It is very true.
Kwa hotuba aliyotoa Mwalimu Nyerere mwaka 1995, ingetokea leo angekuwa hai, angesupport harakati za Ukuta kwa asilimia 100.
Kwa kuwa katika hotuba hiyo ya mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alieleza wazi kuwa tunachagua Rais ili aweze kuitii na kuilinda Katiba kama alivyoapa wakati anakabidhiwa madaraka hayo kuwa ataitii Katiba na kuiheshimu.
Mwalimu aliendelea kueleza kuwa iwapo watanzania watachagua Rais ambaye hataitii na kuilinda Katiba aliongea bila kumung'unya maneno kuwa Rais wa aina hiyo HATUFAI........
Kitendo cha Mkuu wa nchi kupiga marufuku shughuli zozote za kisiasa hadi mwaka 2020 na wakati huo huo kuruhusu chama chake cha CCM kufanya shughuli za kisiasa bila 'kuguswa' na Polisi, ni dhahiri ni kuisigina Katiba ya nchi.
Inashangaza mno kwa wanaccm ambao siku zote husimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kujinadi kuwa watamuenzi Mwalimu kwa vitendo, lakini kwa wosia huo muhimu sana kwa Taifa letu, wameamua kuupiga teke!