Maneno aliyosema Lema Olasiti Arusha

Maneno aliyosema Lema Olasiti Arusha

Status
Not open for further replies.
quote_icon.png
By Chintu
...umeshaanza kuukubali unabii eeh!
Na hata utabiri wa Sumaye umetimia pia kwamba Anayeingia madarakani kwa hila na kalamu "...atatawala kwa risasi" Yametimia kwa Mwangosi, yametimia Arusha tar 5 January, yametimia Morogoro kwa kijana muuza magazeti, yametimia Songea, yametimia kwa wanafunzi uhasibu Arusha kupigwa mabomu kisa kilaza RC, yametimia kwa Lema kuvamiwa nyumbani kwake kama jambazi wakati wangeweza kumuita tu hata kwa simu. Na sasa wanabadili style ni mwendo wa kung'oa meno, kucha na macho. ama kweli Dr na Sumaye ni manabii --sijui waliyaonaje haya -Mungu ana watu wake anaowapa maono kuwatahadharisha viumbe wake. Hongereni Dr Slaa na Mh Sumaye kwa unabii wenu akina WABHEJASANA waliwabeza lakini sasa wanaanza kuwaelewa taratibu.




quote_icon.png
By WABHEJASANA
Hizi ni 'NJEMU' tu hakuna kingine hapa.FULL STOP.



What do you mean Mkuu? au hoja hazijibiki? ni kazi sana kuwa wakili wa Ushetani wa magamba.

Naona umeamua kurukaruka hovyo. Nimesema ni kazi sana kuwa wakili wa mashetani - ona sasa hata kuongea unashindwa.
 
CCM walianzisha vipi udini?

Walianzisha pale walipo anza kuihusisha CUF na Dini ya Kiislamu baada ya Cuf kuwabana ktk chaguzi mbalimbali.Lakini sio Cuf tu hata sasa CDM wanahusishwa na Ukristo.Na hii yote ni baada ya Ccm kuwa inabanwa na CDM kama ilivyokua kwa CUF.

Kwa maana hiyo huwezi kuitenga Ccm na Uanzilishi wa Udini.kumbuka wakati wa Uchaguzi mkuu wa 2010 kauli alizokua anatoa Katibu mkuu wa ccm wakati huo Yusuf Makamba.Eti watanzania wasimchague mgombea wa Cdm kwa kua ni Padri alishindwa kuongoza kanisa je nchi ataiweza?

Kumbuka kauli ya Mwigulu Bungeni kuhusu dk Slaa kwamba wakati wa Kampeni uchaguzi mkuu 2010 alikua akikutana na baadhi ya Wachungaji ktk vokao vyake vya ndani.

Je kauli kama hizi huoni ni ya kutugawa Waislamu na Wakristo.tena kauli inatolewa na kiongozi mkubwa wa Chama chenye kuunda Serikali.Ikitokea CDM ikatwa Dola huoni Waislamu watakosa imani na Serikali kwa kufikiri kwamba ni kweli ni ya Wakristo?

Ccm wanachofanya ni kujaribu kutumia mbinu zozote hata kama ni za kuuwa au Kuvunja Umoja wetu ili tu waendelee kuwepo Madarakani.

CCM NI GENGE LA WAHUNI NA HAIKUBALIKI TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA!!!!!
 
jamani mi chadema ila sina imani na lema kutokana na hili tukio.kama ushahidi wenyewe aliosema ni hili tukio sitakuwa na shaka kufananisha na mchezo mchafu wa mwigulu kuhusu video.ntaamin lema amefanya huo mpango ili kupigilia hoja yake ya udini.na historia ya lema sidhan kama anashinda kufanya hiyo mipango.naichukia CCM kutufikisha hapa ila kwa hili naanza kudoubt juu ya CHADEMA
 
Baadhi ya Waislam wanaona kama vile Wakristu ni maadui zao. Nilisoma post za Majimoto kule kwa biashara ya uchawi tanzania nikaona mahali pameandikwa, kuwa majini hayapendi kabisa kusikia neno Kristu. Neno hilo huyapa majeraha kila yalisiakiapo. Si ajabu vikundi hivyo vya Kiislam vinafuga hayo majitu na ndio maana kila kukicha wanapamabana na Kristu.
 
