Maneno na Kauli tunazoambizana tukiwa na hasira; zinafichua yaliyo moyoni!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Ukimnyoshea mtu mkono kumpiga unaweza ukaurudisha angani au kuukwepesha usimpige au usimpate. Hata hivyo ukilitoa neno ambalo hukulimaanisha na likampata mwenzio huwezi na hauna jinsi ya kulirudisha. Neno likishatoka limetoka hata ukijaribu kulifuta halifutiki bali huacha alama. Lakini wapo watu ambao husema maneno makali wakiwa na hasira maneno ambayo japo wanaweza kujaribu kuyapoza kwa mabusu, miguso na samahani nyingi. NImeyasikia mengi sana kwa mfano mtu katika hasira anaanza kumuita mwenzie:

"Mpumbavu wewe"
"mwanamme gani wewe"
"malaya Mkubwa"
"Kwani miye mtumishi wako"
"Acha mambo ya kijinga"

Je kuna maneno ambayo umewahi kusikia watu wakiyasema na ukajua si mazuri kuambiana hasa watu ambao mnadai kupendana? Je wajua madhara ya maneno yalivyo katika hisia na mioyo ya watu? Inakuwaje mtu mtukanane halafu mwende chumbani pamoja? Je unajua wakati mwingine mtu anaenda pembeni ya pendo lake ili akapate maneno ya utulivu na ya kutulizwa?

THINK ABOUT IT: IF YOU DON'T MEAN IT DON'T SAY IT!

n.k n.k
 
Ni kweli!

Lakini tukumbuke kuwa hasira mara nyingi huondoa upeo wa reasoning wa muhusika; sisemi kama ni kisingizio ila kuna mambo mengi waweza kutenda ukikasirika ukaja sghangaa baada ya hasira kuisha na wee kutuliza akili. l
 
Ulimi ni kiungo kidogo sana lakini madhara yake ni makubwa mno. Ni kama njiti ya kibiriti inavyoweza kuwasha moto mkubwa usiozimika au usukani wa meli unavyoweza kuigeuza meli iliyobeba mamilioni ya kilo za mizigo! Hivvyo ni vyema na inapendeza tujifunze jinsi ya kuwa na control na midomo yetu pale hasira inapokuja either kwa kukaa kimya or kwa kuondoka kwenye mazingira yaliyokusababishia hasira

Bila kufanya hivyo tutajikuta tukiwalaani watoto wetu na pengine hata sisi wenyewe kwa maneno ya kinywa chetu wenyewe. Unaweza kuprove madhara ya ulimi hata kwa taifa letu na nchi jirani kwa kukumbukia suala la sakata la walimu na umbayuwayu, Kaka mkuu na sakata la DJ, hivi juzi tu David Cameroun na ishu zake za misaada ya kishoga nk.

Tuwe makini.
 
ulimi ni kiungo kidogo sana lakini madhara yake ni makubwa mno. Ni kama njiti ya kibiriti inavyoweza kuwasha moto mkubwa usiozimika au usukani wa meli unavyoweza kuigeuza meli iliyobeba mamilioni ya kilo za mizigo! Hivvyo ni vyema na inapendeza tujifunze jinsi ya kuwa na control na midomo yetu pale hasira inapokuja either kwa kukaa kimya or kwa kuondoka kwenye mazingira yaliyokusababishia hasirabila kufanya hivyo tutajikuta tukiwalaani watoto wetu na pengine hata sisi wenyewe kwa maneno ya kinywa chetu wenyewe. Unaweza kuprove madhara ya ulimi hata kwa taifa letu na nchi jirani kwa kukumbukia suala la sakata la walimu na umbayuwayu, kaka mkuu na sakata la dj, hivi juzi tu david cameroun na ishu zake za misaada ya kishoga nk.tuwe makini.
niko nyuma yako,naunga mkono hoja!
 
ni kweli maneno yatokayo mtu anapokasirika yanaweza kuvunja sana, naamini mtu anapokasirika na maneno kumtoka yale maneno huwa anayamaanisha, yaani ndo anatoa mtazamo wake halisi alionao kwako, sasa akikuambia "malaya mkubwa we" ujue ohooooooo kumbe siku zote anakuchukulia hivyo.

kikubwa ni kudhibiti maneno yetu, heri hasira zikiwa juu kunywa maji hadi utulie, au hama kaa mbali na aliyekuudhi n.k kuepuka kubomoa
 
