Maneno ya viongozi wa CHADEMA kukutana na Rais yanatia doa dhamira yao

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
SHINIKIZO LA CHADEMA KUKUTANA NA RAIS LINATIA MASHAKA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Baada ya Mhe Rais kula kiapo Cha kuliongoza Taifa hili, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Mzee Freeman Mbowe waliutangazia umma kuwa wamemwandika barua Rais ya kutaka kuonana naye.

CHADEMA hawakuweka wazi ni mambo gani hasa wanataka kwenda kuzungumza na Mhe Rais, pamoja na kwamba lugha waliyotumia walisema tunataka kuliponya Taifa.

Sina uhakika sana kama Taifa lilikuwa linaugua na kuhitaji uponyaji. Nadhalia ya kuponya inatokana na mtu kuugua na kuhitaji kupewa tiba ili kumaliza ugonjwa huo.

Lakini katika mwendelezo wa ziara za kisiasa anazoendelea nazo Mzee Mbowe na wenzake bado amekuwa anatoa kauli ya kuwa walitaka kukutana na Mhe Rais na hajawapa nafasi. Mbaya zaidi sasa Mzee Mbowe na wenzake wametoka kwenye msingi wa kuwa walimuomba Mhe Rais kuonana naye, bali wamekuwa wakitishia kuwa mwisho wa siku wasije wakalaumiwa.

Sijajua wanamzungumzia nani kuwa atawalaumu na kwa kitu kipi? Ni kitu gani ambacho kipo na wanacho ambacho Rais asipowasikiliza kwa ratiba yake kinaweza kutokea na CHADEMA wakaanza kulaumiwa?

Tuelewane vizuri. Rais ni taasisi yenye jukumu kubwa la kuiongoza nchi yenye idadi ya Watu inayokadiliwa milioni 60. Kwa msingi huo Rais hafanyi kazi kwa mashinikizo ya kundi lolote bali kwa mjibu wa ratiba iliyopo.

Kwa nini hawa CHADEMA wanataka kumshinikiza Rais kuwasikiliza wao wakati ratiba yake bado haijawafikia? Haya mambo wanayotaka kuongea na Rais ni mambo ya dharura? Kama si mambo ya dharura kuna uharaka gani wa kuwa lazima tusikilizwe na tusiposikilizwa asije akatulaumu mtu? Lini wameshawahi kulaumiwa?

Siasa ni agenda na mipango. Lazima vyama vyetu hivi vijifunze kuwa na agenda ya kuwapata wanachama wao na si kutumia njia ambazo ni zilipendwa.

Rais anao washauri wake hasa ukizingatia Urais ni taasisi, huwezi kumpangia siku ya kukusikiliza. Anajua mambo ya dharura yenye masilahi kwa nchi na mambo ya kuchonga yenye masilahi kwa watu binafsi hasa ukizingatia kuwa toka mwaka jana walisema hawamtambui Rais.

Rais hana hata siku 100 Ofisini. Bado hata Ofisi hajasoma mafaili yote, lakini tunamlazimisha tumuone na mara wanasema hatutaki chai. Je kuna wakati walishaenda Ikulu kutafuta chai? Kama hawajawahi kufanya hivyo neno kutaka chai msingi wake ni upi? Mazingira haya ya kuharakisha kuwa Rais awapangie ratiba ya kwenda Ikulu haraka na wasipo pangiwa wasilaumie yanatia mashaka juu ya uhalali wa ajenda zao za kwenda Ikulu. Ni lazima vyombo viendelee kuwachunguza kabla hawajaenda kumfikia Rais kwani kunaweza kuwa na jambo lingine nje na ajenda ambayo inafikiriwa. Hii inatokana na uharaka walio nao ambao hauna simile.

Tulimuandikia Barua Rais Samia Suluhu baada ya kuapishwa, Tukimuomba kukutana, mpaka leo yupo kimya, hatuwezi kupiga magoti kuomba huruma ya kukutana nae kwan hatuhitaji chai ya Ikulu, tunamuona anakutana na makundi mbalimbali anaona sisi hatuna umuhimu, ipo siku atatutafuta na Hatatupata.

- Freeman Mbowe.

Mimi ninataka kujua ni makundi yapi si mhimu ambayo labda Mzee Mbowe alitamani yasubirie kwanza kukutana na Rais hadi CHADEMA wakutane na Rais? Mimi ninadhani makundi yote ni na ndiyo maana Rais anaona lipi aanze nalo na lipi amalize nalo. Lakini kutumia amri, nguvu kuwa lazima sisi ndiyo tungeanza tunakuwa tunaikosea mamlaka adabu na kutaka kutengeneza makundi kuwa kuna kundi mhimu kuliko kundi jingine. Hapana!

