MJINI CHAI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 2,198
- 1,226
Pole sana ndugu yangu naona una uchungu sana na thithiemu...
lakini ningependa kusikia zaidi upande wako wa hoja juu ya u-sumu wake katika mazingira ya sasa ya CCM na siasa za nchi kwa ujumla;
Kama Mangula na Kinana wakiiokoa CCM, hii itakuwa disaster kwa Tanzania. Kwa sasa ni muhimu sana CCM ife halafu izaliwe upya, ianze kwenda kwa baba na mama yake kuomba msamaha halafu iende tena mjini kutafuta kazi.
Mkulima na mfanyakazi ambaye ndio baba wa CCM sasa ametupwa kabisa, walau mtoto wa mfanyabiashara amejitokeza kujaribu kuwalea wazazi waliotelekezwa na mwanao. Kama CCM haiendi kuomba msamaha, laana itaendelea kuitafuna.
Unahoja nzuri lakini tatizo lake unataka CCM iendelee kukaa madarakani!!!
Sisi tumechoka na CCM tunataka itoke madarakani!!!
Pengine mawazo haya yatafaa kwa CCM wakiwa upinzani ili wayatumie kurudi madarakani!!
Sangarara,Mchambuzi.
Kuanzia kwenye Heading tu, ni nini kinakufanya uweke au ukose matumaini ya muenendo wa ccm kwa kuangalia watu hawa wadogo tu kwenye chama? chama hakina mwenyekiti? si ndie anayepaswa kuonyesha njia? sio issue ya kinana na mangula, bali ukweli ni kwamba makamu mwenyekiti yeyote yule na katibu wa chama yeyote yule hawawezi kumlazimisha mwenyekiti yeyote yule kufanya kitu chochote kile.
Leo ndio nimejua na mimi naipenda CCM, nilipofika hapo mahala umeelezea UNIP kupoteza kiti chake cha mwisho bungeni, mwili umenisisimka kwa kukiona kifo cha CCM mpaka machozi yamenitiririka, ila sina njia nyingine, sina budi kuliacha titi la mama.
Tukubaliane jambo moja: CCM inaumwa gonjwa ambalo halina tiba. Dawa za kurefusha maisha ya CCM bado zipo. Kila aliposhauriwa kuzitumia dawa hizi, Mwenyekiti Kikwete amekuwa akizitumia. Tumeona mabadiliko kadhaa kwenye Cabinet yake serikalini. Tumeona pia mabadiliko kwenye secretariet ya CCM. Mwenyekiti Kikwete ameweka rekodi ya kuwa na Makatibu wakuu watatu wa CCM, Makamba, Mukama na sasa Kinana ndani ya miaka hii sita ya Uenyekiti wake!
Tukumbuke pia jambo moja muhimu: Kikwete huyuhuyu alikuwa tayari kuiua CCM endapo ingemnyima kugombea URAIS wa JMT mwaka 2005! Sasa itafia mikononi mwake pamoja na tambo zake zote. Pamoja na akili nyingi alizonazo mtu kama Mangula amekubali kurudi kumsaidia mtu waliehitilafiana pakubwa kuimalizia CCM. Mangula naye amekubali kuwa dawa ya kurefusha maisha ya CCM. Historia itakuja kuliweka wazi hili.
Sangarara,
Nimejenga hoja kujibu maswali kama haya, na wapo baadhi ya watu wameuliza swali kama lako lakini waliporudi kusoma kwa umakini zaidi wakaelewa msingi wa hoja yangu ni nini; Vile vile wapo waliosoma na kunielewa na kuingia moja kwa moja katika mjadala wa kwanini uamuzi wa CCM baada ya 2015 aidha utaokoa au utaangamiza taifa letu; Ni katika muktadha huu ndio nimewajadili hawa wawili kwa hoja;
Tukubaliane jambo moja: CCM inaumwa gonjwa ambalo halina tiba. Dawa za kurefusha maisha ya CCM bado zipo. Kila aliposhauriwa kuzitumia dawa hizi, Mwenyekiti Kikwete amekuwa akizitumia. Tumeona mabadiliko kadhaa kwenye Cabinet yake serikalini. Tumeona pia mabadiliko kwenye secretariet ya CCM. Mwenyekiti Kikwete ameweka rekodi ya kuwa na Makatibu wakuu watatu wa CCM, Makamba, Mukama na sasa Kinana ndani ya miaka hii sita ya Uenyekiti wake!
