Mangula, Kinana Na Hatima ya Taifa Letu


Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Mwongozo wa CCM (1982) umetuwekea utaratibu mzuri sana wa kukabiliana na changamoto ndani na nje ya chama, na laiti viongozi wetu wangekuwa wanazingatia utaratibu huu, ni dhahiri CCM ingeweza kupunguza migogoro mingi inayoikabili sasa; Moja ya urataribu huu ni ule unaohimiza juu ya umuhimu wa kukosoana, kama njia ya kujenga na kuimarisha Chama; Kwa mujibu wa ibara ya 57(5) ya mwongozo wa CCM (1982): "Kujikosoa na kukosoana ni silaha ya Mapinduzi". Ibara ya 58 inazidi kutamka kwamba:

"Ni kweli kuwa katika TUJISAHIHISHE Mwalimu anasisitiza jambo hili na kwamba Katiba ya CCM inatamka waziwazi juu ya umuhimu wake. Lakini ni kweli pia kuwa hatujaijenga tabia hii ipasavyo. Mara nyingi tumependelea kuteteana, kufichiana makosa na hata kutafuta visingizio visivyo na msingi".

Hivyo ibara ya 59 ya mwongozo (1982) inahimiza kwamba:

"Suala la kukosoa, kujikosoa na kukosoana lina sura kadhaa. Kwanza linataka wanachama na viongozi kuwa tayari kusema kweli katika vitendo vyao na kukubali kuambizana ukweli. Pili, linataka wanachama na hasa viongozi wawe tayari kukosolewa bila kuhamaki na inapobidi kukubali kujirekebisha. Tatu ni kuwa Chama chenyewe katika vikao vyake vya ngazi mbalimbali kuwa na utaratibu wa kujikosoa."

Ni katika muktadha huu ndio nimekuja na mada yangu ya leo, ambapo kimsingi, kama mwanachama wa CCM, nalindwa na Kanuni hizi; Ni muhimu tukaambiana ukweli bila ya kufichana, kuteteana, au kuwa wanafiki kwamba - CCM ipo katika kipindi kigumu kuliko vingine vyote katika historia ya Chama; Ni muhimu tufahamu pia kwamba - Hatima ya CCM na Taifa kwa ujumla kwa sasa ipo mikononi mwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Aburahaman Kinana; Miaka ya tisini, Mwalimu alipata kuonya kwamba "CCM ikiyumba, Nchi nayo itayumba", na onyo la Mwalimu linazidi kufikia ukweli; Sote tunajua kwamba Hatima ya kitu chochote kinacho yumba ni aidha kudondoka na kuvunjika/kubomoka au kurejea kwenye Uimara na Utulivu; Outcome ya haya mawili itategemea sana nini kinafanyika kukabiliana na tatizo husika/kuyumba; Hii ndio changamoto kubwa sana ya Mangula na Kinana kuelekea 2015; Nitajitahidi kufafanua;

Hoja yangu ya msingi ipo katika maeneo makuu mawili; Kwanza ni kuhusiana na changamoto za Mangula na Kinana za kurudisha Chama katika hali ya uimara na utulivu, na hivyo nchi kurudia katika hali ya uimara na utulivu hasa kuelekea 2015; Na ni uimara na utulivu huu ndio utakaosaidia CCM (na nchi) isianguke, isibomoke, na badala yake kuivusha nchi salama 2015, huku CCM ikiendelea kuaminiwa na wananchi walio wengi kuendelea kukamata Dola; Eneo la Pili la hoja yangu inahusiana na haja na umuhimu wa Mangula na Kinana kuhakikisha kwamba iwapo kazi hii itawashinda, na kupelekea Chadema kuingia Ikulu 2015, historia itawakumbuka daima kwa shinikizo lao la kuhimiza Mgombea Wa CCM na Chama kwa ujumla kukubali matokeo ya uchaguzi na kuipisha Chadema ikamate dola kutokana na ridhaa ya wananchi walio wengi;

Nikianza na hoja yangu ya kwanza - kitendo cha Mwenyekiti kuwateua Mangula na Kinana kushika nyadhifa za juu katika chama inatoa tafsiri moja tu kubwa kwamba: Mwenyekiti wa CCM Taifa ameshindwa kuja na mikakati ya kukivusha chama salama 2015, hivyo ameona uwepo wa Mangula na Kinana utamsaidia kufanikisha kazi hii pevu; Mwaka 2015, Mangula na Kinana watakuwa ndio nguzo kuu za kuibeba CCM katika Uchaguzi Mkuu wa nne wa vyama Vingi Tanzania, ambapo CCM itakuwa inatafuta ridhaa ya wananchi kuendelea kukamata dola kwa mwaka wa 54 mfululizo; Mwaka 2015, Mwenyekiti wa CCM Taifa atakuwa anamalizia muda wake madarakani kama Rais, na pia atakuwa anajiandaa kumwachia mikoba ya Chama mwana CCM mwingine, bila ya kujalisha kama CCM itaendelea kukamata dola 2015 au itakuwa chama cha upinzani;

