sana sitasahau kipindi flani nilipata matatizo nikiwa mkoa flani nikaja kusaidiwa na Umoja Wa watu wanaoishi ule mkoa....tuchukulie vitu positively wazee sio kila kitu tunawaza mabaya tu
Nakumbuka Kuna siku kulikuwa na harusi imetangazwa ya mchaga kanisani .Mzee wa kanisa akamwomba mchungaji aongee Ana neno.Mchungaji akamwambia sema akasema wachaga wote wa Kilimanjaro waliomo mule kanisani wakutane baada ya ibada ili waongee namna ya kufanikiwa Harusi ya mwenzao.

Mchungaji niliona kabadilika uso kawa mwekundu akafoka kanisani akasema kanisani hakuna Cha myahahudi Wala myunani Wala mchaga wote Ni Wana wa Mungu.Akafuta Hilo tangazo na kupiga marufuku vyama vya kikabila viwe vya kufa na kuzikana kanisani .

Akauliza hivi akiwemo Mmakonde humu kanisani ambaye kabila yake Yuko peke yake akitaka kuoa au kuolewa asaidiwe na Nani? Tukiendekeza huu ujinga wa vikundi vikundi vya kikabila kanisani?

Ukabila haufai sehemu za jumuiya za mchanganyiko wa makabila mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…