vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 1,375
- 2,513
Nimeona watu humu jukwaani, na mitandao mengine kumlaumu kocha wa Yanga kutofanya rotation.
Mshabiki wa Yanga mwenye akili timamu hawezi kulilia kocha afanye rotation kwenye mechi ngumu tena ni za klabu bingwa.
Mechi ngumu huchezwa na wachezaji wanaoaminika na kocha, lakini watu wanajifanya kukosoa eti kwanini Nkane, sijui Farid hawapangwi, je Nkane, Farid, Ngushi, n.k je wana quality ya kupambana dhidi ya Al Ahly? Wale Medeama na spidi ile wangeweza hao akina Ngushi?
Kuhusu rotation, Yanga bado wana michezo mingi sana mbeleni, kuna mechi za ligi kuu na mashindano ya Azam federation cup hivyo watakuja kupangwa kwenye mechi za huko mbeleni na sio kwenye ngumu za klabu bingwa eti umpumzishe Aucho halafu umuweke Mauya au sureboy, eti kisa rotation huo ni ujinga.
Yanga ina mechi ya ligi kuu tarehe 15 kisha tarehe 20 ina mechi ya klabu bingwa, hapo ndipo kwenye mazingira sahihi ya kufanya rotation kwa kocha ili kujipanga kwa mechi ya klabu bingwa. Kocha alikuwa muumini wa kufanya rotation tena alikuwa ni zaidi ya Nabi, kila mechi wanapata nafasi wachezaji tofauti tofauti kasoro Mshery peke yake hakuwahi pangwa ila akaja kudhihirisha kuwa kumbe sio wachezaji wote wa Yanga wana quality ya kucheza Yanga. Kikosi cha pili cha Yanga kimeshindwa kumfunga hata Ihefu iliyokuwa mkiani. Kile kipigo kimemfanya kocha akose imani na wachezaji wengine.
Haya malalamiko yanakuja kwavile Yanga haipati matokeo, ila kwa watu wanaojua mpira tulijua fika kuwa Yanga inashida ya straika wa maana. Kwa mpira unaochezwa Yanga kwasasa kama kungekuwa na straika wa maana, mpaka sasa timu ingekuwa na point sita na sidhani kama haya maneno ya kocha hafanyi rotation sijui maneno ya kocha hana mbinu yangekuwepo. Yanga ya mzize, Musonda na Konkoni ni changamoto kwa Gamond.
Binafsi sioni kasoro ya Gamondi mpaka sasa, timu haina straika wa maana na pia huwezi kufanya rotation kwenye mechi ngumu unayohitaji matokeo. Wenzetu wakimpumzisha mtu anaingia mtu mwenye quality sawa nae au kumzidi. Ila pale Yanga ni nani anaweza kuvaa viatu vya watu kama Pacome, Aucho, Yao, Bacca, Diarra, Max, Lomalisa, kwa ufasaha?