Maneno ya kejeli ya mume wangu

Maneno ya kejeli ya mume wangu

Huu wito wa ndoa umekuwa mgumu sana, walio single sasa wataogopa kuingia kwenye ndoa kwa style hii. Pole sana dada, jaribu pia kumshirikisha Mungu, yeye aliyekuumba anajua solution ya matatizo yako
 
36, no kids, unafanya kazi, ila bado unasubiri akuletee mke mwenzio ndani ndio uondoke sio? au ngoma kabisa.

36 bado marketable bana, ama?

Sasa nimeanza kupata picha kamili ya uwezo wako wakufikiri na kung'amua ni mfinyu mnoo..hustahili kupitia katika haya majukwaa au kwenye thread kama hizi na kuacha ushauri
 
Ingekuwa tukio la mara moja, ningekushauri ushirikishe wazazi ila kwa jinsi ulivyoelezea na kama ni kweli, hama hapo haraka utafute ustaarabu wako.
Omba kabisa talaka muachane, huyo hakupendi na hakutaki kabisa na sijui kwanini hakupi talaka? Au anakutegemea? Achana na huyo mbwa, tafuta life yako, wewe bado binti mdogo, hutakosa wa kukuoa na swala la watoto lisikuumize kichwa, utajua la kufanya baada ya kutoka hapo.

Tena usije ukasikiliza ushauri wa eti mkalishwe chini msuluhishwe, hiyo ni kitu mbaya sana, huwezi ukakubali kuishi na mtu aliekubali kukuheshimu baada ya kusuluhishwa na ndugu, hutakaa kwa amani kwa sababu atakuwa na masimango yasiyoisha kama anavyotumia kauli kuwa alikuoa kwa huruma. Achana na huyo mpuuzi. Medical solutions za tatizo lako zipo? Madaktari wanasemaje? Angalia mbele, achana na jitu jinga hilo.
 
Naungana na hao wote walio kushauri uwemvumilivu na mstahimilizvu katika ndoa yako,hasa katika maombi naamini Mungu huwa hachelewi kujibu..Nakusihi usiache ndoa yako ipiganie na utashinda..!!!issue sio mtoto au wewe kuto kuzaa ila issue kubwa ni mumeo hajajikubali kuwa mume na kuukubali uanaume wake..Utashinda very soon
 
Pole sn unaishi ktk mazingira magum sn lkn endeleea kumwamini Mungu nabkumwombea sn huyo mumeo
 
  • Thanks
Reactions: JGV
Pengine tunatofautiana mtazamo lakini ndoa ikikosa amani ni shida kama sio balaa. Ukivaa nguo unaona haipendezi, ukila chakula "hakipandi" taratibu ufanisi na tija katika kazi na hata biashara unashuka. Dada yangu jamii na Taifa linakuhitaji nakukumbusha msemo wa wahenga "la kuvunda halina ubani". Miaka 36 kwangu mimi bado ni umri mzuri waweza kuondoka na ukaanza maisha yako na Isha-Allah utafanikiwa. Ni ngumu kuwa na furaha hasa ukizingatia unaeishi nae anaamini anaishi na wewe kwa "hisani". Dada songa umri wako ni sawa na binti wa darasa la sita.
 
pole sana dada, jaribu kushirikisha familia kwa mara nyingine. Ikishindikana, chukua maamuzi magumu. Kwani Anaweza kukulete magonjwa ya aibu na yasiyotibika.
 
Simpendi mwanandoa anaye mnyasanyasa mwanandoa mwenzake nikiziona hizi posti nashikwa na hasira sana. Huyo mwanaume hana mapenzi ya kweli kwako wewe na ameshakutamkia lililoko moyoni mwake nawe huna budi kulipokea ingawa linauma. Yeye alichokuwa anakitaka ni watoto na wewe umeshindwa kumpatia hao watoto, hakuna namna nyingine zaidi ya kumuachia nyumba yake amlete atayemzalia mtoto. Mwanaume uliyenaye ni mwanaume katili sana hata ukipatwa na tatizo kumbuka hatakusaidia na hii ukute inachagizwa na upande wa wazazi wake. Ukiona mahali hutakiwi huna budi kuondoka husilazimishe kupendwa, naamini utapata furaha hata kama utatoka kwenye hiyo ndoa usiwe na hofu ya kuchekwa na jamii simama kama wewe na huyo mwanaume atakuja kuregret baadae na usimpe tena nafasi ndani ya moyo wako
 
Ingekuwa tukio la mara moja, ningekushauri ushirikishe wazazi ila kwa jinsi ulivyoelezea na kama ni kweli, hama hapo haraka utafute ustaarabu wako.
Omba kabisa talaka muachane, huyo hakupendi na hakutaki kabisa na sijui kwanini hakupi talaka? Au anakutegemea? Achana na huyo mbwa, tafuta life yako, wewe bado binti mdogo, hutakosa wa kukuoa na swala la watoto lisikuumize kichwa, utajua la kufanya baada ya kutoka hapo.
Tena usije ukasikiliza ushauri wa eti mkalishwe chini msuluhishwe, hiyo ni kitu mbaya sana, huwezi ukakubali kuishi na mtu aliekubali kukuheshimu baada ya kusuluhishwa na ndugu, hutakaa kwa amani kwa sababu atakuwa na masimango yasiyoisha kama anavyotumia kauli kuwa alikuoa kwa huruma. Achana na huyo mpuuzi. Medical solutions za tatizo lako zipo? Madaktari wanasemaje? Angalia mbele, achana na jitu jinga hilo.

