Mangariba 38 wakamatwa Moshi Tanzania

Afisaa mmoja wa serikali kaskazini mwa Tanzania ameambia BBC kuwa kikundi kikubwa cha watu waliokamatwa kwa kuhusika na ukeketaji wa wasichana mjini Moshi watafikishwa mahakamani Jumatano.

Kamishna wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,) amesema kuwa watu 38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa wasichana waliokuwa wanakeketwa.

Alisema kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.

Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata wanawake 38 mnamo siku ya Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.

Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.

Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida kutokea mjini Moshi.

Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.

Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.

Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.

Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.

Mangariba 38 matatani Moshi Tanzania - BBC Swahili - Habari
 
Ngariba maarufu huku JF Mr ZeMarcopolo hayupo Kati ya hao 38?
Ninaichukia sana hii mila,hivi wanawake kwanini hamshikamani ili kuhakikisha kuwa hii mila inatokomezwa kabisa,ukichukulia kwamba wengi wenu mmesoma sana na mna hold very reputable positions in the government.
 
Afisaa mmoja wa serikali kaskazini mwa Tanzania ameambia BBC kuwa kikundi kikubwa cha watu waliokamatwa kwa kuhusika na ukeketaji wa wasichana mjini Moshi watafikishwa mahakamani Jumatano.
Kamishna wa wilaya katika eneo la Kilimanjaro (Herman Kapufi,) amesema kuwa watu 38 waliokamatwa Jumatatu miongoni mwao ni wazazi wa wasichana waliokuwa wanakeketwa.
Alisema kuwa wasichana waliokeketwa wanapokea matibabu.
Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, waliwakamata wanawake 38 mnamo siku ya Jumatatu waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.
Haijulikani idadi ya wasichana walioathirika. Lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.
Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida kutokea mjini Moshi.
Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.

Mangariba 38 matatani Moshi Tanzania - BBC Swahili - Habari
Umaanisha hawa dada zetu wakichanga ni wahanga??hivyo ukiwaona tu count zero??
 
hahahahaha
kakakiiza,mie huko sipo,sijawahi kutest kwao kama wanatoa ama la,ila nimeleta post ili tuelewe nini kinaendelea toka kwao na kumfanya mwanamume kujiandaa na lolote lile,kwani ukiambia uendelee huku yeye anasoma gazeti usishangae,madhara yake ndio hayo-MANGALIBA
 
Back
Top Bottom