Manji atakiwa kuripoti Ofisi za Mamlaka ya Uhamiaji. Pasi 126 za kusafiria zakamatwa ofisini kwake

Maskini wanaamini wanaweza kuwa Matajiri kwa Tajiri kuwa kama wao.....
Sijui kosa lake hasa ni lipi? Manji ndio mkosaji au Serikali ndio wakosaji? Kama walikoseana mahali kwanini wasimalizane tu? ili kuokoa kampuni za Quality group zilizoajiri mamia ya watanzania wanaotegemea kulipa kodi za kuendesha nchi ...

Hatuna wazee wenye busara nchi hii? wasuluhishe hili janga,sioni raha kuona mtu anaumia ...
 
Hapo anayetakiwa kujibu mashtaka ni Quality group of companies sio ishu ya mtu binafsi hiyo.... japo sijui makosa yake ila kwa hili sheria itambeba Manji.
 


"watawala" sio watu wa kula nao deal popote ulimwenguni sababu "watawala" hawaaminiki
 
Tajiri ambaye halipi kodi wala hatoi ajira kwa hili taifa hatumtaki, Manji anajulikana kwa scandals za kifisadi na rushwa kila mtu anajua, alikuwa a nataka kuhonga kule Dodoma ili rais atakayeingia amuendeshe kama farasi wake na achume anavyotaka lakini aliangukia pua.

Kama wale takukuru na police aliwahonga sio wa leo tena lazima sheria ifuate mkondo wake.
 
we vipi?Kuna mtu alienda kupekuliwa kesi ya wizi wa kuaminika akaukutwa na bunduki mbili zisizo na kibali.Tatizo huzaa tatizo mkuu
 
Hapo wakipewa tena vielelezo watahamia wapi! Nimesikia pia gwajima walihamisha kesi toka poda hadi utakatishaji hapo wakakosa,nadhani sasa wanamtafutia lingine
 
Ile ya madawa ya kulevya imeishia wapi? Je yale mashitaka ya kumtaja kuhusika na madawa ya kulevya yamethibitishwa? na lini anafikishwa mahakamani? Hatutaki kumtetea mtu yeyote kwa makosa aliyofanya, lakn hatutaki pia kuona mtu yeyote akionewa na kudhalilishwa bila ushahidi kwa sababu tu ana pesa zake.
 

EWGM'sJF-Expert Member
[HASHTAG]#261[/HASHTAG]
5 minutes ago

New

Kabla hujaanza kuuliza hayo masuala jiulize Kwanza unaemuuliza ni nani immigration na wewe ni nani immigration

ana elimu gani kwenye immigration na wewe una elimu gani kwenye immigration,

ana cheo gani immigration na wewe una cheo gani immigration,

kazi kaanza lini immigration na wewe kazi ulianza lini immigration.

Ukishapata majibu ya hayo maswali ndio uulize sasa maswali yako.
 
Hivi huyo wanamnyanysa kwa siasa zipi hasa.......si MUCCM mwenzao huyo?.......au ndio msemo wa GWAJIMA..........NI WIVU TU.
Wache ccm wanajuwana hao muda wote uhamiaji wapo wapi wasijuwe kuwa kunawafanyakazi wanafanya kazi bila vibali na wao watumbuliwe hakuna namna
 
Hapo anayetakiwa kujibu mashtaka ni Quality group of companies sio ishu ya mtu binafsi hiyo.... japo sijui makosa yake ila kwa hili sheria itambeba Manji.
Sasa afisa uhamiaji anakwambia hapa tunataka kumkamata Manji bahati mbaya wameambiwa amelazwa hospitali.
 


Dah...kwa hakika kazi ipo...Ndugu yetu Yusuph Manji anaangushwa na mambo kadhaa lakini kubwa ni lile la kutotumia vizuri umaarufu wake...Kwa bahati mbaya nadhani hana washauri wazuri....Wako matajiri/wafanyabiashara wengi lakini hawajafuatiliwa kwa kuwa wako kimya na hawako vocal kwa mambo mengi yakiwemo ya kisiasa na kijamii...Kwa maoni yangu tabia yake ya kujaribu kupambana na vyombo mbalimbali vikiwemo vya dola inamjengea maadui wengi pasipo sababu kabisa...Wako TFF ambao nao hawako vizuri naye kwa sababu mbalimbali za soka...mara watu waingie bure mpirani, mara sijui kukataa fedha za wafadhali /Azam, hiyo yote inatengeneza maadui...Ndani ya Yanga nako kuna maadui ingawa ni wachache...kuitisha mkutano wa wanachama katika mazingira tatanishi na wanachama hao kuwatimua na kuwafuta uanachama viongozi wenzake wa klabu pasipo sababu za maana nako ni kujitengenezea maadui pasipo sababu kabisa...Aidha wazo lake la kutaka kukodisha Yanga ni zuri lakini namna au mazingira ya kukubaliwa wazo hilo ni tata kabisa, hali iliyowafanya baadhi ya wanachama kupinga na hata kwenda mahakamani, huko nako ni kujitengenezea maadui...

Hili la juzi la tuhuma za dawa za kulevya linasikitisha...ni kweli mazingira ya kuitwa kwake hadharani ni tata, lakini huwezi kupambana na dola kwa kuitisha press conference na kutoa maneno yale aliyotoa...washauri walipaswa wamshauri kuwa akae kimya na apambane kimya kimya kwa kutumia njia za kisheria...wanachama wa Yanga nao baadhi yao hawamsaidii kabisa Mhe. Yusuph Manji...wanapiga kelele na kufanya vitu visivyostahili...Kumsindikiza huko polisi ni jambo la kawaida, lakini kuamua kuosha gari lake huko polisi ni utovu wa nidhamu, na inaweza kutafsiriwa kuwa ni kudharau na kuingilia majukumu ya chombo hicho cha dola kwa kutaka kushinikiza maamuzi yake. Wako ambao pengine hawatanilelewa kwa andiko hili, lakini kwa maoni yangu Ndugu yetu Manji anahitaji msaada wa ushauri wa namna ya kuendesha mambo ndani ya jamii kwa kutumia umaarufu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…