Asante kwa ushauri, ninatibiwa kwa specialist , daktari anasema hili tatizo linatibika na ninaendelea kutumia dawa za hospital, ila na yeye anatakiwa atumia dawa na vyakula vya kuongeza sperm. Ila kwa stress hizi ni ngumu kupata mtoto na tendo lenyewe la ndoa ni mara chache mtoto atapatikana vipi.
 
Kuna vitu vya kumuomba Mungu. Hili la huyu Nacherewa Mungu alishalijibu zamani kwani ameweza kumuonyesha tabia kamili ya mume wake na lililobaki hapo ni kuchukuwa hatua. Tunatakiwa kuwa na maarifa Mungu ametupa akili... hakuna sababu ya kung'ang'ana na mume mzinzi. Wanawake wengi wamekuwa wanyonge kwa kunyanyasika na kuendelea kuvumilia mateso hata pale penye uwezo wa kutoka na kuishi kwa furaha na ndio maana makanisa yanajaa wanawake wanaolia kila siku kwa mambo ambayo hawakupaswa kuyalilia na matokeo yake huambulia kufa kwa magonjwa ya kuambukizwa na hao wanaume waliokuwa wakiwalilia usiku kucha. Wengine huwa wanafikia hatua ya kuwaombea hao wanaume wafe ili wawaache wajane! Wanawake zindukeniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii looool

yaani ukitakata kujua kwa nini wanawake wamejaa makanisani soma Zaburi 3:14-16, ni mwanamke kutambui adui yake ni nani.. yani inshort unamuambia indirectly aende for divorce, hata katika sheria ya nchi resort ya kwanza sio petition ya divorce lazima kuwe na usuluhishi..all in all, mtu atafanya atakalo, haya Mungu kamuonyesha tabia ya mume wake, the next move is hers, either stand in prayers or get a divorce, zote ni solution na zote zina majibu yake
 
Ndoa ya kikristo haivunjiki bali kwa uasherati, sasa sijajua unang'ang'ania nini hapo dada
 
@faiza foxy huwa hana tatizo la lugha. Ingekuwa huyu mtu amejiita #nachelewa badala ya Nacherewa, ningekuunga mkono!
Unamaanisha nini? wengine sio waandishi wazuri wa kiswahili kwa hiyo uniwie radhi kama lugha ni mbovu.
 
Asante kwa ushauri, ninatibiwa kwa specialist , daktari anasema hili tatizo linatibika na ninaendelea kutumia dawa za hospital, ila na yeye anatakiwa atumia dawa na vyakula vya kuongeza sperm. Ila kwa stress hizi ni ngumu kupata mtoto na tendo lenyewe la ndoa ni mara chache mtoto atapatikana vipi.

Kama linatibika, usiwe na presha, ondoka utapata atakaekuthamini uzae nae mtoto, huyu msahau. Usidhani kelele hizo ni kwa sababu huna mtoto, utanielewa utakapozaa nae halafu akupatie break ya miezi miwili ya labour akionekana kachange halafu baada ya hapo arudi kwenye mstari kama mwanzoni. Hutatamani life!
 
yaani ukitakata kujua kwa nini wanawake wamejaa makanisani soma Zaburi 3:14-16, ni mwanamke kutambui adui yake ni nani.. yani inshort unamuambia indirectly aende for divorce, hata katika sheria ya nchi resort ya kwanza sio petition ya divorce lazima kuwe na usuluhishi..all in all, mtu atafanya atakalo, haya Mungu kamuonyesha tabia ya mume wake, the next move is hers, either stand in prayers or get a divorce, zote ni solution na zote zina majibu yake

Kwa hiyo hapo aombeee nini? Mume aanze kumpenda na kumthamini na kuacha kumtukana?
au Aombe mume akibeba gonjwa huko lisimkute? Au alie tuuuuu na kuomboleza kwa kuwa kamtambua adui yake hivyo adui ageuke rafiki? Mbegu za mume ziimarike naye apone azae?

Kuna vitu vya kulia, kufunga na kuomba sio hivyo!

Linapokuja suala la ndoa.... mengi huchunguzwa toka mwanzo. Inaonekana dhahiri huyu hakuwa kusudio la Mungu kwake na ndio maana wanatofautiana kiasi hicho. Huyu hakuwa ubavu wake.... kuna mistake za uchaguzi zilikuwepo hapo hakuna cha kuzirekebisha. na ndio maana Mungu hajawapa mtoto ambaye kwa namna moja angekuwa kwazo.... aondoke hapo!

Hakuna Zaburi 3:14-16
 
  • Thanks
Reactions: naa
Kama utapata Muda soma kitabu kinachoitwa "BIKIRA YANGU" mwandishi ni Privatus Karugendo. Kingine ni UMEVAA MIWANI GANI & MAJI YAKIMWAGIKA YANAZOLEKA mwandishi ni Faustin M. Kamugisha.
 
Ombeni nanyi mtapewe hata hivo bado hamjaomba bado, usivunjike moyo ulipo vumilia lazima pakuzalie matunda Mungu yu mwema kwako ndo maana umeweza vumilia wanaume wanapenda from 100 to zero afuu wanaanza kupanda chat tartibu atarudiii kwenye chat , wanawake wanaanza zero to 100, mvumilie atarudi kwenye mia huku ukimwambia arud na adabuuu, utamfurahia Munguuu nakwambia, ushajiuliza anazurula lkn anarudi nyumbani kwake hilo ni pepo litamwacha siku moja, HALELUYA
 
Kama utapata Muda soma kitabu kinachoitwa "BIKIRA YANGU" mwandishi ni Privatus Karugendo. Kingine ni UMEVAA MIWANI GANI & MAJI YAKIMWAGIKA YANAZOLEKA mwandishi ni Faustin M. Kamugisha.
Asante nitakitafuta
 
Back
Top Bottom