Manji akibembelezwa 'tutapigwa' tena

Manji akibembelezwa 'tutapigwa' tena

Asante mkuu kwa kukubali kwamba alishirikiana na.... Sasa tufanye nini kama nchi aisee, aitwe mzalendooo...! Au ni mwizi na anapaswa afanye biashara zake Kwa kufuata Sheria??
Muhimu ni kurekebisha mifumo ya uadilifu na udhibiti.

Imagine, mtu anakwambia Manji alihonga madiwani apewe maeneo.

Madiwani wetu wenyewe tunawachagua kwa kupewa rushwa za pombe.

Sasa hapo utaona tatizo ni jamii nzima wala siyo Manji peke yake.

Sasa kama madiwani wanapokea rushwa kutoka kwa Manji wanawezaje kukataa rushwa kutoka kwa mtu mwingine ?
 
Mkuu, hawa ndiyo wale mtaani mtu akinunua Ford Ranger wanakununia - hawajui kwamba kuishi na jirani tajiri ni fursa!!

Karibu Mr. Manji nyumbani hii ni nchi yako !! njoo tukae tuone tutafanya nini pamoja nawe, ukitusaidia ajira walau vijana 5000 hivi ni zaidi ya asante kwa nchi yako - ajira hakuna mzee wangu, vijana wanasaga lami mwanzo mwisho.
Maskini siyo mtu wa kukupatia
 
Manji alikula hata na CCM, alikuwa mfadhili mkuu, kwa wanaokumbuka alinunua jengo la NSSF na kulikarabati kisha kuliuza tena kwa bilions kwa hao waliomuuzia.
Ukweli Ni kwamba katika dili zake zote alishirikiana na wakubwa na sheria zikimlinda.
 
NSSF ndio kabisaaaa. Hakuna msafi.

  • Mbowe alikopa
  • CCM walikopa
  • Serikali imekopa
  • Zitto ( Enzi za Dau )
  • Manji
  • Wanasiasa wa CCM ?????

In short, NSSF ilikuwa ni pora chako mapema. Ndio maana sasa hivi inalipa wastaafu kwa kusuasua mno.
 
Acha chuki na wawekezaji mkuu, jifunze kutoka kwa walifanikiwa.
Kweli kabisa Kuna baadhi ya watu hudhani kila aliye fanikiwa ni mwizi Freemason Katoa ndagu jamaa zake huo ni upofu huwezi kufanikia bila kujifunza kutoka ktk waloofanikiwa hiyo ndiyo formula ya dunia kinyume chake hutofanikiwa na utakapo yatafuta mafanikio utajihusisha na njia hizo haramu na kamwe hutafanikiwa
 
Niseme Kwa ufupi sijui in details hasa
Yanayosemwa yalikuwa 'maovu ' ya manji
Na sijui in details ni kiasi gani 'alionewa'..

Lakini kuna vitu najua kabisa Manji alishiriki 'kupiga ' nchi na alishirikiana na
'viongozi' wetu maeneo mbalimbali..

Pori la Nafco pale kigambon ni eneo moja ambalo alilipiga akiwa amejiandaa 'kuiuzia tena ' serikali'..

Kampuni yake moja ilipewa tenda mbalimbali za upimaji wa ardhi na kuwaweka 'mfukoni' madiwani karibu wote hadi kufanya kampeni ya kumchagua Didas Masaburi enzi hizo ili mambo yake yaende....

Inawezekana kuna maeneo 'alionewa'lakini kama kuna watu wanataka abembelezwe na 'kurudishiwa 'kila kitu basi watakuwa tayari 'kuruhusu '
Tupigwe tena with revenge ..na watu aina ya Manji ..
Si ajabu akadai hadi fidia..
MaMA amuogope huyo jamaa. Atamchafulia CV. Hana mana kabisa
 
Ujio wa Manji naona kama umepokelewa kwa vifijo sielewi ni mashabiki wa Yanga ndio wanaofurahia au watanzania kwa ujumla wetu.

Kama Manji alikimbia nchi kwa kumuogopa JPM aulizwe kwa nini alimuogopa, kwasababu wapo kina Mo walikomaa na JPM licha ya kutekwa na wasiojulikana.

Napenda kujua exactly vinavyoitwa vilikuwa vitega uchumi vya Manji kama ni vyake kweli au aliwashikia wengine, lile jengo pale Quality Plaza tuliambiwa serikali imelichukua Manji alipangisha ila naye akapangishia wengine.

Kama alikuwa navyo kwanini akavikimbia kirahisi hivyo, hata kama inasemekana alihamishia nchi nyingine, bado napata mashaka sana na unaoitwa utajiri wa Manji, au kuitwa mfanyabiashara mkubwa.

