Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU HUDUMA YA VYOO KATIKA STENDI YA MAWASILIANO (SIMU 2000)
Ni kweli kwamba vyoo viwili vilivyokuwa karibu na eneo la awali la stendi vimesitishwa kwa muda kutokana na changamoto ya kujaa maji mara kwa mara, hali inayosababishwa na uoevu mkubwa wa ardhi katika eneo hilo. Hali hii imekuwa ikisababisha vyoo hivyo kujaa maji mapema na kushindwa kutoa huduma ipasavyo.
Hata hivyo, tunapenda kuufahamisha umma kuwa bado kuna choo kimoja kinachotoa huduma, ambacho kina jumla ya matundu 10; matano (5) kwa wanaume na matano (5) kwa wanawake, kuna misala (urinals) 10 kwa wanaume. Pia yapo mabafu mawili (2): bafu moja kwa wanawake na bafu moja kwa wanaume na huduma zinaendelea kama kawaida.
Kutokana na mabadiliko ya eneo la stendi baada ya sehemu ya awali kuchukuliwa na mradi wa DART, stendi imesogezwa mbele, hivyo kufanya baadhi ya wananchi kuona kuwa choo kilichopo ni mbali, hasa baada ya vile vilivyokuwa karibu kufungwa kwa muda.
Kwa sasa, uongozi unaendelea kuchukua hatua za haraka za ukarabati kwa kushirikiana na DAWASA ili kuunganisha mfumo wa maji taka (Public sewerage system) kwenye vyoo vilivyofungwa, ili kurejesha huduma kwa haraka na kwa uhakika zaidi.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea na unawahakikishia wananchi kuwa suala hili linashughulikiwa kwa dharura ili kuhakikisha huduma bora na salama zinaendelea kupatikana.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
==============
UPDATES...
Timu ya tathmini ilienda eneo la tukio ikiwa na gari ya kuvuta maji kutokana na ardhi kuwa oevu, ilishafanyika kilichobaki ni kitengeneza mfumo wa maji safi ndani ya vyoo ili vianze kutumika na kwamba DAWASA itafika hapo Februari 11, 2026 ili kurekebisha mfumo wa maji safi.
Pia soma:
~ Kusitishwa muda mrefu kwa huduma ya vyoo vya Stendi ya Mawasiliano kunasababisha kero kwa wananchi
~ Kero: Vyoo vya Simu 2000 ni vichafu sana
~ Madereva wa mkataba Ubungo halmashauri tunacheleweshwa mishahara