Manji sema usiposema...

Manji sema usiposema...

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,168
Reaction score
48,446
Mwanasiasa mwanachama wa CCM na Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Yusuph Manji inawezekana ndiye Diwani pekee wa CCM ambaye anakumbana na misukosuko mingi sana katika siku za karibuni. Lakini watu kadhaa wanadai kwamba Manji anajua nini kinaendelea dhidi yake.

Kama nadharia kwamba Manji anajua kinachoendelea dhidi yake ni ya kweli, basi ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kusema ukweli ni nini hasa kinachoendelea ili ajinasue kutoka wenye mtego uliomnasa.

Yanga, Coco Beach, Quality Group of Companies,siasa ama ni nini hasa!?
 
Mwanasiasa mwanachama wa CCM na Diwani wa Kata ya Mbagala Yusuph Manji inawezekana ni Diwani pekee wa CCM ambaye anakumbana na misukosuko mingi sana katika siku za karibuni. Lakini watu kadhaa wanadai kwamba Manji anajua nini kinaendelea dhidi yake.

Kama nadharia kwamba Manji anajua kinachoendelea dhidi yake ni ya kweli, basi ni yeye mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kusema ukweli ni nini hasa kinachoendelea ili ajinasue kwenye mtego uliomnasa.

Yanga, Coco Beach, Quality Group of Companies,siasa ama ni nini hasa!
LOWASA
 
Inasemekana aliwahi kumjibu Dereva wa sasa kwamba hawezi kuongea na mbwa anaongea na mwenye mbwa. Sasa hatujui ndio analipia kauli zake sasa ama.laa
kama ni hivyo basi hamna kesi yoyote hapo.
mahakama itamhukumu Manji on legal merit tu, labda kama kweli alihujumu!
 
Inasemekana amekutwa na muhuri wa jeshi isivyo halali. Na pia vitambaa vya sare za jeshi. Mashtaka aliyofunguliwa ni uhujumu uchumi pamoja na kuhatarisha usalama wa taifa.

Nadhani ana mengi ya kusema kama atabahatika kuendelea kuwepo.

Je alikuwa na utaratibu wa kufanya hivyo kila mara?

Vitambaa hivyo vilikuwa vikipelekwa wapi? Kazi haswa ya huo muhuri ni nini?

Maana sasa kuna shtaka la uhujumu uchumi na usalama wa taifa. Sasa kwenye usalama wa taifa sijui tatizo liko wapi, kwani hizo sare zilitakiwa kupelekwa kwa wanajeshi waasi ama kikundi chochote cha uasi? (Mh rais ameshawahi kulihuisha na mauwaji ya kibiti pamoja na mashehe walioko lockup)

Wafanye wafanyacho ila cha muhimu haki itendeke, msumeno wa sheria ukate kotekote.

Yani hata kama kuna walioshirikiana naye na wako kwenye vyombo vya madaraka wabanwe. Unless rais aliyepo ana mpango wa kukaa madarakani maisha yake yote.

Kwasababu huwezi kumkuta na makosa na kumuhukumu kama ameshirikiana na vigogo halafu ukawafumbia macho vigogo hao na hukumu ikawa ya haki.

Kwa upande mwingine pia, asiwe amebambikiwa. Lakini kama vinahusiana na ugaidi ama jitihada za uasi, basi hilo ni suala jingine kabisa.
 
Back
Top Bottom