Ifahamike kuwa toka mwanzo baada tu ya kiapo Mhe Rais alizungumza nia yake ya kutaka kukutana na makundi mbalimbali yatakayomsaidia kupata maoni ya namna ya yeye kutatua kero zao. Na kwa msistizo alisema Watanzania tusahau yaliyopita kama Taifa tuanze upya. Hata nia yake imekuwa wazi kwani tangu wakati huo tumemuona akipambana kutatua changamoto na kupanga safu ya wasaidizi watakao msaidia kutimiza malengo yake ya kulitumikia Taifa. Sasa kwa nini dhamira yake njema ambayo yeye ndiye muasisi tunataka tumpangie kufanya haraka kana kwamba ratiba zake tunazijua? Tuwe wapole.

Rai Samia Suluhu Hassan anaoneka kutaka kuondoa misigano hiyo, ndiyo maana hata Aprili 22, akitoa hotuba yake ya kwanza iliyotoa dira ya serikali yake ndani ya Bunge jinini Dodoma, alieleza azma yake ya kutaka kuonana na vyama vya kisiasa vyote.

Mwenyekiti wa Chadema Mzee Freeman Mbowe alieleza kuwa chama hicho kiliandika barua kutaka kuonana na Rais Samia lakini bado hawaoni nia hiyo ikitekelezeka, ijapo alikiri kuwa ombi lao lilipokelewa. Na alisema wao kama CHADEMA wanataka kumuona Rais na si mazungumzo ya kuhusisha vyama vyote vya kisiasa.

Kwa historia ya nchi yetu tangu kuasisiwa kwa mfumo wa vyama vingi ni jambo la kawaida kwa anayekuwa kiongozi wa nchi kukutana na viongozi wengine wa vyama vya siasa. Ijapo wakati Mwingine kunakuwa na usiri juu ya yale yanayozungumzwa lakini ukweli huwa wanakutana na si kwa kushinikiza. Kiongozi wa Kitaifa anapopata nafasi huwa ndiye anawaita na kuwaomba kuzungumza nao. Hayati Mkapa alifanya hivyo hata Mhe Dkt Kikwete alifanya hivyo mara kadhaa.

Baada ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad, Rais wa Tanzania wa wakati huo, hayati John Magufuli alikiri kupokea barua tatu kutoka kwa Maalim baada ya mkwamo wa Uchaguzi wa 2015 uliotokana na kufutwa kwa uchaguzi Mkuu huo huko visiwani Zanzibar.

Lakini hadi Machi 2020, miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020, Watanzania ndipo waliposhuhudia viongozi hao wakikutana kwa kikao cha faragha kwa Maalim kualikwa na Magufuli katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.

Msururu wa vikao vya Magufuli ni ukweli kuwa haukushirikisha viongozi wengine wa vyama vya Upinzani hasa Chama Kikuu Cha Upinzani kwa wakati huo CHADEMA. Lakini Rais Samia ameweka wazi kukutana na vyama vyote vya kisiasa. Hii ina maana vyama vilivyo hai vitapata wasaa wa kuzungumza naye na kutoa dukuduku zao. Lakini CHADEMA kushinikiza kutaka kumuona haraka na pekee yao kunatia mashaka juu ya dhamira wanayosema kuliponya Taifa. Taifa haliwezi kuponywa na kikundi cha watu, bali uwakilishi wa makundi yote yenye dhamira ya dhati.

Kama kweli CHADEMA wana nia ya kuliponya Taifa kama wanavyosema, basi ninadhani wahenga wanasema "Subira yavuta heri" na haraka haraka haina baraka. Hata hivyo mwisho wa siku jambo la kusema tusije tukawalaimu halileti picha nzuri ukizingatia wao hawakai mbinguni na wote tunaishi Duniani hususani Tanzania. Jambo lolote zuri au baya lonatuhusu wote. Hivyo tusiombe baya lolote litokee ili tuwalaimu CHADEMA, baya lolote likitokea kwa mkutadha wanaosema halitachagua vyama, bali litachagua nchi ambayo hata CHADEMA wako humo. Tuhubirie amani, tusihubirie visasi na laana.
 
CHADEMA ni tatizo Mnyika amenukuliwa na gazeti la mwananchi akitaka kodi mpya kwa ajili ya katiba, anasema wananchi wako tayari kutozwa kodi ili kugharamia mchakato wa katiba.

Sijui aliongea na wananchi gani hadi wakamwambia kuwa wako tayari kukatwa kodi, wote tunakumbuka wakati wa bunge la katiba wajumbe walipokuwa wakilipwa posho ya laki tatu kwa siku ambayo wengine walisema haitoshi lakini kwanza rasimu na maoni ya wananchi yalibadilishwa lakini pamoja na kutumia pesa zote lakini bado katiba haikupatikana.

Ni vyema viongozi kama Mnyika wakitoa maoni wajitafakari kwanza kabla ya kusema.
 
Back
Top Bottom