Hivi sasa nchi inayumba kisiasa, kiuchumi na kijamii, kwa sababu CCM ina mizizi mirefu na inagusa maisha ya watanzania katika nyanja zote hizi tatu; Ingawa uteuzi wa Mangula na Kinana ni wa manufaa, uamuzi huu kidogo umechelewa, na hii inapelekea Mangula na Kinana kukabiliwa na changamoto nyingi sana za kurudisha hali ya CCM na Taifa kwa ujumla kuwa shwari; Moja ya changamoto kubwa zinazowakabili viongozi hawa wawili ni kurudisha chama katika msingi yake, hasa ile iliyojengwa na Mwalimu Nyerere, bila ya kukipasua Chama; Vinginveyo mpasuko wa CCM haupo mbali na utaleta madhara makubwa sana kwa taifa - kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa sababu tulizojadili hapo juu;

Nikija kwenye hoja yangu ya pili, ni muhimu tuambiane ukweli kwamba enzi za CCM kuwa na uhakika wa kushinda uchaguzi mkuu imepitwa na wakati; Na hii haijatokana na nguvu za upinzani, bali Udhaifu wetu wenyewe kama Chama; Mwaka 1995, Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba "Watanzania Wanataka mabadiliko, Na Wasipoyapata Kupitia CCM, Watayatafuta Kupitia Chama Kingine."; Iwapo Mwalimu Nyerere angekuwa hai leo, ni dhahiri kwamba neno Chama Kingine, angelibadili na kuweka "CHADEMA";

Tangia enzi za uhai wake, Mwalimu alikuwa anaionya sana CCM kwamba kinazidi kuacha misingi yake, na pia kinazidi kukaa mbali na base yake ambayo ni wakulima na wafanyakazi; Kwahiyo nguvu ya Chadema, hasa kupitia M4C sio suala la bahati mbaya au ajali, bali ni la uzembe wetu kama Chama; Tutambue kwamba Kiu ya mabadiliko miongoni mwa wananchi haijaletwa na Chadema; Kiu hii ilikuwepo hata wakati Chadema ilipokuwa na miaka michache sana ya uhai wake (rejea mafanikio ya NCCR Uchaguzi wa 1995); Wananchi wamekuwa na Kiu ya mabadiliko kwa muda mrefu, na walichokuwa wanasubiria kwa miaka yote hii ni mawili: Aidha CCM itakayorejea katika misingi yake, au Chama Mbadala ambacho kitaonyesha kuwajali; Kwa vile CCM imeonekana kutojali sana kubadilika kwa manufaa ya wananchi, Chadema imegeuka kuwa mbadala wa wananchi wengi katika kutafuta Maisha bora kwa ajili yao na watoto zao;

Kwahiyo kauli za baadhi ya viongozi wa CCM kwamba bila ya Chadema, wananchi wangekuwa hawana Kiu ya mabadiliko, haijengi Chama Chetu bali inakibomoa kwani imani hii inapingana na ukweli wa mambo; Pia ni muhimu kwa Viongozi wa CCM kukumbuka walipotoka, hasa kwamba kwamba suala la Political Movement ni suala la kawaida katika siasa za ushindani, kwani hata TANU, haikuanza kama Chama Cha Siasa bali "A Political Movement", na ni baadae ndio ikaja kuwa Chama Cha Siasa; Vinginevyo kwa muda mrefu, TANU (kuanzia na TAA) ilikuwa inaendesha harakati kama za Chadema (M4C), kwahiyo kitendo cha baadhi ya viongozi wa CCM kukebehi M4C ni sawa na kusaliti historia ya chama chetu cha CCM; Ni muhimu CCM ijue kwamba - Uhuru wa kiuchumi bado haujapatikana miongoni mwa watanzania wengi, na huu ndio msingi na pia mafanikio ya M4C;

Iwapo CCM itaanguka 2015, ni dhahiri nchi itapata mtikisiko mkubwa; Lakini kusema hivi haina maana kwamba wananchi waache kutafuta mabadiliko kupitia Chadema; Hoja yangu ya msingi hapa ni kwamba iwapo wananchi wataendelea kutoridhika na utawala wa CCM, ni muhimu kwa CCM kuanza kujiandaa kisaikolojia kuipa Chadema ushirikiano iwapo CCM tutaanguka 2015 kutokana na wananchi kuamua kuipa Chadema dhamana ya kuongoza dola; Siku matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 yatakapokuwa yanatangazwa, ni dhahiri kwamba Mangula na Kinana watakuwa ni miongoni mwa watu wachache na muhimu watakaokuwa karibu na Mgombea Urais husika wa CCM kufuatilia matokeo hayo; Katika hili, yapo masuala mawili makuu kwa Mangula na Kinana:

Kwa upande mmoja, iwapo CCM itatangazwa mshindi, kihalali, Mangula na Kinana wataingia katika historia ya nchi kama viongozi walio iokoa CCM pengine na kuifanya pengine iendelee kutawala kwa muda mrefu zaidi; Kwa upande mwingine, iwapo CCM itashindwa kihalali, nchi itakuwa mikononi mwa Mangula na Kinana kwa manna ya kwamba - watakuwa ni watu muhimu sana katika kumshauri mgombea wa CCM pamoja na CCM kwa ujumla juu ya uamuzi wa kuyakubali au kuyakataa matokeo ya uchaguzi; Ushauri wao, hasa juu ya kukubali matokeo, utawaingiza katika the right side of our country's history na watakuwa mashujaa kwa vizazi vingi; Kwahiyo, Uwezo wa Mangula na Kinana kusimamia CCM ivuke salama 2015 na kuendelea kutawala kihalali, na bila ya kupasuka vipande vipande, na pia busara zao kumshauri mgombea wa CCM na chama kwa ujumla kukubali matokeo ya Uchaguzi iwapo Chadema itashinda, ndio msingi mkuu wa hoja yangu kwamba Hatima ya CCM na Taifa kwa jumla ipo mikononi mwa Mangula na Kinana;

