Maneno ya Mwalimu Nyerere juu ya Udikteta

Maneno ya Mwalimu Nyerere juu ya Udikteta

JK NYERERE!
Huyu ni moja ya viongozi walio katika kundi la wanafalsafa,huwa na sifa kuu mbili
1.Wana uwezo wa kuongoza.
2.Hawapendi Uongozi.
Lakini Bwana Plato alidai hawa ni bora waongoze maana huwa hawang'ang'anii madaraka/kuwanyanyasa wana wa Nchi.

Lakini kwa Afrika hii na Tanzania hii hawa watu sidhani kama wanapatikana.
 
Mpaka awamu yake iishe tutakuwa tumekoma maana dalili za unkurunzinza zimeshaonekana kupitia lichama lake. Eee Mungu tunaomba utuepuashe na mikono ya watu wa aina hiii. naamini huyu jamaa hawezi kukubali katiba ya Warioba ipite maana itampunguzia mamlaka. Yeye anapenda kuitwa"My Lord", Rabi, na majina ya aina hii yenye kutukuza. yaani anatamani kila anapopita abebwe, ashangiliwe na atukuzwe hata kama watu wako kwenye hali mbaya kimaisha
 
Angekuwepo leo mngekuwa bize kumuandama na kumpinga enyi wanafiki..
 
Angekuwepo leo mngekuwa bize kumuandama na kumpinga enyi wanafiki..

Dah.....unawaza kama mimi....waswahili ni wanafiki sana......Huyu babu leo angekuwa hai watu kama akina Bashite wangekuwa wanamtukana au ngumi kama kawa
 
Mwl. Nyerere hakuona udikteta wake lakini alikuwa mzuri kuona udikteta wa watu wengine.

Nchi alikuta ina vyama vingi lakini akafuta na alipoondoka akashinikiza vianzishwe.

Wakati wa utawala wake, Mtu unaenda kupiga kura unapewa fursa ya kuchagua sura ya Mwl. Nyerere au kibox kilichowazi ambacho kimewekewa alama ya kosa au hapana.

Alikuwa kila akitembelea maeneo fulani ilikuwa tunalazimishwa tufunge biashara zetu ili tuende kumsikiliza na kama ukikataa mali zako zinachukuliwa na unatupwa gerezani.

Waliokuwa wanajaribu kumpinga walijikuta wakitupwa magerezani au iliwabidi waikimbie nchi na kuwa wakimbizi.

Pamoja na udikteta wake lakini ni kiongozi pekee ambaye anapendwa na kuheshimiwa na wengi nchini Tanzania.

Ninawashangaa wanaopiga kelele kupinga udikteta halafu kwa ujinga wao wanatumia mifano ya Mwl. Nyerere ambaye alikuwa dikteta kiasi kwamba alitaka kupinduliwa zaidi ya mara tatu.

Kwa maana nyingine, udikteta sio hoja nchini na kama ingekuwa ni hoja basi Mwl. Nyerere asingekuwa anaheshimika na kupendwa na wengi nchini.
 
pic+lissu.jpg


Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu

Kwa ufupi
  • Kauli hiyo ya Lissu imekuja siku moja baada ya juzi, Rais Magufuli kusema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakishinikiza Serikali kuwaondoa gerezani watu wanaoshikiliwa na polisi na akawaonya wanaofanya hivyo kufunga midomo.
By Raymond Kaminyoge, Mwananchi rkaminyoge@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesema kitendo cha Rais John Magufuli kuwataka wafunge midomo ni kuminya haki ya watu kutoa maoni yao.

Kauli hiyo ya Lissu imekuja siku moja baada ya juzi, Rais Magufuli kusema baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakishinikiza Serikali kuwaondoa gerezani watu wanaoshikiliwa na polisi na akawaonya wanaofanya hivyo kufunga midomo.

Hivi karibuni, waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikaririwa akitaka kuachiwa huru kwa masheikh wa taasisi ya Uamsho akisema wamekaa ndani kwa muda mrefu bila kuhukumiwa.

Kauli hiyo ilisababisha Lowassa aitwe Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa mahojiano ili chombo hicho cha dola kione kama maneno yake yana mwelekeo wa uchochezi au la.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu kauli ya Rais Magufuli, Lissu alisema wananchi wana haki ya kuhoji viongozi hao wa dini wanaoendelea kukaa mahabusu bila kuhukumiwa.

Alisema wanasiasa watamkosoa Rais kama ataminya uhuru wao wa kutoa maoni bila kuvunja sheria.

Aliungwa mkono na Anna Henga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), aliyesema kisheria hakuna kosa kuhoji ikiwa mtu anakaa muda mrefu mahabusu bila kuhukumiwa.

“Si kosa kwa wananchi kuhoji kama wanaona ndugu au jamaa zao wamekaa mahabusu bila kuhukumiwa, ni wajibu wao kuhoji,” alisema Henga ambaye pia ni mwanasheria.

Alisema wananchi wana haki ya kuuliza kwenye mamlaka husika kuhusu mienendo ya kesi zinazowahusu ndugu na jamaa zao.

“Kwa hiyo wanatakiwa kuelewa sababu zinazochelewesha kutolewa kwa hukumu za ndugu ama jamaa zao, hii ni haki yao,” alisema.

Alisema hata wanasiasa wanaozungumzia kuhusu watu walioko mahabusu wana haki ya kufanya hivyo.
 
Ukiona kiongozi wa nchi aliyeingia madarakani kwa kura anageuka kuwa dikteta uchwara ndani ya mwaka mmoja tangu kuingia kwake madarakani basi hesabu huyo atakuwa terrifying dictator kadri muda unavyoenda!!

