Manji akibembelezwa 'tutapigwa' tena

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,873
Niseme Kwa ufupi sijui in details hasa yanayosemwa yalikuwa 'maovu ' ya Manji na sijui in details ni kiasi gani 'alionewa'..

Lakini kuna vitu najua kabisa Manji alishiriki 'kupiga ' nchi na alishirikiana na 'viongozi' wetu maeneo mbalimbali.

Pori la Nafco pale Kigambon ni eneo moja ambalo alilipiga akiwa amejiandaa 'kuiuzia tena ' serikali'. Kampuni yake moja ilipewa tenda mbalimbali za upimaji wa ardhi na kuwaweka 'mfukoni' madiwani karibu wote hadi kufanya kampeni ya kumchagua Didas Masaburi enzi hizo ili mambo yake yaende.

Inawezekana kuna maeneo 'alionewa'lakini kama kuna watu wanataka abembelezwe na 'kurudishiwa 'kila kitu basi watakuwa tayari 'kuruhusu '.

Tupigwe tena with revenge ..na watu aina ya Manji.

Si ajabu akadai hadi fidia..
 
Who cares after all-Hata wewe kama umeona loop hole mahali kwenye sheria za nchi wekeza tu utupige no problem.Ni wajibu wa serikali kuziba loop holes katika sheria na siyo mwekezaji.

Sisi waafrica tupo maskini na tutaendelea kuwa maskin as long as tutaendelea kuamini kila tajiri,mwekezaji au mwenye mafanikio ni jambazi.
 
Mkuu, Kwa nchi yangu hii, mwenye kuelewa ulichosema ni wachache mno, ni wale tu wanaotamani siku waione nchi hii ikiwa kwenye viwango Bora vya maendeleo kama zilivyo nchi nyingine huko.

Lakini Kwa wenginewengi, hawatataka kufahamu ni kivipi atatupiga na kivipi upigaji huo unaathiri vipi huduma za kijamii na Kwa vizazi vijavyo, watafurahia tu kupata vibarua ili mkono uingie kinywani. Na ndiyo wengi hao,

Ninamashaka na Elimu yetu hasa ya uraia kama imetusaidia kama taifa
 
Acha chuki na wawekezaji mkuu, jifunze kutoka kwa walifanikiwa.
Mkuu, hawa ndiyo wale mtaani mtu akinunua Ford Ranger wanakununia - hawajui kwamba kuishi na jirani tajiri ni fursa!!

Karibu Mr. Manji nyumbani hii ni nchi yako !! njoo tukae tuone tutafanya nini pamoja nawe, ukitusaidia ajira walau vijana 5000 hivi ni zaidi ya asante kwa nchi yako - ajira hakuna mzee wangu, vijana wanasaga lami mwanzo mwisho.
 
Manji hakuondoka nchini au kuadhibiwa kwa "Upigaji"

Manji alishughulikiwa kwa beef personally kabisa na Magufuli.

In short Manji hakuwahi kuwa kiongozi wa serikali nchi hii, alipiga kwa kushirikiana viongozi wa serikali ambao wengine kila serikali inayoundwa wapo.

Magu angekuwa anamshughulikia Manji kwasababu za upigaji, asingemkaribisha Rostam Ikulu na angewadhibiti walioshiriki kula na Manji pia.

Sasa huwezi kudeal na Manji personally wakati wapigaji wengine kama yeye unafumba macho. Huo ni uonevu.

In short, kwa walalahoi ujio wa Manji ni faida kuliko hasara, kwasababu:
  • Ajira
  • Kodi
  • Ununuzi wa mazao hasa Mbaazi na ufuta

Kuhusu UPIGAJI hata asipopiga yeye, UPIGAJI upo, watu WATAPIGA hata kama siyo Manji na wala hatutapata faida yoyote.

Suala la UPIGAJI lipo tu, whether Manji yupo au Hayupo.
 

Manji hakuondoka nchini au kuadhibiwa kwa "Upigaji"

Manji alishughulikiwa kwa beef personally kabisa na Magufuli....
Asante mkuu kwa kukubali kwamba alishirikiana na.... Sasa tufanye nini kama nchi aisee, aitwe mzalendooo...! Au ni mwizi na anapaswa afanye biashara zake Kwa kufuata Sheria??
 
Issue sio Manji, Panjebee, Mohamed, Sharifu, Masanja wala Bakari...

Issue ni Haki na Sheria, kila binadamu awe judged kutokana na sheria na alichotenda sio allegations wala alichofanya juzi wala jana..

Kama alikuwa mpigaji na ameshikwa akipiga basi apelekwe kolokoroni ili alichopiga kirudishwe kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa hisia...

Tukiendesha dunia kwa misingi ya Haki na Sheria mengine yatajiseti automatically...
 
Back
Top Bottom