Katika Uchaguzi mkuu wa kwanza wa Vyama Vingi Zambia Mwaka 1991,Chama tawala cha Zambia – UNIP, kiliamini kwa uhalali kabisa kwamba wananchi (maskini) wa Zambia bado wangekuwa na shukrani kwa UNIP ya kuwaletea uhuru na kudumisha amani, utulivu na umoja wa taifa; Kwahiyo UNIP iliamini kwa dhati kabisa kwamba wananchi wa Zambia wangefanya uamuzi sahihi kwenye sanduku la kura, yani KUIPA UNIP KURA ZOTE ZA NDIO; Tofauti na matarajio haya, chama cha MMD- chini ya Chiluba, kikaibwaga UNIP kwa kura nyingi sana; Wazambia walichagua MABADILIKO (MMD), sio UNIP;

Baada ya matokeo haya, wasaidizi wa Kaunda ndani ya UNIP na Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wakakimbilia Ikulu kwenda kumuuliza Mzee Kaunda jinsi gani wageuze matokeo ya uchaguzi; Kwa wakuu hawa, ilikuwa ni jambo lisilokubalika kabisa kwamba Chama tawala, kilicholeta uhuru, na kujenga amani, utulivu na umoja, kiachie madaraka; Kwa pamoja wakamueleza Mzee Kaunda kwamba: ZAMBIA WITHOUT UNIP? NEVER! Baada ya Mzee Kaunda kuwasikiliza kwa makini, kwa busara zake, akaanza kuwapa somo refu sana juu ya umuhimu wa "WILL OF THE PEOPLE"; Wengi ya viongozi wale wa UNIP na USALAMA wakamkubalia kwa shingo upande; Usiku ule ule, Mzee Kaunda akampigia simu Rais Mteule – Fredrick Chiluba, na kumpa hongera ya ushindi na kumualika aende Ikulu mapema siku inayofuatia; Chiluba aliitikia wito ule, Mzee Kaunda akamtembeza Ikulu na kumpa wosia mwingi, huku akimuonyesha njia za dharura za kutokea ikulu, simu za dharura, maandaki ya kujificha n.k; Transition of Power ikatokea kwa amani na utulivu wa hali ya juu kwa sababu UNIP, chini ya Mzee Kaunda, ilikubaliana na "WILL OF THE PEOPLE";

Kutokana na uamuzi wake wa busara, leo hii Mzee Kaunda hayupo kifungoni kutokana na vifo vya raia wasio na hatia ambavyo lazima vingetokea iwapo UNIP ingeng'angania madaraka kinyume na will of the people; Mzee wetu huyu leo hii anaheshimika sana kimataifa, na kila kukicha anaalikwa katika vyuo mbali mbali duniani na mikutano mbalimbali kwenda kutoa somo juu ya Democracy in Africa; Na kwa vile UNIP haikujipanga kuishi bila ya kutegemea Serikali na Nguvu ya Dola, UNIP ikajikuta inaingia kwenye mgogoro mkubwa, ambao haukupatiwa ufumbuzi kwani katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana nchini Zambia (2011), UNIP ikapoteza kiti chake cha mwisho Bungeni; Hivi sasa, UNIP imebakia historia vitabuni;

Jinsi Gani CCM Itaweza Vuka Salama na Kwa Uhalali 2015

Kama nilivyosema hapo awali, pamoja na uamuzi mzuri wa kuteua Mangula na Kinana, uteuzi huu umechelewa kidogo, hivyo kupelekea viongozi hawa wawili kukabiliwa na changamoto nyingi sana; Kipindi muafaka cha uteuzi huu ilitakiwa iwe wakati ule Mwenyekiti wa CCM taifa alipounda kamati ya Kinana, Msekwa na Mzee Mwinyi imsaidie kuvunja makundi ndani ya chama; All that said and done, bado kuna uwezekano wa CCM kufanikiwa (ingawa itakuwa kazi sana), na sehemu ifuatayo itajadili baadhi ya maeneno muhimu towards that end;

Kwanza, ni muhimu kwa Mangula na Kinana kumshauri Mwenyekiti wao abadili mtazamo wake (kupitia hotuba ya ufunguzi Mkutano Mkuu Dodoma 2012) kwamba ukiachilia Siasa za makundi ndani ya CCM, Chama ni shwari na hakina matatizo yoyote makubwa; CCM inakabiliwa na matatizo mengine makubwa zaidi ya hilo; Kwa mfano, kauli aliyoitoa Marehemu Kolimba miaka 20 iliyopita kwamba CCM imepoteza DIRA bado ni kauli HAI; isitoshe, Kolimba aliyasema haya wakati CCM ilikuwa haina siasa za makundi; Uhai wa kauli hii unajitokeza katika maeneo ya Utekelezaji Holela wa Sera Za Soko Huria zisizokuwa na Tija kwa Wananchi kwani tofauti na enzi za azimio la arusha, chini ya azimio la Zanziabar, nchi haina ownership of its development agenda, Uhai wa kauli hii unajitokeza katika Ufisadi ambao ulifunguliwa mlango mchana kweupe na Azimio la Zanzibar (1992), na katika maeneo mengine mengi; Pamoja na mapungufu mengi ya Azimio la Arusha, mambo kama haya yalikabiliwa vilivyo kupitia POLITICAL WILL chini ya Mwalimu Nyerere; Ni Muhimu Uongozi wa CCM Taifa ukarudisha hii Political Will;