Radio Maria baada ya kuona Mh. Lema anaongea pumba walimtoa hewani. Na kwa kuonyesha kwamba hawabahatishi, walimtoa hewani mara mbili.

Mh. Lema akili yake haipo sawa, kuna uwezekano mkubwa alipokuwa mtoto alisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
haya tuwekee hizo pumba nasi tujudge, kwn kuna watu kama wewe waliotoa dhahabu wakapewa shanga
 
jamani mi chadema ila sina imani na lema kutokana na hili tukio.kama ushahidi wenyewe aliosema ni hili tukio sitakuwa na shaka kufananisha na mchezo mchafu wa mwigulu kuhusu video.ntaamin lema amefanya huo mpango ili kupigilia hoja yake ya udini.na historia ya lema sidhan kama anashinda kufanya hiyo mipango.naichukia CCM kutufikisha hapa ila kwa hili naanza kudoubt juu ya CHADEMA

Wewe siyo chadema mkuu. Chadema hakuna mbulula kama wewe.
Ulitaka kujua alichosema Lema ni kweli subiri ushahidi wake kuwa Jk ni muasisi wa udini tanzania. Labda spika aufiche kapuni
 
twaweza kusema kauli ya Mh. Lema haikuwa nzuri na kuwa sawa lakini tunasahau kuwa katika wakati mgumu kama ule ndipo mtu huweza kusema ukweli wa moyoni badala ya unafiki wa kupima maneno.
Ukiangalia habari zinazoanza kutiririka sasa, sio muda mrefu ukweli wa tukio hili utaanza kujulikana (kama RC/RPC walivyowaomba wananchi kutoa ushirikiano kumtafuta mhusika) na kwa mshangao wa wengi ambao ni great thinkers ndio watajua kuwa hayo maneno ya Mh. Lema hata ni 'cha mtoto' kulinganisha na ukweli wenyewe.
Sio ajabu sana maana duniani kote nchi zilizoendelea zilijengwa na wananchi wake na nchi masikini pia zimedumazwa na wanachi wake hao hao!
 
CCM walianzisha vipi udini?

Hivi ndivyo walivyoaanzisha ndugu zako Mafisadi au Magamba

Katika kipindi chote hicho cha miaka kumi na mitano suala la kuwa Dk. Slaa alikuwa ni padre halijawahi kuwa jambo la kuwakwaza watu. Aliposimama kuwanyoshea vidole mafisadi bungeni alimtaja miongoni mwao mtu ambaye alikuwa ni Mkristu, Gavana David Balali.

Suala la kuwa aliwahi kuwa Padri halikuwa suala kubwa. Na aliposimama pale Mwembe Yanga alitaja majina ya watu mbalimbali kuwatuhumu vitendo vya ufisadi. Hakukuwa na mtu yeyote aliyesimama na kusema ‘imekuwaje mbunge aliyewahi kuwa padri kufanya jambo hili"?

Ukweli ulibakia ni kuwa Watanzania hawakujali dini ya Dk. Slaa wala hali yake ya upadre. Watanzania walitamani na hatimaye walipata mwanasiasa mwenye ujasiri wa kuita embe embe, chungwa chungwa, na kitunguu kitunguu!

Hadi pale chama chake kilipompendekeza kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania. Hapo ndipo tulipoona wabaguzi wa kidini wakianza kujitokeza na kufanya suala la upadri wa Dk. Slaa kuwa hoja.

