Hivi kweli tukiziweka fikra zetu kuwa huru, Tutasema Hayati Madiba ni Shujaa wa Waafrika au Wazungu?
Nasubiri kwa hamu kusikia yaliyojiri kaburini ambapo wazee wa kimila walijiandaa sana kwa taratibu nyingi za kiasili kwa ajili ya mazishi ya chifu wao...
Hata hivyo ninashawishika kusema kuwa Viongozi wa Kikristo wamefanikiwa kuteka nyara taratibu za mazishi... na je ule uvumi (sina vyanzo vya uhakika) kuwa Dume la Ngómbe litazikwa nae utaratibu huu utatimia????
Huu mgongano wa mila na imani kwa waafrika ni kitu cha kushangaza sana.Mila zetu nyingi zinaambatana na mauzauza.Hii huwa inajipa jibu kuwa waafrika huingia kwenye dini kama fashion tu ili tuonekane wa kisasa lakini mila ambazo zinaconflict imani huwa hatuziachiNINAONA MGOGORO WA KANISA NA WAZEE WA KIMILA KATIKA KUANDAA MAZISHI SIJUI MMENOTICE WADAU?
Mazishi yalipaswa kuanza saa 4 ili kuruhusu hatua za kimila kufuata kuelekea njia ya kaburini, lakini Kiongozi wa Kanisa amehakikisha amekula muda wa kutosha ili tukio hili lisitokee, pia hajaondoka pale mbele inawezekana anasubiri kuchukua hatamu... sina uhakika hali itakuwaje nina hamu sana ya kujua jinsi watakavyobalanc makundi haya mawili ambayo yamekuwa yakizozana kuhusu utaratibu wa mazishi
kuliko winie na Gacia au Mandla na Ndaba?Duhhhhhh...nna majonzi sana