Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula: Lowassa bora uondoke kuliko kuivuruga CCM

Mangula makamu mwenyekti wa CCM Taifa amepigilia msumari mkali kwenye ndoto ya Edward Lowassa kwa kumwambia bora aondoke kwani hata simamishwa na CCM kama mgombea wake wa Urais kwani matendo anayofanya yanampoyezea sifa ya kuwa mgombea wa CCM labda chama kingine!

Kayasema hayo leo mchana Lumumba CCM Sub HQs!

-------------------------



------------------------------

CCM WAAMUA KUMTELEA UVIVU LOWASSA MBIO ZA URAIS 2015



Unaweza kusema sasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamua kumfungia kazi Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa baada ya jana Makamu Mwenyekiti wake (Bara), Phillip Mangula kusema kuwa wanachama wake walioanza mbio za kuwania urais mwaka 2015 watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Mangula alisema kama wanachama hao wasipochukuliwa hatua watakifanya chama hicho kupoteza mvuto katika medani ya kisiasa nchini;

“Wapo watu wanataka waichanechane CCM kwa sababu ya uroho wao wa madaraka, uroho wa udiwani, ubunge na hata urais. Kuna makundi ndani ya chama kazi yake ni kuwabomoa wenzao, kamwe hatuwezi kuyafumbia macho.”

Akifafanua hilo Mangula alisema: “Tutawaita wote walioonyesha nia ya kuutaka urais 2015 na kuwahoji kwanini wanafanya hivyo wakati muda bado haujafika. Tumeshawachunguza katika mikutano wanayoifanya, tumebaini kuwa wanatoa misaada na kusafirisha watu, tunajua dhamira yao ni nini.”

Mangula ametoa kauli hiyo ikiwa imepita siku moja tangu Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye kusema mwanachama yeyote wa CCM anayetangaza nia ya kuwania urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa atapoteza sifa za kugombea.

Nape alitoa kauli hiyo baada ya Lowassa siku mbili zilizopita, kutangaza nia ‘kimtindo’ akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumaini ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.

Mangula aliwashukia vigogo wa chama hicho wanaoutaka urais jana katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Kamati ya Siasa tawi la Ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, wakati akitoa salamu za mwaka mpya kwa wanachama wote wa CCM nchini.

Ataja kanuni za uongozi

Katika mkutano huo Mangula alisaidiwa kusoma kanuni za uongozi na maadili ya chama hicho, kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali na Katibu Tume ya Udhibiti wa Nidhamu ya Viongozi wa CCM na wanachama taifa, Masoud Mbengula.

Moja ya kanuni hizo inasema “Ni mwiko kwa kiongozi wa CCM kutumia dini yake au kabila au rangi au jinsia au eneo analotoka, kama sifa ya kushawishi wapiga kura wamchague ama yeye mwenyewe ama mgombea anayemuunga mkono.”

Mangula alisema kwa mujibu wa kanuni za chama hicho, mwanachama anayefanya mambo kinyume na kanuni huitwa msaliti na hafai kuendelea kufumbiwa macho kwani anaweza kukiangamiza chama wakati wowote.

Too late, babuu
 
Kikwete asisema
Wanaotaka urais waanze kujipitisha mapema ili wananchi wawajue.sasa kosa-la lowassa nini kwanini.wasimwachetu.ili wajewamkwamishe kwenye michakato yakuteua majina ccm wanahofianini kwa mtu huyu
 
Mzee Mangula nae ni MZIGO tu. Tangu amewadanganya wadanganyika kuwa ndani ya miezi sita atakuwa ameshawaondoa walioingia kwenye uongozi wa ccm kwa Rushwa mbona hajafanya lolote?

Je kati ya Lowassa na Mwigulu nani anastahili kufukuzwa?

Lowassa na Jk walikuwa wanakusanya(kuiba) Tsh.152,000,000/- kila siku mfululizo kwa zaidi ya miaka 2 bila umeme kuwaka(Richmond)

Mwigulu alitupa bomu kwenye mkutano wa cdm watu wakafa achilia mbali kushikwa ugoni Igunga.

Ccm imesheheni MIZIGO

WAPIGWE TU TUMEWACHOKA.
 
Mangula amesahau yaliyompata 95 ,ushauri wangu yeye akae kimya matamko amwachie katibu mwenezi
Yaani Mara hii ameshiba amesahau njaa ya juzi. EL akiingia ikulu tena kupitia CCM atafanyaje na hayo Matamko
 
Kweli mkuu, EL ni tatizo ambalo Mwenyekiti wa CCM alitatue mwenyewe.

Kwanza huyu mzee Mangulla anajiumauma midomo tu hapa. Anatuhakikishia kuwa CCM kuhonga ndiyo siasa wanayoijua. Ndo maana anasema wasianze mapema mno kuanza kuzisambaza. Wameambiwa wangojee kengele ili zimwagwe nchi nzima.
Wataanza na kugombea udiwani, wazimwage kila kata Tanzania, waje wabunge wazimwage kila jimbo la uchaguzi. Ndipo apite huyo EL mwenyewe akitoa ahadi za kuwaletea maisha mema vijana. Atawakumbusha boda boda alizowanunulia hivyo hizo ahadi hewa wataziamini tu na kumpa kura zote.
Lazima mzee Mangula ajifanye kukemea lakini hiyo tunaijua ni janja ya nyani tu. Huna meno ya kumng'ata mtu Mangulla. Acha tu kelele unaharibu hewa bure.
Si unaona amekujia hapo hapo lumumba ofisi ndogo J2 ijayo. Hebu ipige stop, kama sio hivyo tutajua ccm yako ipo nyuma ya huo mpango mzima wa EL.
 
