Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,330
Sikubaliani na hoja kuwa Kinana na Mungula wanaweza kuwa chanzo cha aina yoyote ile cha Mustakabali wa Taifa letu, Pili sikubaliani na hoja kuwa Mukama alishindwa kuisimamamia na kuiongoza CCM,
Tatizo kubwa la CCM ni Mwenyekiti wa Chama, Mwenyekiti anaonekana kushindwa kukiongoza Chama, kwa hiyo uwepo wa Kinana na Mangula hautaweza kubadilisha chochote kwenye Chama kama Mwenyekiti atashindwa kusimama kama Mwenyekiti wa kutekeleza ushauri atakao pewa na hao (Kinana na Mangula).
Lowassa, Membe, Mwakyembe, Sitta na watu wanaofanana na hao ndio tatizo kubwa la chama kwa sasa, na hao hawagusiki kwa sababu Mwenyekiti hana uwezo wa kuwafanya chochote, Nape alijaribu kupambana na Lowasa lakini matokeo yake kila mtu anayaona, na Mangula na Kinana pia hawataweza kufanya lolote kwani Mwenyekiti hataweza kufanya maamuzi magumu yatakayoshauriwa na Mangula na Kinana
Mwenyekiti wa Chama na familia yake, tayari wameshakigawa chama kwa kuonyesha wazi kuwa wanamsupport Membe, sasa hapa Kinana na Mangula watakuwa na kazi gani ya kukijenga na kukirekebisha chama ili hali mtu wa kugombea 2015 ana baraka za mwenyekiti wa chama? na Hili si jambo geni kwa Kinana na Mangula, kwani hata Mangula mwenyewe ni muasisi wa hayo Makundi. Mangula ni miongoni mwa watu waliompinga JK kwa nguvu zake zote, kwa Mangula Sumaye ilikuwa bora kuliko JK, na kila mtu anajua kilichompata Mangula baada ya JK kuingia ikulu, kwa sasa sidhani kama Mangula atakuwa na uwezo tena wa kupingana na mwenyekiti kuhusu nani agombee 2015. Na hapa ndipo Mukama alionekana kana kwamba ameshindwa, Mukama aliangushwa na udhaifu wa Mwenyekiti.
Mimi naweza kukubaliana na wewe kuwa nchi inaweza kuyumba kama CCM ikitoka kwenye madaraka kwa sababu ifuatayo ambayo haiusiani kabisa na Kinana wala Mangula
Wakuu wengi wa vyombo vya usalama wanaisimamia CCM kwa minajili ya kulinda maslahi yao binafsi, ushahidi ulidhihirika wakati wa uchaguzi uliopita ambako tulishuhudia wakuu wa Usalama, Police, Jeshi wakitoa kauli tata ambazo zilituonyesha CCM inasimamia wapi. Kauli ya mwenyekiti wa CCM pale dodoma (CCM wasitegemee police) Pia inaonyesha ni kwa jinsi gani CCM ilikuwa ikitegemea wakuu wa vyombo vya dola.
Kama CCM itashindwa Kihalali na hao niliowataja hapo juu wakishirikiana na TBC na Msajili wa Vyama pamoja na NEC wakijaribu kufanya hila yoyote kwa ajili ya maslahi yao basi nchi itayumba na hapo itakuwa sio Kinana wala Mangula