Manispaa ya Kinondoni yapata 'Division one' tano tu!

Manispaa ya Kinondoni yapata 'Division one' tano tu!

CHADEMA wangejaribu ku-break
down kwa kila jimbo ili wabunge wa CCM waone madhara ya ndiyo zao
bungeni. Kawambwa bado yuko ofisini anacheka. Kama Chami, Mkulo na Omar
Nundu waliondolewa kwa sababu za kiutendaji, kwa nini Kawambwa abaki
wakati generation inageuzwa mbumbumbu? 94% wamefeli, bado wana matumaini
na Waziri kuwa ana jipya?

Kawambwa ni ndugu wa damu wa Kikwete.
 
Mkuu wa mkoa, dc na mkurugenzi wa manispaa wanachekacheka tu. Hakuna usimamizi kwenye kila eneo ni kudai mshahara na posho tu. Wapo kama hawapo nao wanadai waziri ajiuzulu. Mungu wangu!
 
SHULE ZA KATA BANA, MTOTO ANAPIGA PEDO YA BYC ZAIDI YA SA2,AFU MOTIVATION KWA WALM HAKUNA, BWEN, MAABARA HAKUNA, WALM KUJAMIIANA NA DENT, MKUKU NI ZUZU KTK UONGOZ, WALM NA DENT WANAGONGANA BAR,GUEST,DISCO NAN ATAMKANYA, HAKUNA MCHUJO,MTAALA FEKI. Haa
 
Tena walio faulu ni 23,000..... assume wote watafaule pia form 6, mahitaji ya vyuo vyoooote mwaka 2015 inakdiliwa wahahitajika zaidi ya 97,000.... wengine watatoka wapi?

Hv mwaka huu A level ztajazwa na kina nan maana wakipeleka huu uozo cmiaka miwil ijayo hz zero ztahamia A level
 
Hivi kwa nini inaonekana kama vile ni jambo la kuidhihaki serikali eti kwa sababu walimu wamefelisha wanafunzi kwa sababu madai yao hayakusikilizwa,hii kazi ya ualimu haina ethics?

Bwana mkubwa wewe unalala mahali pazuri, umeshiba, maji yapo, umeme upo, daladala zipo! mwalimu aliyeko mahali fulani mazingira yake ni ya kutisha na wewe kama bosi wake hata kumfikiria humfikirii halafu unatweta ethics ethics! WaTZ wana akili baba wajali nao watajali. Wakati wa nyuma walikuwa wanaangaliwa na wanapewa wito wa kazi ktk mazingira magumu na wanaikubali hali.
Matokeo mabovu hata wa kuwajibika hakuna hizo ethics ni kwa upande mmoja tu? Heri ya Mkuu wa Mitaala aliliona hilo mapema.
 
Wivu tu mbona wabunge wengibwa cdm majimbo yao hayana division 1!!
 
Nasoma bachelor ya human resource management,nataka kukuambia nafaham kuhusu ethics na ethics it goes together with job satisfaction!walimu hawani wa Tanzania hawna job satisfaction,na pia hawasikilizwi wakiongelea matatizo yao,so lazima wakose ethics which imepelekea matokeo haya mabaya ya form four na ROOT cause ni serikali ya ccm!

Kama mtu hayuko satisfied na kazi anayofanya si arisign, akafanye kazi inayomridhisha, kwa nini imefikia hatua ya kujipa vifungo vya kazi? kama kweli kufail kwa wanafunzi ni reaction ya walimu kwa serikali kushindwa kutimiza madai yao, basi hao walimu ni wajinga kabisa.
 
As if TZ kuna machaguo ya kazi.
Wangekuwa wajinga kama wangeacha kazi na kuwa jobless. Weka input ndogo upate output kidogo; so wanadeliver kutokana na serikali yenu inachowapa, la watakuwa mafala kuibiwa nguvu zao.

Private schools mwalimu wa primary (ndugu yangu) ana degree ya ualimu na anaondoka na 1.5m per month na anadeliver kazi yenye same thamani. So mwl anayelipwa .3m tegemea na kazi yake itakuwa pungufu mara 5 ya anaye lipwa 1.5m
 
Feza boys n girls zipo wilaya gani?
Teh teh, ziko Wilaya ya Kinondoni, teh, lakini siyo shule za Manispaa, ni binafsi. Wakati wengine wanakuwa na uchungu wa kweli kwa matokeo haya wengine mnajaribu kutafuta sababu
ya kuwaona wapuuzi kwa sababu ya uchama, tutafika kweli?
 
Labda tungeanzia na kujiuliza kama uongozi wa juu kama kiti cha urais, uwaziri mkuu, uwaziri hauna ethics? Maana matatizo yote yanaanzia huko. Hatuwezi kutegemea kuona ethics za kazi kwa walimu kama huko juu hakuna ethics.

Hivi kwa nini inaonekana kama vile ni jambo la kuidhihaki serikali eti kwa sababu walimu wamefelisha wanafunzi kwa sababu madai yao hayakusikilizwa,hii kazi ya ualimu haina ethics?
 
Wivu tu mbona wabunge wengibwa cdm majimbo yao hayana division 1!!
Shule za serikali, mitaala inatolewa na serikali, walimu wanalipwa na serikali, loh, ndugu yangu, unajua wazi kuwa hapo CDM MPs got nothing to do with it, so why do you come out with this?
 
Kawambwa ni ndugu wa damu wa Kikwete.

