Kimsingi jamaa yupo vizuri kwa mtazamo wake na vipaumbele vya ilani ya chama chake, Ila kutokana na malighafi nyingi tulizonazo inatakiwa tupate kiongozi atakae fumua mfumo w elimu iliyopo kwa sasa ambayo si rafiki Sana kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja.
Tukifanikiwa kutoa elimu itakayomfanya Kila mhitimu aweze kujitegemea na kuwa na uwezo wa kugundua fursa katika eneo lake itakuwa poa Sana, apo serikali kazi yake itakuwa ni kuwaendeleza na kuwatafutia masoko kwakile kinacho zalishwa.
Kwa kumalizia ni vyema nchi yetu ikafanya mabadiliko kwenye uongozi hiki chama kimoja hakitatufikisha kule tunakotarajia kwenda,inatakiwa siku moja wakae pembeni wajifunze kwa wenzao ili wakirudi Tena watajifunza kufuata ushauri wa wananchi Kama mtoa mada hapo juu!!
Hakuna asiyetaka mabadiliko ya uongozi kama yanaambatana na mabadiliko chanya. Ni msingi huo huo Rais amekuwa akiwatumbua viongozi wasiotimiza matarajio ya nafasi zao.
Hivyo basi kutahitajika chama chenye Sera mbadala na bora zaidi kwa maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia. Hicho chama pia kinapaswa kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa (wenye kuziishi sera za chama).
Hapa nchini kuna mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, bado wanasiasa na wananchi wanaishi, kwa maneno na matendo kama vile nchi iko kwenye mfumo wa chama kimoja.
Hilo linajitokeza dhahiri wakati wa chaguzi. Vyama vya siasa vingi huteua wagombea wenye sifa binafsi. Vichache, ambavyo hutumia mchakato wa kura za maoni pia huteua wagombea wanaokidhi sifa zilizowekwa na chama lakini si uwezo wao wa kuelewa na kuieleza Ilani ya Uchaguzi ya chama kwa wapiga kura.
Wagombea karibu wote, kwenye kampeni, badala ya kunadi sera zao wanashambuliana na kuonesha ubingwa wao jukwaani, wakijirundikia sifa wasizostahili na wakati mwingine kutoa ahadi hewa. Wananchi nao badala ya kusikiliza sera huvutiwa na malumbano na misifa ya wagombea jukwaani.
Pamoja na mapungufu hayo, kwa vyama vya siasa vinavyoshiriki chaguzi Mkuu, mwaka huu, ni CCM bado inazo sifa za kuongoza nchii, kimuundo, Kisera na aina ya viongozi wake.