Tatizo ni kwamba watu wengi wakiwa kwenye kutoelewana maneno na matendo yao wanayaelekeza kenye kuwaumiza wenzao.
Ndo hapa kama mtu hana ukweli unaoweza kumuuliza mwenzake anachagua neno tu kama hayo hapo juu na kumtupia.Itakua vizuri kama watu watajitahidi kuendesha hasira zao pale inapobidi...ukiona kimekufika kooni chukua muda nenda sehemu..toka kimbia..lala..lia..vyote hivyo ukiwa mbali na mwenzako alafu zikishapungua ndo urudi kumcomfront, badala ya kutengeneza nyufa zisizozibika kwa tuwapendao.
 
Wakati wote .... Pinga au toa marekebisho bila hisia hasi za hasira, chuki na kadhalika!! ...Kwa namna yeote kama una fundo la hisia hizi.. airisha matamshi yako kwa unayemkusudia...kuarisha huko ndio Ujasiri,Ushindi na Upendo wa dhati!

Ni ushindi na upendo kwani umeamua kwa akili timamu kabisa kufanya hivyo!!
 
bahati mbaya ugomvi mwingine huzuka sehemu ambayo haikupi wasaa wa kutafakari; kwenye kadamnasi ya watu...........usiku wa manane!

Wakati wote .... Pinga au toa marekebisho bila hisia hasi za hasira, chuki na kadhalika!! ...Kwa namna yeote kama una fundo la hisia hizi.. airisha matamshi yako kwa unayemkusudia...kuarisha huko ndio Ujasiri,Ushindi na Upendo wa dhati!

Ni ushindi na upendo kwani umeamua kwa akili timamu kabisa kufanya hivyo!!

Nyote wa wawili mmenena mambo muhimu sana lakini tunahitaji kusaidia njia za haraka za kudhibiti hizi hasira
 
Miye nimewahi kusikia mtu anamsema mke wake na kumlinganisha na ex wake. "muone mwanamke gani hujui kuvaa, angalau x,y alikuwa anavaa vinavalika"..
 
....hata hivyo, ukiambiwa nawe ujiambie bana...

mimi mwalimu wangu ni kipofu na kiziwi!....
mfano; nikiambiwa "mwanaume gani wewe!," athari yake kwangu sio kubwa kiviiiile...

--najua ni maneno ya mkosaji tu hayo!
 
Very true mwanakijiji... and kibaya zaidi ni pale ambapo zao la kauli huwa ni watoto, kwa mfano maneno yahusuyo uhalali wa mtoto, uaminifu na personal ability to do something

Looking at the picture below (though it is just a visual), unaweza ukatabiri life ya huyo mtoto na familia kwa ujumla wake
family issue.jpg
 
Ni kweli!

Lakini tukumbuke kuwa hasira mara nyingi huondoa upeo wa reasoning wa muhusika; sisemi kama ni kisingizio ila kuna mambo mengi waweza kutenda ukikasirika ukaja sghangaa baada ya hasira kuisha na wee kutuliza akili. l

Baada ya kugundua hili sasa unapaswa ujifunze kutulia pindi unapokuwa na hasira. Kwa maana hasira ni jambo moja na matokeo ya hasira ni lingine. Tafakari, chukua hatua!
 
Kuna baba ambaye alimtandika mwanawe mdogo vidoleni kisawasawa kisa alichora kwenye mlango wa gari. Mtoto ilibidi alazwe na ikagundulika ameumia sana na vidole vyake havitakua tena. Yule baba alisikitika sana na akarudi kwenye gari na kupga teke mlangoni. Badae akaona pale alipokwangua mwanawe aliandika, 'I love you Daddy'....
 