Pili, ili kuivusha CCM salama 2015, Mangula na Kinana wanahitaji kuja na Comprehensive Document i.e. Organizational Renewal Document ambayo itakuwa na SWOT Analysis ya Chama; Naposema SWOT analysis, maana yangu ni kwamba Chama kijifanyie uchambuzi wa kina ili kubaini nguvu za chama, udhaifu wa chama, fursa za chama, na mambo yanayotishia uhai wa chama; Ikiwezekana, CCM isifanye kazi hii yenyewe bali iteue timu kutoka nje ya nchi, hasa kutoka moja ya nchi za Jumuiya Ya Madola, kwani kwa utamaduni wa sasa wa CCM, haitakuwa ajabu kwa CCM kuchakachua hata matokeo ya utafiti unaohusu uhai wake wenyewe;

Baada ya Chama kubaini nguvu, udhaifu, fursa na vitisho vinavyokikabili, zoezi la kufuata liwe ni chama kuja na mikakati ya kutumia nguvu ya chama (sio nguvu ya dola bali ya CCM kama taasisi) kuondoa madhaifu, kutumia nguvu zake kuwekeza kwenye fursa zilizopo, kutumia nguvu zake kuondoa mambo yote yanayotishia uhai wa Chama, kutumia fursa zilizopo kuangamiza madhaifu, matishio n.k; Yafuatayo ni maeneo mengine muhimu ya kuyafanyia kazi:

1. Chama kije na mikakati to fire the imagination of the YOUTH, hasa ikizingatiwa kwamba ifikapo mwaka 2015, inakadiriwa kwamba 70% ya wapiga kura Tanzania watakuwa chini ya umri wa miaka 35; Na wengi kati ya hawa leo hii wanakabiliwa na tatizo la ajira, na umaskini wa kipato;

2. Chama kinahitaji kuja na mkakati wa kushinikiza nchi ipate ‘POLICY SPACE' kwenye utekelezaji wa Sera za Maendeleo ambazo hatuzimiliki bali zinamilikiwa na IMF, WorldBank na WTO; Sera hizi zimeachangia sana umaskini wa watanzania kwani zinahimiza Serikali kutoingilia Liberalization, Marketization, Privatization & Stabilization katika uchumi chini ya kanuni kwamba - ili tuondokane na umaskini, ni lazima UTAJIRI kwanza ujengwe na wachache walio juu, halafu utajiri huu ndio ushuke chini/trickle down kwa wananchi; Kwa miaka zaidi ya 25, CCM imekuwa ikitekeleza sera hizi, huku pengo la kipato baina ya walio nacho na wasio nacho likizidi kupanuka; Hivi sasa Tanzania ni nchi ya kumi na tano kutoka chini duniani kwenye kipato cha wananchi wake (based on the poverty indicator of people earning less than $2 a day); Its such an irony kwa nchi yenye utajiri mkubwa kuwa na wananchi maskini hivi;

3. Chama kinahitaji kuja na Effective Program to revamp mfumo yetu wa Elimu na Afya, kwani ni humu ndio HUMAN CAPITAL huzaliwa, nguvu kazi hujengwa na kuboreshwa, lakini pia RETURNS TO EDUCATION kwa watoto wetu hupatikana;

4. Chama kinahitaji Kuja na Land Tenure System Mbadala ambayo itakidhi mahitaji ya Wakulima na Wafugaji, itapatia nchi Food Security, na itasaidia maendeleo ya viwanda vidogo vidogo; Haya yatasaidia kurudisha imani ya wakulima kwa CCM kama awali;

5. Chama kinahitaji kufuata mfumo kama wa Botswana juu ya usimamizi wa rasilimali za taifa kwa manufaa ya umma, kwa mfano kwa serikali kushikilia hisa nyingi (ikiwezekana 50% kama Botswana) katika miradi husika Kwa niaba ya wananchi, chini ya mazingira transparent na yanayoweka maslahi ya taifa mbele;

6. Chama kinahitaji kuja na Sera ya Mambo Ya Nje ambayo itaweka Sub Saharan Africa at the centre, na dunia nje ya Afrika baadae; Bara la Afrika lina fursa nyingi sana za kiuchumi (masoko n.k). ambazo nchi serious kama Afrika ya Kusini, Kenya, ns Mauritious zinazitumia kikamilfu kukuza uchumi wao; Chini ya CCM, tumebakia kuangua vilio kuhusu madhara ya EAC, SADC, wakati kwa taifa lililojipanga, faida ni nyingi kuliko hasara;