Tukumbuke pia jambo moja muhimu: Kikwete huyuhuyu alikuwa tayari kuiua CCM endapo ingemnyima kugombea URAIS wa JMT mwaka 2005! Sasa itafia mikononi mwake pamoja na tambo zake zote. Pamoja na akili nyingi alizonazo mtu kama Mangula amekubali kurudi kumsaidia mtu waliehitilafiana pakubwa kuimalizia CCM. Mangula naye amekubali kuwa dawa ya kurefusha maisha ya CCM. Historia itakuja kuliweka wazi hili.
Hivi mabadiliko yanaweza kuletwa na watu wawili tu, tena wastaafu na wachafu katika chama kichafu, mfumo mchafu na wanachama wachafu?
Nikuulize jambo moja Mchambuzi: Kwa nini bado watu na akili zao timamu kabisa wanabanana kugombea nafasi za UONGOZI ndani ya CCM inayokufa kwa kasi hivi? Au hili linafanana na masuala ya ngono na ukimwi( nisamehe kwa lugha hii ya kuudhi)?Na ndio maana nimekuwa nasema kwamba kilichotokea ni mabadiliko ya Kichwa (na sio chote), huku shingo ikibakia kuwa ni ile ile; Na tunajua kwamba Shingo ndio hugeuza kichwa kulia kushoto, ku-nod ndio, hapana, yote haya ni kazi ya shingo na misuli yake na sio kichwa per se;
Nikuulize jambo moja Mchambuzi: Kwa nini bado watu na akili zao timamu kabisa wanabanana kugombea nafasi za UONGOZI ndani ya CCM inayokufa kwa kasi hivi? Au hili linafanana na masuala ya ngono na ukimwi( nisamehe kwa lugha hii ya kuudhi)?
Tukubaliane jambo moja: CCM inaumwa gonjwa ambalo halina tiba. Dawa za kurefusha maisha ya CCM bado zipo. Kila aliposhauriwa kuzitumia dawa hizi, Mwenyekiti Kikwete amekuwa akizitumia. Tumeona mabadiliko kadhaa kwenye Cabinet yake serikalini. Tumeona pia mabadiliko kwenye secretariet ya CCM. Mwenyekiti Kikwete ameweka rekodi ya kuwa na Makatibu wakuu watatu wa CCM, Makamba, Mukama na sasa Kinana ndani ya miaka hii sita ya Uenyekiti wake!
Tukumbuke pia jambo moja muhimu: Kikwete huyuhuyu alikuwa tayari kuiua CCM endapo ingemnyima kugombea URAIS wa JMT mwaka 2005! Sasa itafia mikononi mwake pamoja na tambo zake zote. Pamoja na akili nyingi alizonazo mtu kama Mangula amekubali kurudi kumsaidia mtu waliehitilafiana pakubwa kuimalizia CCM. Mangula naye amekubali kuwa dawa ya kurefusha maisha ya CCM. Historia itakuja kuliweka wazi hili.
kabadili kila kitu ila dunia yake haiendi vyema,sasa wote wabeadilishwa na mambo hayaendi ni wazi kuwa sasa yeye ndio tatizo.Mchambuzi
Hii mambo ya Jakaya kubadirisha watu kila siku sijui ni nani kamuambia ndio jibu, mambo yalianza kuharibika pale azimio la arusha lilipowekwa pembeni, hapo ndio milango ilifunguliwa na uchafu wa kila aina kuingia kila mahala ndani ya nyumba, badala ya ccm kufanya structural change imekuwa kama kipofu, blindly inabadirisha viongozi kila kukicha, tena this time anasema kapewa ushauri na mkapa, the same person aliyechukua nchi blindly akaanza kutekeleza sera za soko huria.