Ukimnyoshea mtu mkono kumpiga unaweza ukaurudisha angani au kuukwepesha usimpige au usimpate. Hata hivyo ukilitoa neno ambalo hukulimaanisha na likampata mwenzio huwezi na hauna jinsi ya kulirudisha. Neno likishatoka limetoka hata ukijaribu kulifuta halifutiki bali huacha alama. Lakini wapo watu ambao husema maneno makali wakiwa na hasira maneno ambayo japo wanaweza kujaribu kuyapoza kwa mabusu, miguso na samahani nyingi. NImeyasikia mengi sana kwa mfano mtu katika hasira anaanza kumuita mwenzie:

"Mpumbavu wewe"
"mwanamme gani wewe"
"malaya Mkubwa"
"Kwani miye mtumishi wako"
"Acha mambo ya kijinga"

Je kuna maneno ambayo umewahi kusikia watu wakiyasema na ukajua si mazuri kuambiana hasa watu ambao mnadai kupendana? Je wajua madhara ya maneno yalivyo katika hisia na mioyo ya watu? Inakuwaje mtu mtukanane halafu mwende chumbani pamoja? Je unajua wakati mwingine mtu anaenda pembeni ya pendo lake ili akapate maneno ya utulivu na ya kutulizwa?

THINK ABOUT IT: IF YOU DON'T MEAN IT DON'T SAY IT!

n.k n.k

Kaka hizo misuguano na maneno kama haya zipo tu, yaaani ukiona hazipo kabisa ujue kuna kasoro, na hizi zilianza pale wale wazazi wetu wa mwanzo walipo haribu kule bustanini. it is much easier living real life than ideal life, na wanadamu ni wavivu kwa asili so wanapenda rahisi, na hata ikifika kwenye madhara ya hivyo vinavyofanywa kwa urahisi bila kufikiri, wanakwepa pia.
 
siwasemi kina mama ila wao ndio haswa wenye tabia za kuongea chochote wanapokasirishwa
kuna rafiki angu alishaambiwa hana mbegu za kumzalisha na watoto alionao sio wake yeye ni mshika pembe
tu anatunzia wengine.yule bwana alikuwa mstaarabu alitoka bahati tulikutana nae bar fulani mitaa ya mwenge
tulimshauri ajipe moyo atulie so long watoto wanamfanania.ilikuwa kesi kubwa ila kwa sasa jamaa ana mpango wa nje
kitu ambacho hakuwahi kudhania angefanya na mapenzi kwa mkewe sii kama zamani,hapo ndo nakubali madhara ya ulimi.
 
Sasa mtu anamwambia mwenzake vitu kama hivyo anatarajia nini baadaye?
"Mtu akinambia kila siku kua mimi ni mjinga, the day I have to choose between kumtendea jambo la busara au kumtendea ujinga, nachagua ujinga because that is how he sees me, hata shangaa. nikitenda kwa busara atacheka na kuneng'eneka: ehen? leo you want to play the smat girl and surprise the world?
Basi naona ya nini kujitesa? give him what he asks for..."​
Well, that is not me, ila ni reasoning ya watu wengi ninao wajua.
 
Wakati wote .... Pinga au toa marekebisho bila hisia hasi za hasira, chuki na kadhalika!! ...Kwa namna yeote kama una fundo la hisia hizi.. airisha matamshi yako kwa unayemkusudia...kuarisha huko ndio Ujasiri,Ushindi na Upendo wa dhati! Ni ushindi na upendo kwani umeamua kwa akili timamu kabisa kufanya hivyo!!

Masikini_Jeuri;2788450]Nyote wa wawili mmenena mambo muhimu sana lakini tunahitaji kusaidia njia za haraka za kudhibiti hizi hasira

Njia ya haraka iko based na understating yako kabla ya tukio la kupata hasira. Uelewa wako ukiwa unakuruhusu kuona kuwa hasira ni tatizo then utakuwa unasababu tayari ya Kui overcome! Na utakuwa tayari kuhesabu moja hadi mia moja kimoyo moyo kabla ya kutamka na kuchukua hatua ambayo kwa wakati huo utaiona ni haki na sahihi, lakini kwa makusudi unahesabu hadi one hundred before you speak out or act in any way!! ... Simply because you have a reason and you understand!!

Baada ya kugundua hili sasa unapaswa ujifunze kutulia pindi unapokuwa na hasira. Kwa maana hasira ni jambo moja na matokeo ya hasira ni lingine. Tafakari, chukua hatua!

Hicho kipindi cha kufanya mahesabu kwa sababu umeamua kwa msukumo wa undersatanding yako ...hicho kipindi ..Nigekiita kipindi cha utulivu na tafakari ili baada ya mahesabu hayo, sasa ... Ndipo uchuke hatua! Yes ..Contemplation while doing the silent counting in your heart!

This shows your character and in fact the real meaning of greatest love!!
 
Back
Top Bottom