Maendeleo ya watu au vitu?

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Ni hoja ambayo imegeuzwa na Wanasiasa kama mtaji wa kisiasa na huenda ikatumika kama agenda kuu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kuna dalili ya kuelekea huko kutokana na jinsi Wanasiasa wanavyotafsiri taarifa ya Benki ya Dunia kuitambua Tanzania kama moja ya nchi yenye Kipato cha Kati.

Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?

UPDATE
Hatimaye wananchi wapenda maendeleo, kwa maana ya "VITU", wamethitisha hilo kwenye sanduku la kura.
 
Yanategemeana bila kujenga barabara miji itapanuka polepole bila kuwa umeme wakutosha kukiwa na migao ya umeme unarudisha biashara zinazotumia umeme nyuma watu wanakosa mapato bila hospitali watu wanaishi kwa afya mbovu bila miradi ya maJi watu wanapoteza muda kupata maji na kufikiria anapata wap maji ya kutumia badala ya kuwaza mawazo ya kimaendeleo au kufanya na hii miradi inasaidia pia kukuza ajira sababu waendeshaji ni sisi sisi wa tz hii ni mada chonganishi kutoka kwa wapinzani ila ukikaa chini ukawaza inasaidia sana ni nyenzo za kimaendeleo
 
Watu wanataka pesa mfukoni(maendeleo ya watu) ,hata ukijenga lami hadi mlangoni,flyover hadi kushukia sebuleni etc kama watu hawana fedha, mzunguko hovyo wa pesa kamwe watu hawawezi kukukubali.

Watu wakiwa na Mpunga usipowajengea barabara watajiorganise na kujenga hata ya moramu ,usipowaleta umeme kwakuwa wana fedha wataweka solar,usipowaleta maji kwakuwa wana fedha mifukoni watanunua bolzer au watachimba visima!!!
 
Ashukuru tume ya uchaguzi na Polisi vyote ni mali yake. Kinyume na hapo, majibu angeyapata hiyo Oktoba.

Angefahamu kama wapiga kura ni zile bombadia zake, flyovers, stiglers gorge, au ni hawa Watanzania wanaohitaji kuendesha maisha yao pasipo na msongo wowote ule wa mawazo na uliosababishwa na maisha magumu.
 
Ni hoja ambayo imegeuzwa na Wanasiasa kama mtaji wa kisiasa na huenda ikatumika kama agenda kuu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kuna dalili ya kuelekea huko kutokana na jinsi Wanasiasa wanavyotafsiri taarifa ya Benki ya Dunia kuitambua Tanzania kama moja ya nchi yenye Kipato cha Kati.

Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?
Maendeleo ya watu, huleta mahitaji ya vitu! Maendeleo ya vitu badala ya watu, tutakuwa kama North Korea!
 
Chige kaja na dhana ya microeconomics vs macroenomics ambayo kiasi inashabiana na hiyo yako jmushi1.

Kwa nadharia yako jmushi1 iliyo kwenye bandiko lako (maendeleo ya watu huleta au huchochea maendeleo ya vitu), bado kutakuwa na maswali ya msingi:

• Nini maendeleo ya watu yatakayochochea maendeleo ya vitu

• Je, maendeleo ya vitu yanaweza kuchochea maendeleo ya vitu?

√ Kuna utenganifu/mipaka gani kati ya maendekeo ya watu na vitu?
 
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu. Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana. Na ndio hasa yanayofanya watu wafanye kazi kwa bidii ili wabadilishe mazingira yao na kuitawala dunia. Maisha yamekuwa rahisi zaidi kuliko karne kadhaa zilizopita kwasababu ya maendeleo ya vitu yaliyoletwa na vumbuzi kadhaa.

Kwahiyo hatuwezi kuyakataa moja kwa moja. Jambo la msingi la kujadili hapa pengine ni jinsi gani tutawekeza kwa watu ili hayo maendeleo wajiletee wao wenyewe badala ya kutegemea watu wengine. Hapa tunazungumzia intellectual + moral development kwa watu wetu. Kama nchi kwa kiwango kikubwa bado ni tegemezi.

Bidhaa nyingi ambazo tunazo katika nchi yetu hatujazalisha sisi wenyewe na hatuna technologia ya kufanya hivyo. Bado ni tegemezi kwa kiwango cha juu kwenye masuala ya technologia kwahiyo tunahitaji kuwekeza kwa watu ili wawe na skills za kutosha ili walete hayo maendeleo ya vitu kutokana na intellectual capability zao. Nadhani huu ndio msingi wa kujitegemea kama nchi na ndio msingi wa kuwekeza kwa watu na maendeleo ya watu. Na Elimu yetu inapaswa kujengwa katika mtizamo huo.