CCM hawana ubavu wa kumshugulikia Lowasa! Wathubutu waone cha moto! JK mjanja! Kama EL kusimamishwa atasimamishwa dakika za mwisho ili asipate pa kujishika! Lowasa atatoka CCM akitaka ingawa akitoka dakika za mwisho atakuwa kachelewa!
 
Ni Lowassa pekee mwenye uwezo wa kusimama na CHADEMA 2015 akawasumbua.Msipomchagua huyu tegemeeni maumivu makali.Hata mkipitisha hao wagombea wenu wengine ambao wengi ni vibaraka wa mataifa ya kibeberu(kama mzee wa "safari") halafu mkaiba kura na kushinda, kwa namna watakavyoendesha nchi kwa maslahi ya mataifa ya nje(kama hivi sasa) ni lazima tutaingia kwenye machafuko.Angalia nchi ilivyofilisika na inavyoyumba hivi sasa.Kila kitu hadi elimu wameharibu makusudi ili nchi ikose wasomi wa kuwachallenge watoto wao na mabeberu huko mbele.Namwelewa sana Eddo boy anapopigania elimu.Kuna jambo analijua.Kuna mpango wa uovu anaoupiga vita.Ndio maana baada ya kujiuzulu yeye shule za kata(mpango wake) zimekosa mwelekeo.Hii network ya vibaraka tusilogwe tukaipa nafasi watz wenzangu,tutalia sana,hawana uchungu na nchi.Kura yangu ya kwanza iko kwa Slaa,ya pili iko kwa "Eddo boy".Hawa ndio watu pekee wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya watz dhidi ya Barrick,Statoil,ExxonMobil n.k
 
Ni Lowassa pekee mwenye uwezo wa kusimama na CHADEMA 2015 akawasumbua.Msipomchagua huyu tegemeeni maumivu makali.Hata mkipitisha hao wagombea wenu wengine ambao wengi ni vibaraka wa mataifa ya kibeberu(kama mzee wa "safari") halafu mkaiba kura na kushinda, kwa namna watakavyoendesha nchi kwa maslahi ya mataifa ya nje(kama hivi sasa) ni lazima tutaingia kwenye machafuko.Angalia nchi ilivyofilisika na inavyoyumba hivi sasa.Kila kitu hadi elimu wameharibu makusudi ili nchi ikose wasomi wa kuwachallenge watoto wao na mabeberu huko mbele.Namwelewa sana Eddo boy anapopigania elimu.Kuna jambo analijua.Kuna mpango wa uovu anaoupiga vita.Ndio maana baada ya kujiuzulu yeye shule za kata(mpango wake) zimekosa mwelekeo.Hii network ya vibaraka tusilogwe tukaipa nafasi watz wenzangu,tutalia sana,hawana uchungu na nchi.Kura yangu ya kwanza iko kwa Slaa,ya pili iko kwa "Eddo boy".Hawa ndio watu pekee wenye uwezo wa kusimamia maslahi ya watz dhidi ya Barrick,Statoil,ExxonMobil n.k

Lowassa alikuwa mzigo kwa Taifa

Lowassa amekuwa mzigo CCM

Lowassa hata kwa vipi hawezi kupeperusha bendara ya chama makini kama CCM..

Chama ambacho kinafanya maamuzi kwa kufuata kanuni na maslahi ya taifa tangu enzi za mwalimu.
 
Sasa Bwana ACHEBE kwanini hukuingia hapa kwa jina lako tulilolizoea? Nimeuliza tu lakini
 
Last edited by a moderator:
Kama Lowassa amevunja kanuni za chama mbona hawamfukuzi na kumpokonya kadi ya chama? Mansoor Yusuf Himid wa Kiembesamaki Zenji alifukuzwa uanachama na kupokwa kadi kwa sababu alitetea muungano wa mkataba, ilhali hio si sera ya CCM. Kama kuanza kampeni za uraisi mapema si sera ya CCM basi wampoke kadi Lowassa! Wanaogopa nini?
itakua hatari kwa ccm wakijaribu hilo. mi naona mkono wasioweza kuukata waulambe tu.
 
Lowasa kiboko, akipiga chafya Lumumba yote inatikisika, je akija 4WD si ndiyo mwisho wa CCM? Kusema ukweli CCM wooooooooooooooote wanamgwaya huyu jama yaani hawamuwezi.
 
El hawezi kuwa rais, nani anataka mafisadi wachuku
e nchi? Urais gani wa kununua , mangula mtoseni huyoo jamaa, ww muache haangaike lkn nchi hachukui, watanzania wa leo hawajalala
 
We mzee umekosa cha kusema wew, unafata upepo ehh,muachenii lowasa afanye yake hautakii pigana sas tukuone, alf kama c ujinga hamuoni kuwa nyie ni wajinga mnamsema m2 yy kakaa kimya anawaona jinsi mlivyo mabwegee, nyie ccm hamna jipyaa nyiee mkalale mbele
 
Back
Top Bottom