7. Chama kinahitaji kupigania haki za Wafanyakazi kama vile, Mafao, Job Security, Mishahara inayoendana na hali zao za maisha, n.k; Hii itasaidia kurudisha imani ya wafanyakazi kwa CCM kama awali;

8. Pia CCM inahitaji kuanzisha mfumo wa mashauriano baina ya serikali yake na wananchi, hasa kuhusu maandalizi ya sera mbalimbali zinazohusu maisha ya wananchi, na kushirikisha wananchi katika maamuzi muhimu ya nchi kwa jumla; Mfumo huu ni muhimu uende mbali zaidi na mfumo wa sasa ambao ni wa Bunge, kwani mfumo wa bunge umejaa mapungufu mengi, hasa juu ya suala zima la ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi na maandalizi ya sera za maendelo;

8. Chama kinahitaji kurudia mfumo wake wa zamani wa leadership recruitment ambapo watanzania, hasa vijana walihisi kwamba fursa za kuchangia ujenzi wa taifa lao zilikuwa wazi kwa watanzania wote bila ya kujali dini, ukabila, uwezo wa fedha za kuhonga, mahusiano ya wazazi husika na Rais, Waziri Mkuu, au Viongozi wakuu wa CCM n.k, bali kutokana na sifa za mhusika (on merit) kama vile elimu, uzoefu, Uzalendo kwa taifa, n.k; Mfumo wa sasa ni wa leadership succession, ambapo wakubwa na matajiri wanapeana madaraka kiundugu, kifamilia, kirafiki, au kwa kuhonga chochote in Demand;

9. CCM lazima itambue kwamba Watanzania wamechoka siasa za kauli mbiu na misamiati ambayo miaka nenda miaka rudi, haiboreshi maisha ya watanzania, sana sana ina maintain maisa yao yawe duni, kama sio kuyadumaza; CCM itambue kwamba suala la utekelezaji wa ilani ya uchaguzi halitoshi kuletea wananchi mabadiliko, kwani mengi ya haya ni huduma za msingi kwa wananchi, to enable them to survive the next day, not to prosper into the future kwa kuwajengea wananchi uwezo mbalimbali; Ilani za Uchaguzi wa CCM zinatawaliwa na miradi inayopelekea survival of the majority, and prosperity of the few at the expense of the majority (their taxes); Mafanikio ya Chama cha Siasa hayapimwi kwa miradi ya kusaidia wananchi to survive the next day bali miradi itakayowasaidia wananchi to prosper into the future, hasa kwa kujengea wananchi capabilities mbalimbali; CCM tuna uwezo wa kufanya haya, tunachokosa ni POLITICAL WILL;

Watanzania wamechoka na empty promises, na pia hawataki Miradi ya Maendeleo inayojenga tu Kiini macho cha Maendeleo huku wanaofaidika na Miradi hiyo mikubwa mikubwa inayotokana na fedha za walipa kodi ni Viongozi na Familia zao; Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba watanzania wengi wapo tayari to share the burden (kulipa kodi kwa wingi kwa hiyari) kama miradi ya Maendeleo itakuwa ni kwa faida yao, na kama benefits are equally shared;

10. Iwapo CCM itarejea katika misingi yake, basi kijiandae kupambana na propaganda nyingi za kukiangusha, kutoka kila kona – kitaifa na kimataifa; Njia pekee ya kuinua wananchi ni kuendelea kushirikiana na IMF, World Bank na WTO BUT on our own terms; Nchi za Asian Tigers kama South Korea zilifanikiwa kwa kukaidi matakwa mengi ya World Bank, IMF na WTO, hasa kuhusu kuiondoa serikali kwenye uwekezaji katika maeneo yenya manufaa ya moja kwa moja kwa maskini; Serikali inatakiwa izalishe ajira za kisasa, ipatie vijana elimu na ujuzi wa kisasa, ilinde rasilimali muhimu kwa wananchi n.k; Tuhawahitaji sana IMF na WorldBank lakini pia we need ownership of our DEVELOPMENT AGENDA, na pia we need to have POLICY SPACE; Ni muhimu kwa Chama kujiandaa kuitwa ni Radical, au chama kinachorudisha Ujamaa from different quarters of the society, kama njia ya kuwatia hofu wananchi hofu; Lakini iwapo Chama kitakuwa na nia ya dhati ya kubadilisha maisha ya watanzania, hasa kwa kuwashirikisha katika maamuzi na pia katika kula matunda ya mafanikio, ni dhahiri wananchi wengi watakilinda chama dhidi ya propaganda za aina yote kutoka ndani na nje ya nchi;

Tukubali, tusikubali, Liberalization, Marketization, Privatization & Stabilization peke yake haziwezi ku - address the fundamental problems facing the majority of Tanzanians – hasa wa vijijini; Mabadiliko ya kweli kwa wananchi yatapatikana iwapo CCM itakuja na Dira na Itikadi ya vitendo inayoendana na matakwa ya wananchi vijijini; Ni muhimu itikadi hii iwe na elements za Ujamaa na Soko Huria kwa pamoja, lakini muhimu zaidi, iweze kukemea mapungufu ya Soko Huria na Ubepari, na ipatie Serikali ya ccm A POLICY SPACE, hasa katika kuingilia Uchumi kwa manufaa ya maskini, pale SOKO LINAPOFELI na kumwangamiza mwananchi;