Kwangu Manji alikuwa ni mjasiriamali anaechipukia ambaye alikuwa anaangalia fursa ya kupiga kwa kushirikiana na utawala uliokuwepo madarakani kabla ya Magufuli, lakini simuoni Manji kama mfanyabiashara anaeweza kusimama peke yake bila kufanya ujanja ujanja kwa kushirikiana na viongozi wa serikali, Samia awe makini nae sana.

Ndio maana wakati ule pakawepo na tuhuma nyingi za ukwepaji kodi zikimuhusisha Manji, huyu mtu ni msanii anaechota akili za wasiojielewa ndio maana kwa kutambua hilo akaenda Yanga.

Apate kuungwa mkono na mashabiki wa Yanga, ili akiharibu akiguswa na serikali jamaa wamtetee bosi wao, na hata Yanga kwenyewe hakuwa muwekezaji kama Mo alivyo Simba, Manji alikuwa ni mfadhili tu kwa kuogopa kupoteza pesa zake bure.
 
Unajua manji alikua ameajiri watu wangapi kabla ya kufurushwa??
Acha chuki za kifala kama ulikua ushajimilikisha baadhi ya assets zake jiandae kuzitapika.

All in all manji ni mtanzania
 
Hivi dogo bado unafanya kazi ya ulinzi?
Manji hakuondoka nchini au kuadhibiwa kwa "Upigaji"

Manji alishughulikiwa kwa beef personally kabisa na Magufuli.

In short Manji hakuwahi kuwa kiongozi wa serikali nchi hii, alipiga kwa kushirikiana viongozi wa serikali ambao wengine kila serikali inayoundwa wapo.

Magu angekuwa anamshughulikia Manji kwasababu za upigaji, asingemkaribisha Rostam Ikulu na angewadhibiti walioshiriki kula na Manji pia.

Sasa huwezi kudeal na Manji personally wakati wapigaji wengine kama yeye unafumba macho. Huo ni uonevu.

In short, kwa walalahoi ujio wa Manji ni faida kuliko hasara, kwasababu:
  • Ajira
  • Kodi
  • Ununuzi wa mazao hasa Mbaazi na ufuta

Kuhusu UPIGAJI hata asipopiga yeye, UPIGAJI upo, watu WATAPIGA hata kama siyo Manji na wala hatutapata faida yoyote.

Suala la UPIGAJI lipo tu, whether Manji yupo au Hayupo.
 
Subiri mabavicha yatakuita mataga sasa hivi!

Yenyewe yanasubiri hela zirudi mtaani ili yawe yanaokota na wanaozirudisha yanaamini ni hao kina Manji
 
Unajua manji alikua ameajiri watu wangapi kabla ya kufurushwa??
Acha chuki za kifala kama ulikua ushajimilikisha baadhi ya assets zake jiandae kuzitapika.

All in all manji ni mtanzania
Twambie vitega uchumi vya Manji ambavyo alikuwa ameajiri watu
 
NSSF ndio kabisaaaa. Hakuna msafi.

  • Mbowe alikopa
  • CCM walikopa
  • Serikali imekopa
  • Zitto ( Enzi za Dau )
  • Manji
  • Wanasiasa wa CCM ?????

In short, NSSF ilikuwa ni pora chako mapema. Ndio maana sasa hivi inalipa wastaafu kwa kusuasua mno.
Du! Ndio maana huwezi kumsikia Zitto wala Mbowe wakiwatetea wastafu!!
 
Twambie vitega uchumi vya Manji ambavyo alikuwa ameajiri watu

Unajua ujanja aliotumia kujenga QUALITY plaza; zile ni hela za wafanyakazi alizokomba NSSF na mafisadi wakina Ramadhani Dau!!!
 
Niseme Kwa ufupi sijui in details hasa
Yanayosemwa yalikuwa 'maovu ' ya manji
Na sijui in details ni kiasi gani 'alionewa'..

Lakini kuna vitu najua kabisa Manji alishiriki 'kupiga ' nchi na alishirikiana na
'viongozi' wetu maeneo mbalimbali..

Pori la Nafco pale kigambon ni eneo moja ambalo alilipiga akiwa amejiandaa 'kuiuzia tena ' serikali'..

Kampuni yake moja ilipewa tenda mbalimbali za upimaji wa ardhi na kuwaweka 'mfukoni' madiwani karibu wote hadi kufanya kampeni ya kumchagua Didas Masaburi enzi hizo ili mambo yake yaende....

Inawezekana kuna maeneo 'alionewa'lakini kama kuna watu wanataka abembelezwe na 'kurudishiwa 'kila kitu basi watakuwa tayari 'kuruhusu '
Tupigwe tena with revenge ..na watu aina ya Manji ..
Si ajabu akadai hadi fidia..
Connection ya Manji kurudi imetengenezwa na Albert Marwa, am sure they are up to something evil
 
Back
Top Bottom