Kwanza walianza kuhoji ana "udaktari" wa kitu gani? Wakaanza kubeza kuwa udaktari wake ni wa "Elimu ya Kanisa" na hivyo siyo elimu hasa na wengine wakajenga hata hoja kuwa labda hastahili kuitwa daktari. Licha ya maelezo ambayo yalitolewa wakati ule na kuwapa watu elimu kuwa shahada ya uzamivu aliyonayo inatoka kwenye chuo kinachotambulika na siyo ya kununua kama ya kina fulani bado wengine hawakuridhika.

Au soma hapo: https://www.jamiiforums.com/tanzani...aliyeingiza-udini-kwenye-kampeni-hizi-18.html

Kutoka kwa
Mzee Mwanakijiji
 
CCM walianzisha vipi udini?

Kama una uwezo wa kutaja, basi taja ni mahakama za dini zipi ambazo ziliwekwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ambazo zingeshughulikiwa na CCM kama ahadi ya uchaguzi.
 
Kwa hili hakuna udini ila ni chuki za mtoto wa mama mkubwa na mama mdogo ambazo waislamu hawajastafautashi kati ya dini na hii chuki.
Isaka ni mtoto wa mama mkubwa na Ismaeli ni mtoto wa mama mdogo.
Isaka ni uzao wa kikisto na ismael ni uzao wa kiislamu lakini wote ni watoto wa baba moja ila mama tofauti.
Tutafakari ni tuusiige uadui wa mtoto wa mama mkubwa na mama mdogo.
Tugiuleze ni kwa nini ukristo hakupokelewa na Waarabu wakati wamepakana na Waisraeli?
Waarabu walisema kuwa huyu naabii Yesu alikuwa kwa ajili ya mayahudi na siyo kwa ajili yao na wao walisubiri mtume wao kwa miaka 700.
Tuache ushabiki wa kidini kwa sababu inchi hii itakuwa haikaliki.
 
Nilikuwa mmoja kati ya watu waliokerwa na maelezo kuhusu Lema lakini kama kweli haya ndo aliyoongea sioni ubaya ulipo,badala yake nadhani amesimamia ukweli, ccm wanaiharibu nchi yetu

Hapo kwenye RED umethibitisha jinsi JF ilivyojaa wakurupukaji wa kuamini kila kinacholetwa kama unavyoamini maneno ya mganga wa kienyeji.

Sasa, mwanzoni ulikerwa na nini wakati binafsi niliweka maneno haya kwenye thread zangu za jana.
 
Radio Maria baada ya kuona Mh. Lema anaongea pumba walimtoa hewani. Na kwa kuonyesha kwamba hawabahatishi, walimtoa hewani mara mbili.

Mh. Lema akili yake haipo sawa, kuna uwezekano mkubwa alipokuwa mtoto alisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.


Huenda unatoa ushuhuda wa yaliyowahi kukukuta wewe!
 

Yaani Haujui? Ni kivipi Sheikh Ponda alipata fursa ya kuongea Hadharani dhidi ya Dini zingine? Bila ya Serikali kujua?

Inakuwaje Rais hajui UDINI ulianzaje wakati campaign zake za 2010 alikuwa anaongelea UDINI na UKABILA? Bila Tricks zake za DIVIDE and RULE unadhani anakuwa Rais wa NCHI hii this term?

Lakin vile vile maneno ya Dr Slaa mara alipohisi amedgulumiwa kura zake alitamka wazi kabisa KUWA NCHI HAITAWALIKI. Je haya mnayatazamaje ?

nafikiri WaTz mjikite zaidi katika kutafuta ukweli kuliko kuanza kutazamana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya dini zenu na makabila yenu.

Na kama mtaona pazito waiteni FBI wawasaidie kama walivyofanya kule Znz mjue ukweli na uongo upo wa wapi. Suala je ripiti ya FBI kuhusu Znz ipo wapi? au ndo imefichwa kabatini!