Mabadiliko ya kweli lazima yatokane na itikadi ambayo itakuwa More Radical, itakayozaa National Autonomous Development Programmes/Policies na Vision, bila ya kujalisha kama itikadi na dira hii itabatizwa Ujamaa, Ujamaa wa Kidemokrasia au whatever; Kitu muhimu na cha msingi ni kwamba itikadi na dira hii MUST PUT PEOPLE at the CENTRE, badala ya hali ya sasa ambayo PEOPLE ARE PUT AT THE PERIPHERY, huku at the CENTRE wakiwekwa Wawekezaji, Matajiri, na Mafisadi, kwa imani kwamba, eti wao wakizalisha, wakitajirika na kupata chao, basi their WEALTH will trickle down to the poor; Kwa miaka zaidi ya 25 sasa ya utekelezaji wa sera za soko huria kiholela chini ya CCM, hakuna punje za maana za soko huria na ubepari zilizoangukia wananchi wa vijijini chini ya Kanuni eti ya kuachia watu wachache wa nje na ndani, wawe hati miliki ya rasilimali za wananchi kwa faida ya taifa;

Haya ni baadhi ya masuala muhimu ambayo Mangula na Kinana ni muhimu wayafanyie kazi iwapo nia yao ni kusaidia chama chetu kiigaragaze Chadema kupitia Sanduku la Kura 2015 - KIHALALI; Nje ya hapo, ni muhimu kwa Mangula na Kinana wajiandae kuja na ushauri wa busara kwa mgombea wetu wa CCM 2015 kwamba akubali "WILL OF THE PEOPLE", iwapo watachagua mabadiliko kupitia chama kingine kama Nyerere alivyoonya, kwani hii itasaidia nchi kuepuka machafuko kwa faida ya kizazi cha sasa na baadae; Kwa kufanya haya mawili, Mangula na Kinana wataingia katika the Right Side of History of Our Beloved Country - Tanzania;

Muhimu: CCM kumeguka na kuwa vyama viwili ni njia rahisi zaidi ya kutekeleza mengi ya masuala niliyojadili;

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI​
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
32,264
Points
2,000
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
32,264 2,000
Mkuu wangu; I have a different view of what the Mangula-Kinana axis means towards 2015. Nitashare nanyi nikimaliza kuandika hapa. Sijui kwa kiasi gani tutakuwa tunaangalia kitu kile kile.
 
Dingswayo

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
4,020
Points
1,250
Dingswayo

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
4,020 1,250
Kutokana na mfump wa CCM ulivyo sasa hivi, itakuwa vigumu sana kwao kutekeleza hayo uliyosema. Itakuwa dawa chungu sana kwao kumeza. Hii ni kama mlevi wa kupidukia anapoambiwa aache pombe vinginevyo atakufa karibuni kwa sababu ini lake limeanza kuharibika. Ndio kwanza atafungua chupa ya whisky ajiliwaze kutokana na mshtuko huo na vile kwa sababu hawi mtu kamili bila kunywa!

Sent from my GT-I9100 using Tapatalk 2
 
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Messages
3,577
Points
1,195
M

Mwanaweja

JF-Expert Member
Joined Feb 8, 2011
3,577 1,195
mkuu ulichokisema ni sawa ila kwa ccm kwa sasa hayatezekeleki kwa maana mfumo wote kuanzia chini hadi juu hauko sawa. kwaa kifupi ccm kwa sasa inatakiwa kiwe chama cha upinzani ili kijifunze na kujisahihisha pale kilipo kosea
 
Magwangala

Magwangala

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2011
Messages
2,082
Points
2,000
Magwangala

Magwangala

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2011
2,082 2,000
Samahani,makamu mwenyekiti wa CCM ni Philpo Mangula na katibu mkuu ni A.Kinana,ntarudi baadae!
 
Mwana Mpotevu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined
Sep 7, 2011
Messages
3,295
Points
1,500
Mwana Mpotevu

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Joined Sep 7, 2011
3,295 1,500
Nimesoma nimefika katikati, nimeweka alama maana usingizi umenikamata.

Asubuhi na mapema nitarejea kumalizia sehemu iliyobakia, I promise!
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Mchambuzi,

Kwanza nikubali kuwa mimi ni mvivu wa kusoma post ndevu. Lakini nimejaribu kuisoma hii na nikimaliza kazi zingine nitaendelea kuisoma.

Mimi ni mtanzania. Sina chama cha siasa na kwa uchambuzi wangu CCM kina matatizo hata kama kitarudi kwenye siasa za Nyerere na kuyafuta ya Nyerere aliyotaka. Kinachofanyika sasa ndani ya CCM ni kuchelewesha mabadiliko ya kweli ya nchi.

Umeeleza vizuri kuhusu utamaduni wa viongozi kukubali kukosolewa. Lakini tukumbuke ni rahisi kusema kuliko kutenda. Kutokana na mtaji huu kwanini unawashauri CCM warudi kwenye utamaduni ambao unawezekana kinadharia lakini sio kivitendo?

Ukweli wa mambo mfumo utakaobadilisha siasa ya Tanzania na kuleta maendeleo ni mfumo wa check and balance. Tusikubali mtu akosee kwanza afu akosolewe. Tuweke utaratibu wa watu kuchukua majukumu yao huku wakiangalia kushoto na kulia. Wakiangalia mbele na nyuma. Hili waakikishe kuwa wanachofanya kinakubalika na jamii. Wakikosea basi waachie ngazi na kuanza upya.

Wako,

Z10
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Mchambuzi,

Kwanza nikubali kuwa mimi ni mvivu wa kusoma post ndevu. Lakini nimejaribu kuisoma hii na nikimaliza kazi zingine nitaendelea kuisoma.

Mimi ni mtanzania. Sina chama cha siasa na kwa uchambuzi wangu CCM kina matatizo hata kama kitarudi kwenye siasa za Nyerere na kuyafuta ya Nyerere aliyotaka. Kinachofanyika sasa ndani ya CCM ni kuchelewesha mabadiliko ya kweli ya nchi.

Umeeleza vizuri kuhusu utamaduni wa viongozi kukubali kukosolewa. Lakini tukumbuke ni rahisi kusema kuliko kutenda. Kutokana na mtaji huu kwanini unawashauri CCM warudi kwenye utamaduni ambao unawezekana kinadharia lakini sio kivitendo?

Ukweli wa mambo mfumo utakaobadilisha siasa ya Tanzania na kuleta maendeleo ni mfumo wa check and balance. Tusikubali mtu akosee kwanza afu akosolewe. Tuweke utaratibu wa watu kuchukua majukumu yao huku wakiangalia kushoto na kulia. Wakiangalia mbele na nyuma. Hili waakikishe kuwa wanachofanya kinakubalika na jamii. Wakikosea basi waachie ngazi na kuanza upya.

Wako,

Z10
Zakumi,

Asante kwa mchango wako; Unayoyasema kimsingi nakubaliana nayo; ndio maana baadhi ya wachangiaji humu kama vile dingswayo wamejenga hoja kwamba CCM kutekeleza haya ni vigumu; Suala la msingi hapa ni CCM, lakini hasa Mangula na Kinana kujua kwanini Hatima ya Taifa letu ipo mikononi mwao; Nimejadili njia kuu mbili za kuokoa taifa letu lisizidi kuyumba, moja ni kujitahidi kufanyia kazi maeneo muhimu kama yale niliyoainisha, na pili, iwapo CCM haitabadilika, ni muhimu ikafahamu kwamba UMMA utaikataa 2015, hivyo viongozi kama Kinana na Mangula wajiandae kisaikolojia kutoa ushauri wa busara kwa mgombea wa CCM na chama kwa ujumla kukubali WILL OF THE PEOPLE, 2015;

Huo ndio ulikuwa ni msingi wa hoja yangu; Samahani kwa makala ndefu; Nia yangu huwa ni kuepuka maswali yasiokuwa ya lazima, kuepuka kutakiwa kutoa ufafanuzi, kuelezea assumptions n.k;
 
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2011
Messages
3,605
Points
0
C

Concrete

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2011
3,605 0
Hakuna chochote cha maana ambacho Mangulla na Kinana wanaweza kufanya ili kuinusuru CCM isianguke 2015, nafikiri ni bora wakafanya haya:
1/Kuiandaa CCM kukabidhi madaraka kwa CHADEMA kwa amani.

2/Kuaindaa CCM kuja kuwa chama cha upinzani imara.
 
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
834
Points
1,000
Y

ycam

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
834 1,000
Mkuu Mchambuzi, kwanza asante kwa makala zako za uchambuzi wa kina. Lakini ifahamike kwamba tatizo la CCM ni la kimfumo zaidi. Kinana and Mangula will have no impact on the performance of the party if the top leader (mwenyekiti) continues to be adamant on what real change in the party and government should look like. Remember already Kikwete has advisors who are probably more informed, experienced and educated than Kinana and Mangula. He even has the "intelligence"! Do you see any significant positive changes under his leadership? I see too few posivite changes under his leadership. It is unfortunate that most of the leadership changes CCM makes are for protecting and perpetuating the status quo in the party, as opposed to developing the country as a whole.
 
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2008
Messages
4,849
Points
1,500
Zakumi

Zakumi

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2008
4,849 1,500
Zakumi,

Asante kwa mchango wako; Unayoyasema kimsingi nakubaliana nayo; ndio maana baadhi ya wachangiaji humu kama vile dingswayo wamejenga hoja kwamba CCM kutekeleza haya ni vigumu; Suala la msingi hapa ni CCM, lakini hasa Mangula na Kinana kujua kwanini Hatima ya Taifa letu ipo mikononi mwao; Nimejadili njia kuu mbili za kuokoa taifa letu lisizidi kuyumba, moja ni kujitahidi kufanyia kazi maeneo muhimu kama yale niliyoainisha, na pili, iwapo CCM haitabadilika, ni muhimu ikafahamu kwamba UMMA utaikataa 2015, hivyo viongozi kama Kinana na Mangula wajiandae kisaikolojia kutoa ushauri wa busara kwa mgombea wa CCM na chama kwa ujumla kukubali WILL OF THE PEOPLE, 2015;

Huo ndio ulikuwa ni msingi wa hoja yangu; Samahani kwa makala ndefu; Nia yangu huwa ni kuepuka maswali yasiokuwa ya lazima, kuepuka kutakiwa kutoa ufafanuzi, kuelezea assumptions n.k;
Mchambuzi,

Hakuna sababu ya kuomba msamaha. Nitaisoma posti yote. Kitu kinachofanyika sasa ndani ya CCM sio kigeni katika masuala ya uongozi. Nilishawahi kutoa mifano mingi na nitarudia mmoja tu.

MIT -Massachusetts Institute of Technology, Ilikuwa inatoa ajira kwa maprofesa kwa wahitimu wa kutoa MIT. Waliamini kuwa wao ndio the best. Matokeo yake chuo kilianza kudorora kutokana na utamaduni wa kuelewana. Utamkosoa vipi mwalimu aliyekusimamia na kukupa kazi?

Tume huru iliyochunguza matatizo ya MIT ilishauri uongozi uanze ku-recruit watu wanaomaliza kutoka shule zingine na wenye sifa. Matokeo yake ubora ulirudi. Kwa mtaji huu MIT waliambiwa kuwa the world doesn't revolve around MIT.

Similary, Tanzania doesn't revolves around CCM. The top leadership itabidi ni lazima ikubali mabadiliko ya kuwaingiza vijana wenye damu mpya na idea ambazo zinafanya chama kikubalike na kizazi kipya.

Tatizo linalokuja ni kuwa hao viongozi wazee bado wanafikiri kuwa wana nafasi ya kushika madaraka makubwa ya nchi. Hivyo wanakuwa chanzo cha migogoro.
 
Ngagarupalu

Ngagarupalu

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
156
Points
0
Ngagarupalu

Ngagarupalu

Senior Member
Joined Oct 13, 2012
156 0
Mchambuzi,
kitu muhimu umenena, ili kufanya mchango effective jaribu uwe una post kwa chapter!! ni nzuri ila ndefu!! nikimaliza nitrejea
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Mchambuzi,
kitu muhimu umenena, ili kufanya mchango effective jaribu uwe una post kwa chapter!! ni nzuri ila ndefu!! nikimaliza nitrejea
Nashukuru kwa ushauri wako ngangarupalu;
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,495
Points
1,250
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,495 1,250
Hofu yangu ni kwamba CCM ni ileile hata baada ya ujio mwingine wa Mangula na upandaji cheo wa Kinana. Labda kama Kikwete naye angekubali kuondoka kwenye Uenyekiti akarudi Mkapa au mtu mwingine yeyote lakini asitokane na WANAMTANDAO wa mwaka 1995-2005. Hawa wanapaswa kuwa na CHAMA chao. Kwa kuwa bado wamo humu CCM, malengo yao bado hayajatimia, Mangula na Kinana hawataweza kuleta mabadiliko yoyote hata kama wangetaka sana mabadiliko yaje haraka.

WANAMTANDAO sio wanaCCM ya akina Mangula. Watafanyaje kazi nao? Bahati mbaya kabisa wana nguvu kubwa mno za kifedha ambazo ziliwaelemea mno akina Mangula mwaka 2005. Hali bado iko vilevile hadi sasa. Mbaya zaidi wamekuwa wengi na hawana uhakika na maisha na mali zao endapo CCM ya akina Mangula itashika hatamu za uongozi wa NCHI hii. Mzee Msekwa na Wilson Mukama wameondoka kimyakimya baada kushindwa kufanya mabadiliko yoyote ya maana mbali na kurudisha ujumbe wa NEC kugombewa wilayani, mabadiliko ambayo hayajaisaidia sana CCM na wameyafanya kinyume na KATIBA yao.

Sitarajii muujiza wowote toka kwa Mangula na Kinana.
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,005
Points
1,500
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,005 1,500
Hakuna chochote cha maana ambacho Mangulla na Kinana wanaweza kufanya ili kuinusuru CCM isianguke 2015, nafikiri ni bora wakafanya haya:
1/Kuiandaa CCM kukabidhi madaraka kwa CHADEMA kwa amani.

2/Kuaindaa CCM kuja kuwa chama cha upinzani imara.
Naungana na ww maaana nikiangalia kwa mfano kinana mfano yupo bussy sana na mipango yake bifasi kama kuendeleza kampuni yake ya Sharaf Shipping Company na mambo ya kifamilia kwa hiyo kufanya hayo uliyopendekeza bado itakuwa taabu kidogo maana yeye anajiangalia kwanza mwenyewe pili kuhusu kukubali kuiachia cdm nchi hapo 2015 pia pana shida maana kwa ufisadi ambao wanaccm wamehuusika watakataa ili wasije kuumbuliwa na chama ambacho kitachukua nchi so kwa hapo lazma usalama wa taifa walazimishe kuikabidhi nchi kwa chama kingine na hapo mangula na kinana itabidi wafanye kazi ya ziada kuanzia kumteua atakaye peperusha bendera ya CCM
maana kuna wagombea wengine watakuwa kinganganizi hata akishindwa atataka kutangazwa yy
 
Bramo

Bramo

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2009
Messages
10,341
Points
2,000
Bramo

Bramo

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2009
10,341 2,000
Mkuu Mchambuzi , unge edit Kichwa cha Habari na kuwa " Mangula, Kinana Na Hatima ya CCM"

Hii Inge make sense Zaid
 
Last edited by a moderator:

Forum statistics

Threads 1,296,582
Members 498,672
Posts 31,252,965
Top