Madikteta yote duniani yana sifa moja inayofanana! Hawa wanadhani ni wao ndio wenye uchungu na nchi kuliko wengine! Wataongea majukwaani kwa lugha za kujionesha wao ni wazalendo kweli kweli!

Watatenda yale ambayo average person wataona yanafanywa kwa ajili yao kumbe lengo la madikteta ni kuwa na population kubwa nyuma yao iliyojaa mazuzu kwa sababu, kwa asili, mazuzu huwa hawahoji kwa vile Mungu amewanyima uwezo wa kuweza kuangalia mambo kwa jicho la tatu!!

Na kwavile hawana uwezo wa kuhoji, wao watabaki wakishangilia tu kwa kila kitu!!

Hakuna dikteta hata mmoja duniani anayetaka watu wahoji kile anachofanya au kutenda!! Hawa wanataka kauli zao ziwe kama kauli za mitume!! Ukiwa mtu wa kuhoji hoji wewe utakuwa kwenye top list ya maadui wa madikteta duniani kote!! Na kwa madikteta na makuwadi wao, dhima ya kuhoji wanaibadilisha na kuiita KUPINGA!!


Kwa bahati mbaya kabisa, popote utakapoenda duniani, mazuzu kwa viwango vya eneo husika ni wengi kuliko werevu!!!

Hawa mazuzu ndio mtaji wa madikteta duniani kote! Na kwavile madikteta yanafahamu kabisa kwamba population inayowaunga mkono ni Mazuzu Republic, basi mara zote watafanya mambo ya kuwaonesha mazuzu kwamba wao ni "The Chosen!"

Na kwavile ni mazuzu, yatasimama na kushangilia "Wewe ndie mwokozi wetu na tupo tayari kufa kwa ajili yako!!" Na kweli yatakuwa tayari kufa kwa sababu, ni mazuzu tu!!!
 
Mwl. Nyerere hakuona udikteta wake lakini alikuwa mzuri kuona udikteta wa watu wengine.

Nchi alikuta ina vyama vingi lakini akafuta na alipoondoka akashinikiza vianzishwe.

Wakati wa utawala wake, Mtu unaenda kupiga kura unapewa fursa ya kuchagua sura ya Mwl. Nyerere au kibox kilichowazi ambacho kimewekewa alama ya kosa au hapana.

Alikuwa kila akitembelea maeneo fulani ilikuwa tunalazimishwa tufunge biashara zetu ili tuende kumsikiliza na kama ukikataa mali zako zinachukuliwa na unatupwa gerezani.

Waliokuwa wanajaribu kumpinga walijikuta wakitupwa magerezani au iliwabidi waikimbie nchi na kuwa wakimbizi.

Pamoja na udikteta wake lakini ni kiongozi pekee ambaye liked and admired by many na mpaka sasa anayeheshimika sana nchini Tanzania.
Anaheshimika kwa darasa la saba, form 4 failures na mbumbumbu wa vijijini! Mtu anayejitambua hawezi kumsifia Nyerere kwa kiwango hicho! Halafu eti wakatoliki wanataka awe mtakatifu! Rubbish!
 
Kwa haya yanayoendelea hapa, a good number ya watanzania ni mazuzu... ukiondoa wafuasi wa Ukawa. Wachache wa CCM wanajua ukweli lakini njaa inawasumbua.
 
"Katiba hii imenipa madaraka makubwa sana, ipo siku atakuja mtu ataitumia atakavyo na atakuwa kama Mungu."

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
23 Februari 1982.

Katiba imempa madaraka makubwa lakini aliona sawa tu, hakuibadilisha!

Sasa yeye katoka, anatuambia sisi tufanye nini, yeye kashindwa!

Yale aliyokuwa anayataka yaingie kwenye katiba alikuwa anampa makaratasi Kawawa avuke barabara ayapeleke pale Karimjee Hall kumpa Msekwa na Mkwawa, wanayapitisha yanakuwa Katiba, yanakuwa sheria.

Mbona hili la kupunguza nguvu za Rais hakuligusa? Halafu tunamuita Baba wa Taifa. Yani alikuwa anatuona wajingaaaaaa!
 
Nyerere hakuwa malaika na alifanya makosa mengi tu na hata yeye mwenyewe alikiri hivyo. Na kama si yeye ile Tume iliyotembea nchi nzima kukusanya maoni kuhusu mfumo wa vyama vingi nchini ingeandika kwamba Watanzania wamekataa mfumo wa vyama vingi hivyo si ajabu hadi hii leo tungekuwa bado tuna mfumo wa chama kimoja.

Pamoja na mapungufu yake kama kiongozi kama binadamu lakini bado ana sifa nyingi za mazuri mengi aliyoyafanya nchini ambayo yanastahili kumpa heshima ya Baba wa Taifa ukilinganisha na wote waliokuja baada yake ambao walikuwa wezi, waliojilimbikizia mali kwa njia za haramu na mengine mengi mabaya dhidi ya nchi yetu ikiwemo mikataba mbali mbali ya kifisadi.

Katiba imempa madaraka makubwa lakini aliona sawa tu, hakuibadilisha!

Sasa yeye katoka, anatuambia sisi tufanye nini, yeye kashindwa!

Yale aliyokuwa anayataka yaingie kwenye katiba alikuwa anampa makaratasi Kawawa avuke barabara ayapeleke pale Karimjee Hall kumpa Msekwa na Mkwawa, wanayapitisha yanakuwa Katiba, yanakuwa sheria.

Mbona hili la kupunguza nguvu za Rais hakuligusa? Halafu tunamuita Baba wa Taifa. Yani alikuwa anatuona wajingaaaaaa!
 
Back
Top Bottom