Watu hawajaendelea kama hawawezi kujenga madaraja kwa kutumia watu wao wenyewe, kujenga reli kwa kutumia watu wenyewe, ndege kwa kutumia watu wao wenyewe, barabara, bunduki na vifaa vya kijeshi kwa kutumia watu wao wenyewe na mambo mengine mengi wanayotumia kwa maisha yao wenyewe ya kila siku. Tunapima uwezo wa nchi na maendeleo yake kwa uwezo wa raia wake kutengeneza vitu wanavyotumia kila siku na sio kutumia wasichozalisha.

Kuna kauli inazungumzwa na watu nchi yetu ni tajiri ina mali ghafi wanasahau kwamba ili malighafi iwe mali ugunduzi wa vitu unatakiwa ufanyike. Petroli bila ugunduzi wa magari isingekuwa na thamani. Gunduzi ndio zinazofanya malighafi kuwa mali. kwa mantiki hiyo tusidhani kwamba malighafi zetu zitatufaidisha zaidi ya wale waliofanya malighafi kuwa mali, waliofanya malighafi kuwa mali ndio wenye nguvu zaidi. Katika uhalisia wake malighafi haiwezi kuwa mali pasipo gunduzi. Tusipokuwa na aina hii ya fikra tusitegemee kuendelea kama taifa. Maendeleo ya kweli ni uwezo wa watu kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kutumia watu wao wenyewe .

Above all else tunahitaji watu wenye skills na maarifa ya kutosha miongoni mwa watu wetu kuliko kitu kingine ili maendeleo yetu tujiletee wenyewe bila kusubiri watu wengine waje watuletee. So tunahitaji watu wenye nidhamu, skills , uzalendo na maarifa ya kutosha kama tunataka kuendelea na kuwa na dira kama taifa.
 
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu. Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana...

Ni kweli kabisa mkuu.

Kwa kuongezea tu, watu wasio na maendeleo ya akili hakuna wanachomiliki kwa ukamilifu hata kama kinaonekana cha kwao kwa sheria za kawaida.

Yaani hata miili yao na akili zao zaweza kutamalakiwa na watu wengine.

“Kwao ni kwetu kwanini, na kwetu kwao kwanini?”(S S Kandoro, Diwani ya Akilimali)

Wekeza kwanza kwenye maendeleo ya watu nao wataleta maendeleo ya vitu.
 
Watu hatuli stendi mpya za mabasi wala maflyover wala bombadier .....hivi ni vitu tu kama tunavyoona ktk tv au movie kuhusu Maendeleo ya Vitu ktk nchi za Marekani, Asia, Ulaya na Oceania.

Kule Afrika ya Kusini wale weusi waliviona vyote kuhusu Maendeleo ya Vitu lakini hawakuvihusudu bali walilia mabadiliko.

Mguso mkubwa kwa wote ni Maendeleo ya Watu.
 
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu.

Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana. Na ndio hasa yanayofanya watu wafanye kazi kwa bidii ili wabadilishe mazingira yao na kuitawala dunia. Maisha yamekuwa rahisi zaidi kuliko karne kadhaa zilizopita kwasababu ya maendeleo ya vitu yaliyoletwa na vumbuzi kadhaa...

Wewe ndio umeongea kitu kikaniingia akilini.
 
Hakuna maendeleo ya watu bila vitu. Dunia ilianza na vitu na hata Mungu alianza kuumba dunia na kisha mtu. Meli itasaidia watu kusafiri na kupunguza adha ya kusafiri kwa mateso hata kama wana pesa kama hamna vitu utazifanyia nini ingawaje ili uwe na vitu unahitaji watu na pesa kama mtaji tu kuzalisha ikiwemo ardhi.

Hospitali na madawa zikitumiwa na madaktari zitatibu watu na kuwapa afya na kisha kuzalisha kuitafuta hiyo pesa. Fedha tunazozitaka kwa wingi za kuzagaa hazipo tena kutokana na mianya ya rushwa madawa ya kulevya etc kuzibwa. We playing with formal source of income na controlled economy inayohitaji uchape kazi.

Inabidi tuseme ni vitu gani ambavyo hatuvitaki na havina multplier effect! Hii ni issue tu ya kanuni za uchumi haya mambo yanategemeana mwisho wa siku. Mjadala huu ni mpana.
 
Watu hawajaendelea kama hawawezi kujenga madaraja kwa kutumia watu wao wenyewe, kujenga reli kwa kutumia watu wenyewe, ndege kwa kutumia watu wao wenyewe, barabara, bunduki na vifaa vya kijeshi kwa kutumia watu wao wenyewe na mambo mengine mengi wanayotumia kwa maisha yao wenyewe ya kila siku. Tunapima uwezo wa nchi na maendeleo yake kwa uwezo wa raia wake kutengeneza vitu wanavyotumia kila siku na sio kutumia wasichozalisha.

Swadakta, ndiyo nchi tajiri zilivyotajirisha watu wake na kuchochea Maendeleo ya Watu.

Tofauti na CCM Mpya yenye ufinyu wa mawazo kwa kukopi na kupesti reli SGR, madaraja na flyover za China kununua bombadier Canada au Dreamliner USA ili tu zionekane angani bila tija, kujenga stendi mpya za mabasi ambazo ni kubwa kuliko hospitali za rufaa za kanda ....listi ni ndefu
 
Hakuna maendeleo ya watu bila vitu. Dunia ilianza na vitu na hata Mungu alianza kuumba dunia na kisha mtu. Meli itasaidia watu kusafiri na kupunguza adha ya kusafiri kwa mateso hata kama wana pesa kama hamna vitu utazifanyia nini ingawaje ili uwe na vitu unahitaji watu na pesa kama mtaji tu kuzalisha ikiwemo ardhi...

Nadhani dhana nzima ya maendeleo ya vitu vs watu inachanganywa. Watu ndio wanaoleta maendeleo ya vitu. Kwahiyo hakuna budi kuwekeza kwa watu kwa kuwapa elimu bora na kuangalia kwa ukaribu ukuaji wa kiakili wa watu. Ukiwa na madaraja kibao, ndege, magari na kila kitu alafu watu wako ni wajinga haisaidii kitu. Lakini ukiwekeza kwa watu ili walete vitu hivyo wao wenyewe kwa kuwekeza kwenye Elimu yao umewasaidia sana.

Leo hii hiyo Reli sio watz wanaoijenga, hatuna uwezo wa kutengeneza ndege, madaraja na barabara za kisasa. Tunawajibika kujenga uwezo huo kwa watu wetu. Na huku ndio kujitegemea. So tunahitaji kujenga watu wetu kuwa na skills za kutosha ili walete maendeleo kwenye nchi yao wenyewe badala ya kutegemea watu wengine watuletee maendeleo ya vitu.

Maendeleo ya vitu ni muhimu lakini lazima yaletwe na watu wenyewe. Bado tuna kiwango kikubwa sana cha ignorance kwenye nchi tunapaswa kupambana na hilo. Kuwafanya watu wetu kuwa na uelewa mkubwa na wenye kujitambua ili wajiletee maendeleo.

Ukiangalia hadi leo hii afrika imekuwa sehemu ambayo wachina na wazungu ya kutafutia malighafi na masoko sababu ya uwezo wetu mdogo wa kuzalisha wa ndani, Tumekuwa soko la mataifa mengine. So tunahitaji watu wenye skills za hali ya juu ili kuzalisha. Kutokana na hilo hatuwezi kufaidika sana. Nguvu ya nchi inatokana na uwezo wao wa ndani wa kuzalisha.
 
Ni hoja ambayo imegeuzwa na Wanasiasa kama mtaji wa kisiasa na huenda ikatumika kama agenda kuu katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu. Kuna dalili ya kuelekea huko kutokana na jinsi Wanasiasa wanavyotafsiri taarifa ya Benki ya Dunia kuitambua Tanzania kama moja ya nchi yenye Kipato cha Kati.

Labda WanaJF mtasaidia kujibu swali langu hili, Je, wapiga kura, wengi wao (70%) wanaishi vijijini, watapenda kusikia nini kutoka kwa Wagombea, ili waridhie kuwapa kura yao?
Awamu hii inaboa sana, propaganda zimezidi wananchi hatuoni maendeleo ya maana, hali imekuwa ngumu sana. Tutajaribu wapinzani tuone mambo yatakuwaje.
 
Swadakta, ndiyo nchi tajiri zilivyotajirisha watu wake na kuchochea Maendeleo ya Watu.

Tofauti na CCM Mpya yenye ufinyu wa mawazo kwa kukopi na kupesti reli SGR, madaraja na flyover za China kununua bombadier Canada au Dreamliner USA ili tu zionekane angani bila tija, kujenga stendi mpya za mabasi ambazo ni kubwa kuliko hospitali za rufaa za kanda ....listi ni ndefu

Na kujenga viwanja vikubwa vya michezo badala ya ghala za kuhifadhi chakula cha tahadhari.
 
Back
Top Bottom