Maneno ya bibi baada ya kuisoma namba

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
"Mjukuu wangu,hivi toka juzi nashindia UJI!Japo ulinitumia ile 100000 wiki jana lkn haijasaidia kwa kukidhi haja.

Mjukuu wangu,debe la mahindi kwa sasa ni 22500 kusaga ni 2500.Pata picha!

Nimelima heka 5 mvua hazitoshi na azao yamekauka!Ktk ile laki moja ulonitumia elfu 75000 niliielekeza ktk kilimo cha makondeni.Ajabu huko nako holaa!

Nafanye nini sasa mjukuu wangu?!Bwana shamba nilimpigia simu zaidi ya mara 20 naye kuniahidi aja ni mara idadi fanani na hiyo-lkn hajapata kuonekana!Anaishi huko mjini,km yapata 78 kutoka kituo chake cha kazi!

M/kiti nilimpa taarifa kuhusu jambo hilo naye anasema hawezi kuhangaika na bwana shamba huku kwake kuna njaa pia.Na hata ile posho yake ya kila mwezi 20000 (sina hakika) eti hajaipata!Kumbuka debe la mahindi ni elfu 22500!

Mbunge toka achaguliwe haonekani jimboni!Simu hapokei pia.Leo ni miezi 2 hata tone la mvua halijatona!HATARI hapo!

Mjukuu wangu,hawa maafsa wa kilimo wanalipwa kwa kazi ipi hasa?!HAPA KAZI TU i-wapi maana yake?!Dharau na kiburi kwa tuliowachagua kutuwakilisha inatoka wapi?!

Ama kweli NAJUTA!Najutia hasa kile nilishauliwa nanyi wajukuu kwamba mabadiriko hayaepukiki tena!Nakumbuka niliwazodoa sana huku nikiimba kale ka wimbo ketu kapya ka-WATAISOMA KIRUMI!Natamani uchaguzi uwe leo."


Pole bibi yangu.LKN HATA WEWE?! Ndiyo hasa swali langu.Sikukutarajia km nawe utayatamani mabadiliko!Ama kweli halipo lefu likosalo ncha!

Vumilia bibi yangu leo tena nitauza yule ng'ombe mkubwa angalau nikutumie laki 2 ikupoze machungu.

VIPI KUHUSU BIBI ZETU WASIO KUWA NA MSAADA WA VIJANA WAO?!

Serikali,TIMIZENI wajibu wenu.
 
Pole bibi. Kuhusu mbunge wenu, alikuwa bize bungeni anataja mali za Makonda.
Nadhani bado anafuatilia mali zingine ataje kikao cha bunge kijacho
 
mwambie bibi aache kuandika kihuni pia kukosa mvua mwaka jana njaa haiwezi kuja kipindi hiki so aache uongo
 
Back
Top Bottom