 
Wewe unatazo la ubinafsi, je SHEKHE PONDA NDIYE MUASISI WA UDINI TANZANIA? KUWA MKWELI ILI TUINURU INCHI YETU. MUKIENDELEZA UBAGUZI KAMA HUU WA JAMII FORUM TUTAFIKA TUSIKOKUPENDA.

KUNA MENGI YANAENDELEA YA AJABU- Serikali ya CCM Ndo iko madarakani Mihadhara ni mingi ya kushambuliana katika Misikiti kusakama Ukristo. Kuna madhehebu machache pia madogo ya Kikristo yanayoendesha mihadhara kusakama uislamu. Kuna CDs kibao Zinasambazwa mitaani zinauzwa. Ndo MAANA Mbunge mmoja alisema hakuna haja ya Raisi kukutana na Masheikh na Maaskofu, akamate wachochezi. WAKATI WA MWALIMU HIVI VITU HAVIKUEPO. Makanisa kuchomwa moto imetokea mara nyingi tu Huko Zanzibar. Yako mengine mengi tu kama ya mbagala na huko Geita. HAPA MTAWALA NI NANI? Mbona watu hawaogopi, mbona hawa wachochezi hawaogopi? Huko Arusha baada ya Sheikh kulipukiwa/kulipuliwa na bomu nyumbani kwake hakuna anaejua police iligundua nini na ni hatua gani zilichukuliwa. Bomu la Jana wanasema huenda ni haya ya kutengeneza mitaani nani anajua yametengenezwa mangapi? Na ni nani anasimamia hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa gharama zake? WAKATI WA MWALIMU LEO WANGEKUA WOTE WAMEKAMATWA KWA KUTAJWA AMA KUKUTWA NA USHAHIDI asingelala mtu popote panapohisiwa. CCM Msijitenge na matatizo ya udini Mmeyalea sana.

Kuhubiri washindani wako kisiasa ni wadini una maana kuna dini wamefungamana nayo! Maana halisi ni kuwa chama cha wenzako kina dini na cha kwako hakina dini (tafsiri ya mwalimu Tanzania haina dini ila watanzania wana Dini). Wakati CCM ikisema CHADEMA nI WADINI ili maanisha ni wakristo na Iliposema CUF ni Wadini ilimaani sha ni Waislamu. SHERIA YA VYAMA VYA Siasa iko wazi chama cha kidini hakiruhusiwi nchi hiii, Chama cha kikabila hakiruhusiwi nchi hiii, Sheria zinazosimamiwa na CCM hazikufuatwa majukwaa yametumika vibaya kuwapa imani watu wa imani tofauti kuonana ni kama maadui katika nchi hii.

Imefikia mahali tutakua hatuli tena pamoja na kunywa yatakuja tu!

Ciao!!!
 
Lakin vile vile maneno ya Dr Slaa mara alipohisi amedgulumiwa kura zake alitamka wazi kabisa KUWA NCHI HAITAWALIKI. Je haya mnayatazamaje ?

nafikiri WaTz mjikite zaidi katika kutafuta ukweli kuliko kuanza kutazamana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya dini zenu na makabila yenu.

Na kama mtaona pazito waiteni FBI wawasaidie kama walivyofanya kule Znz mjue ukweli na uongo upo wa wapi. Suala je ripiti ya FBI kuhusu Znz ipo wapi? au ndo imefichwa kabatini!



Ni kwasababu ya JINSI mgombea wa CHAMA TAWALA alivyokuwa anawabaguwa WAPINZANI oh CUF ni Waislamu; CHADEMA ni WAKRISTO... Miswachague... Hapohapo hakujua ya kuwa kaingiza DOA la UDINI ndani ya MIDOMO ya watu

Yeye Kama Rais; Lazima ana washauri na Lazima akemee chochote kinachohatarisha NCHI; Amesikia UDINI anakimbia ansema hajui UMEANZAJE sawa Jaribu kuufuatilia na kuuzima basi???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom