Mangariba 38 wakamatwa Moshi Tanzania

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,467
2,000
Maafisa wakuu mjini Moshi Tanzania, wamewakamata wanawake 38 waliopatikana wakiwakeketa wasichana katika eneo hilo.
Haijulikani idadi ya wasichana waliokuwa wanakeketwa , lakini ripoti zinasema kuwa walikuwa kati ya umri wa miaka 3 na 16.

Ingawa ukeketaji ambao umeharamishwa huendelezwa katika sehemu nyingi za Mara na Dodoma nchini Tanzania , hilo sio jambo la kawaida mjini Moshi.
Inaarifiwa wanawake hao walikamatwa Jumapili walipokuwa wanacheza dansi ya kitamaduni wakiwazingira wasichana ambao ndio walikuwa wamekeketwa tu.
Baadhi ya wasichana inaarifiwa bado walikuwa wanavuja damu na wengine wakiwa wanauguza majeraha.
Ukeketaji umeharamishwa nchini Tanzania tangu mwaka 1998 ingawa bado unaendelezwa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.
Inakisiwa asilimia 15 ya wasichana pamoja na wanawake wamekeketwa nchini humo.

CHANZO:BBC/Swahili :Mangariba 38 wakamatwa Moshi Tanzania - BBC Swahili - Habari
 
kisinja

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
238
500

Acha kupotosha na hao BBC Wako. Mangariba wamekamatwa Same na sio Moshi mjini kama unavosema.
 
Vmark.

JF-Expert Member
Aug 2, 2011
1,353
0
Same/ Upareni huko ndo walikonaswa hao mangariba na sio Moshi mjini.
 
Uledi

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
583
500
BBC Swahili ni shirika linalopoteza credibility kwa kasi ya ajabu. Utoaji wao wa habari umekaa kiudaku udaku kama gazeti la Kiu. Aibu sana kwa kweli
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,579
2,000
 
bysange

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
4,429
2,000
Kaaazi kwelkweli sasa hapa maandali ya gemu bila hicho kionjo inakuwa je..jamaani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom