CCM wamechanganyikiwa, hawajui nini cha kufanya

CCM wamechanganyikiwa, hawajui nini cha kufanya

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
606
Hapo awali, tulikuwa taifa la watu waliokuwa wanaenda makazini na kurudi majumbani bila ulinzi, tukiishi kwa amani tele. Hakuna aliyekuwa anamdhuru mwenzake; uungwana na utu vilikuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Leo hii mambo yamebadilika — watu wanalindwa baa, mitaani, na hata barabarani kana kwamba tuko vitani.

Hii siyo Tanzania tuliyoizoea. Watanzania si watu wa vurugu, si watu wa chuki; haya ni mambo mapya ambayo CCM wameyataka, na bado wanaendelea kuyataka.

Nchi ipo njia panda, hakuna kinachoendelea zaidi ya kukamatana, kuwindana, visasi na vilio. Ni hali ya huzuni na kuchanganyikiwa, hasa kwa wale waliokuwa na imani kwamba amani yetu ni ya kudumu.

Kwa sasa, ni wazi kabisa CCM wamechanganyikiwa, hawajui nini cha kufanya.
1762695336916.png
 
Zile mali ulizoiba siku ya vurugu zifukie chini muda siyo mrefu unafikiwa, ndo itakua kielelezo chako cha kuunganishwa kwenye uhaini
 
Kosa la kwanza la ccm ilikuwa kutuchagulia viongzi wanaotaka wao kwa hisani yao kwakuzima sauti ya watu kwa mtutu wa bunduki.kosa la pili mauaji na utekaji kosa la 3 kuhodhi mihimili wa mahakama na kudharau katiba na sheria nakuita ni makaratasi kosa la 4 ni ufisadi japo wananchi wamevumilia vyakutosha dharau imezidi na mateso kwa wananch wananunua magari ya kifahari kwa viongozi huku wananchi wanachmbiwa maji kwa hisani ya waturuki mwananch anayepgia kura ccm hata nyama kula ni mpaka sadaka ya wahisani wa waturiki,choo ni mpaka usaid kuna mambo ya ovyo sana.ukisema jambo la ukweli unatekwa.
 
Zile mali ulizoiba siku ya vurugu zifukie chini muda siyo mrefu unafikiwa, ndo itakua kielelezo chako cha kuunganishwa kwenye uhaini
Jamaa una busara sana umeibiwa basha na umesamehe
 
Back
Top Bottom