elia stephen
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 263
- 82
Ukiwa mwerevu na uelewa mdogo utaonekana mjanja sana kwenye kundi la wapumbavu...sasa kwani kutoa misaada kunaleta tija gani?Lowassa hajaanza leo wala jana huwa anatoa misaada kibao tu.
Vipi ile miiezi sita aliyotoa kwa walioingia hakmashauri kuu kinyemela??? Hana lolote huyu
mkuu kama anawazingua si wamfukuze.Wanamwogopa kama ukoma.Vibabu vingine bwana. Vijiendee kulima nyanya kule Ilula. Mfupa mgumu huo, ni rahisi kutamka EL lakini kumfikia si rahisi. Mbona mzee unasahau kanuni za chama??? VIKAOOOO. Itisheni kikao cha CC cha dharura. Mjadili mtoe tamko. Usikurupuke tu ukajisemea baadaye M/kiti wako akamwinua mkono na kusema; EL ni jembe. Jifunzeni kwa makosa ya nyuma tu.
Kweli mkuu, EL ni tatizo ambalo Mwenyekiti wa CCM alitatue mwenyewe.Vibabu vingine bwana. Vijiendee kulima nyanya kule Ilula. Mfupa mgumu huo, ni rahisi kutamka EL lakini kumfikia si rahisi. Mbona mzee unasahau kanuni za chama??? VIKAOOOO. Itisheni kikao cha CC cha dharura. Mjadili mtoe tamko. Usikurupuke tu ukajisemea baadaye M/kiti wako akamwinua mkono na kusema; EL ni jembe. Jifunzeni kwa makosa ya nyuma tu.
Kweli mkuu, EL ni tatizo ambalo Mwenyekiti wa CCM alitatue mwenyewe.
muacheni atafute riziki yakeMangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!
Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!
-------------------------
------------------------------
CCM WAAMUA KUMTELEA UVIVU LOWASSA MBIO ZA URAIS 2015
Unaweza kusema sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kumfungia kazi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya jana Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Phillip Mangula kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015 watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;
Wapo watu wanataka waichanechane CCM kwa sababu ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi kuyafumbia macho.
Akifafanua hilo Mangula alisema: Tutawaita wote walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu, tunajua dhamira yao ni nini.
Mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kusema mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.
Nape alitoa kauli hiyo baada ya Lowassa siku mbili zilizopita, kutangaza nia kimtindo akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.
Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.
Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho wanaoutaka urais jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati ya Siasa tawi la Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wote wa CCM nchini.
Ataja kanuni za uongozi
Katika mkutano huo Mangula alisaidiwa kusoma kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali na Katibu Tume ya Udhibiti wa Nidhamu ya Viongozi wa CCM na wanachama taifa, Masoud Mbengula.
Moja ya kanuni hizo inasema Ni mwiko kwa kiongozi wa CCM kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono.
Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.
Duh mkuu umetoa mfano mzr sana, kimsingi hoja c el bali wanachekecha upepo wa siasa ili wajue kama anakubarka. Ki msingi sioni njia ya edo kupitia may b watu wote waliokuwepo wakati wa kashifa wawe wamekufa, halafu kiibuke kizaz kingine! Maana wakimpitsha edo ssm itapata vit vya ubungo bt urais itatafuna kwao. Pole edo njia uliharbu mwenyeweee!Acheni kuimba wimbo wa taifa,,,,simtetei,,,,njooni na ushaidi wa utajiri wake,,,semeni ana nini labda LAKE OIL,,,,na naniii
Kama Lowassa amevunja kanuni za chama mbona hawamfukuzi na kumpokonya kadi ya chama? Mansoor Yusuf Himid wa Kiembesamaki Zenji alifukuzwa uanachama na kupokwa kadi kwa sababu alitetea muungano wa mkataba, ilhali hio si sera ya CCM. Kama kuanza kampeni za uraisi mapema si sera ya CCM basi wampoke kadi Lowassa! Wanaogopa nini?Ni kweli, na nimemuomba mode aufunge!.
Masikini, namhurumia Mangula na Nape!, they simply don't know the name of the game!.
Pasco.