So hii nchi ni ya Kikwete na ndugu zake??. Huu ndio ukweli wa mambo japo unauma sana kwa kweli. Sina wa kumlaumu kwenye hili zaidi ya watanzania nikiwemo mimi mwenyewe.

Halafu Kawambwa hiyo Phd yake ni ya nini na aliisomea wapi? Juzi kanishitua kweli aliposema nanukuu " Watu wanailaumu serikali mbona hata shule za private nao wamefeili kwanini msiangalie matokeo"? Mwisho wa kunukuu. Kawambwa amesahau kwamba serikali inawajibika hata kwa shule za binafsi meaning hao pia wanapaswa kufaulu na ni kazi ya serikali ya kutengeneza mazingira hayo ya kufaulu. Lakini pia kwa mujibu ya maelezo yake ni kama ni vile ni sahihi kwa sekondari za serikali kufeli kwa kuwa na za private nazo zimefeli this is pathetic indeed.
 
Hivi kwa nini inaonekana kama vile ni jambo la kuidhihaki serikali eti kwa sababu walimu wamefelisha wanafunzi kwa sababu madai yao hayakusikilizwa,hii kazi ya ualimu haina ethics?

Mkuu, hao viongozi wetu wa serikali wao wanafanya kazi zao kwa kufuata hizo ethics? Ukijiuliza mara mbili unaweza ukapata majibu ya swali lako.
 
As if TZ kuna machaguo ya kazi.
Wangekuwa wajinga kama wangeacha kazi na kuwa jobless. Weka input ndogo upate output kidogo; so wanadeliver kutokana na serikali yenu inachowapa, la watakuwa mafala kuibiwa nguvu zao.

Private schools mwalimu wa primary (ndugu yangu) ana degree ya ualimu na anaondoka na 1.5m per month na anadeliver kazi yenye same thamani. So mwl anayelipwa .3m tegemea na kazi yake itakuwa pungufu mara 5 ya anaye lipwa 1.5m

Kaunga sikubaliani na wewe.
Namna hii hatuwezi kujenga hii nchi, kama ni swala la mishahara midogo nchi hii kila sekta ina mishahara midogo, namna hii ni kuwafanya ng'ombe kuwa na akili kuliko binaadamu, ng'ombe akikataa kunywa maji hanyw'i ng'o, kwa nini walimu wanashindwa kukataa kufundisha kama wanaona hawapati wananchokitaka.

naona watu wote tumeamua kuangalia upande mmoja tu kiasi cha kusababisha ionekane walimu hawawajibiki kwa namna yoyote ile na hili tatizo.

Mimi binafsi nimesoma katika shule za namna hii hii, walimu wanapata pesa nyingi tu kwenye tuition hasa mjini, wajijini wanaweza kujikimu vizuri tu kwa kilimo, na wengi wanafanyisha wanafunzi kazi kwenye mashamba na bustani zao, in fact kila sehemu wanayohishi walimu wanapata favor nyingi sana, achilia mbali heshima wanayopewa, leo wanabehave kiajabu ajabu watu mnajitokeza kutetea.

sisemi kwamba hawastahili kupatiwa malipo mazuri, lakini nchi hii nani analipwa vizuri, watu wanataja wanasiasa na wakuu wenginine serikalini, wakati hawa tayari kuna agenda iyosambaa nchi nzima kwamba ni mafisadi, au ndio tumefikia hatua ya kutamani ufisadi wao?
 
Nipo kwenye mkutano wa hadhara hapa mwananyamala!makamanda wanaungurumisha wakiongozwa na mh. Jj Mnyika!diwani wa kata ya Saranga ametoa taarifa kwamba shule za manispaa ya kinondoni zipatazo kumi na saba division one ni tano tu!haya yote ni matokeo ya uozo wa mfumo m'bovu wa ccm!kaa chonjo 2015 mabadiliko lazima!

Wewe + Mnyika + huyo diwani = vichaa.

Unaijua manispaa ya kinondoni na mipaka yake? unajua shule zilizopo ndani ya manispaa ya kinondoni? kwa kukusaidia moja ni Feza boys, na yenyewe pekee ina div one (1)=48, div two (2)=20 na div (3) 8. Sasa hao wapuuzi wenzio kawashauri ya kwamba, div 1 sio jambo la msingi sana na wenda hata wao hawakuipata, cha msingi ni kile kiwango cha ufaulu kilichowekwa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kufikiwa.
 
Hivi kwa nini inaonekana kama vile ni jambo la kuidhihaki serikali eti kwa sababu walimu wamefelisha wanafunzi kwa sababu madai yao hayakusikilizwa,hii kazi ya ualimu haina ethics?

Nadhani vema kuanza kujiuliza kama siasa ina ethics kuliko kuanzia kwa walimu ndo tutapata uhakika wa mazungumzano. Vinginevyo tunapoteza muda...! Kwa maoni yangu siasa ya TZ haina ethics na kwa hiyo mengine yote yanakosa ethics na ndo maana kuendelea ni ndoto za mchana. Tukitaka kwingine kote kuwe na ethics, tuanzie kwa viongozi (siasa) maana ndo watunga sera, watekelezaji na wawajibishaji. Kama hawana ethics nani atawajibika kwa watoto kufeli?
 
hebu wewe tupe hizo sahihi ulizo nazo kama hizi sio sahihi....

very simple........kama nchi nzima kuna div 1 alfu moja na kitu tu......je kuna wilaya ngapi?........gawanya utapata wastani wa ufaulu kwa kila wilaya!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom