Maendeleo ya watu au vitu?

Maendeleo ya watu au vitu?

Hakuna asiyetaka mabadiliko ya uongozi kama yanaambatana na mabadiliko chanya. Ni msingi huo huo Rais amekuwa akiwatumbua viongozi wasiotimiza matarajio ya nafasi zao.

Hivyo basi kutahitajika chama chenye Sera mbadala na bora zaidi kwa maendeleo ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia. Hicho chama pia kinapaswa kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa (wenye kuziishi sera za chama).

Hapa nchini kuna mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa, bado wanasiasa na wananchi wanaishi, kwa maneno na matendo kama vile nchi iko kwenye mfumo wa chama kimoja.

Hilo linajitokeza dhahiri wakati wa chaguzi. Vyama vya siasa vingi huteua wagombea wenye sifa binafsi. Vichache, ambavyo hutumia mchakato wa kura za maoni pia huteua wagombea wanaokidhi sifa zilizowekwa na chama lakini si uwezo wao wa kuelewa na kuieleza Ilani ya Uchaguzi ya chama kwa wapiga kura.

Wagombea karibu wote, kwenye kampeni, badala ya kunadi sera zao wanashambuliana na kuonesha ubingwa wao jukwaani, wakijirundikia sifa wasizostahili na wakati mwingine kutoa ahadi hewa. Wananchi nao badala ya kusikiliza sera huvutiwa na malumbano na misifa ya wagombea jukwaani.

Pamoja na mapungufu hayo, kwa vyama vya siasa vinavyoshiriki chaguzi Mkuu, mwaka huu, ni CCM bado inazo sifa za kuongoza nchii, kimuundo, Kisera na aina ya viongozi wake.
CCM hii hii ambayo kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika imeshindwa kuondoa maadui wakuu watatu wa Watanzania zaidi ya kuwaongeza maadui wengine ndio inayoweza kuwa imara kuwaletea maendeleo Watanzania kweli!?
Msikilize huyu bibi hapa chini.
 
Kumekuwepo na mjadala mpana sana kuhusu mantiki mbili za maendeleo kwenye mitandao ya kijamii, nami ningependa kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili, Kuhusu maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu. Jambo la kwanza ambalo tunapaswa kutambua ya kwamba maendeleo ya vitu ni kwaajili ya watu. Watu ndio wanaotumia vitu na ndio walio vitengeneza kwaajili yao. Kwahiyo maendeleo ya vitu ni muhimu sana. Na ndio hasa yanayofanya watu wafanye kazi kwa bidii ili wabadilishe mazingira yao na kuitawala dunia. Maisha yamekuwa rahisi zaidi kuliko karne kadhaa zilizopita kwasababu ya maendeleo ya vitu yaliyoletwa na vumbuzi kadhaa.

Kwahiyo hatuwezi kuyakataa moja kwa moja. Jambo la msingi la kujadili hapa pengine ni jinsi gani tutawekeza kwa watu ili hayo maendeleo wajiletee wao wenyewe badala ya kutegemea watu wengine. Hapa tunazungumzia intellectual + moral development kwa watu wetu. Kama nchi kwa kiwango kikubwa bado ni tegemezi.

Bidhaa nyingi ambazo tunazo katika nchi yetu hatujazalisha sisi wenyewe na hatuna technologia ya kufanya hivyo. Bado ni tegemezi kwa kiwango cha juu kwenye masuala ya technologia kwahiyo tunahitaji kuwekeza kwa watu ili wawe na skills za kutosha ili walete hayo maendeleo ya vitu kutokana na intellectual capability zao. Nadhani huu ndio msingi wa kujitegemea kama nchi na ndio msingi wa kuwekeza kwa watu na maendeleo ya watu. Na Elimu yetu inapaswa kujengwa katika mtizamo huo.

Watu hawajaendelea kama hawawezi kujenga madaraja kwa kutumia watu wao wenyewe, kujenga reli kwa kutumia watu wenyewe, ndege kwa kutumia watu wao wenyewe, barabara, bunduki na vifaa vya kijeshi kwa kutumia watu wao wenyewe na mambo mengine mengi wanayotumia kwa maisha yao wenyewe ya kila siku. Tunapima uwezo wa nchi na maendeleo yake kwa uwezo wa raia wake kutengeneza vitu wanavyotumia kila siku na sio kutumia wasichozalisha.

Kuna kauli inazungumzwa na watu nchi yetu ni tajiri ina mali ghafi wanasahau kwamba ili malighafi iwe mali ugunduzi wa vitu unatakiwa ufanyike. Petroli bila ugunduzi wa magari isingekuwa na thamani. Gunduzi ndio zinazofanya malighafi kuwa mali. kwa mantiki hiyo tusidhani kwamba malighafi zetu zitatufaidisha zaidi ya wale waliofanya malighafi kuwa mali, waliofanya malighafi kuwa mali ndio wenye nguvu zaidi. Katika uhalisia wake malighafi haiwezi kuwa mali pasipo gunduzi. Tusipokuwa na aina hii ya fikra tusitegemee kuendelea kama taifa. Maendeleo ya kweli ni uwezo wa watu kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kutumia watu wao wenyewe .

Above all else tunahitaji watu wenye skills na maarifa ya kutosha miongoni mwa watu wetu kuliko kitu kingine ili maendeleo yetu tujiletee wenyewe bila kusubiri watu wengine waje watuletee. So tunahitaji watu wenye nidhamu, skills , uzalendo na maarifa ya kutosha kama tunataka kuendelea na kuwa na dira kama taifa.
Akhsante
 
Back
Top Bottom