Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,157
- 28,766
Namheshimu sana Mandela, lakini nimekuwa nikijiuliza sana, hivi ni nini hasa kinachofanya Mandela akuzwe sana duniani? Mara nyingi naona Mandela amekuzwa kulikoanavyostahili. Hivi ni lipi hasa la ajabu sana alilowafanyia Wa-South Africa,kuwapa uraisi wa mtu mweusi? Kwanza hata hayo mazungumzo ya kupata raisi mweusiAfrika Kusini Mandela hakushiriki kiasi hicho, walishiriki wengine.
Hebu linganisha Nyerere na Mandela katika kuchangia ukombozi wa demokrasia Afrika Kusini. Maoni yangu ni kwamba Nyerere alikuwa na mchango mkubwa kwa ukombozi wa Afrika Kusini kuliko hataMandela. Kumbuka Nyerere ndie aliyewashawishi ANC na wengineo AfrikaKusini wafanye mazungumzo na Makaburu, mazungumzo yaliyozaa demokrasia Afrika Kusini.In fact baadhi ya ANC walimtukana Nyerere alipowaambia wakae na kuzungumza naMakaburu. Kumbuka pia Nyerere ndiye alieanzisha kampeni iliyoitwa "boycottSouth Africa" kwa kampuni za kimataifa kutofanya biashara na Afrika kusiniya Makaburu.
Nyerere huyo huyo ndie aliyesababisha Afrika Kusini iondolewe kwenyeCommonwealth, jambo ambalo Makaburu waliona ni pigo kubwa sana. Nyerere ndiealiyetoa ardhi kwa kambi za ukombozi wa kusini mwa Afrika ili eneo lote lakusini likombolewe, kutia ndani kambi za wapigania uhuru za ANC, PAC (SouthAfrica), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZAPU, ZANU-PF (Zimbabwe) na MPLA(Angola). Nyerere alikuwa akitoa ndege kwenda kuwatorosha wapigania uhuru tokaSouth Afrika, ambapo kuna ndege moja ya East African Airways ililipuliwa ikiwakwenye hiyo mission. Nyerere ndiye alikuwa mstari wa mbele kuzuia mataifa ya nje kuwauzia Makaburu silaha akisema silaha hizo zilitumika dhidi ya watu weusi.
Halafu Mandela huyu, ziara zake za kwanza baada ya Afrika kusini kupata uhuruhaikuwa kuzitembelea nchi zilizoisaidia Afrika Kusini kupata demokrasia, balialienda Ulaya. Alipotaka kufanya ziara ya pili Ulaya kabla ya kuzitembelea nchizilizowasaidia alikataliwa na baadhi ya watu ndani ya ANC. Mandela alidai etianaenda Ulaya kuwaelimisha kwa nini ilikuwa muhimu yeye aachiwe kwa sababu nchikama Uingereza na Marekani waliwashauri Makaburu wasimwachie huru.
Suala la msamaha kwa yale Makaburu waliyowafanyia Wazalendo halikuwa laMandela, bali sehemu ya makubaliano katika mazungumzo kati ya Makaburu na ANC.
Basi hadi leo nashindwa kuelewa ni nini hasa kinachofanya Mandela akuzwe kiasihiki. Kwa sababu alifungwa? Mbona wapo wengi tu waliofungwa nae hatusikiiwakivuma kama Mandela?
Binafsi hata huwa inanisikitisha na kuniuma sana kwamba South Afrika huwa haionyeshi appreciation kamili kwa mchango alioufanya Nyerere kwa ukombozi wa nchi yao. Leo hii vijana wa South Afrika hawamjui Nyerere, wanajua uhuru wao uliletwa na Mandela tu. Nasikia kuna barabara pale Durban inaitwa Nyerere, kweli hiyo ndiyo shukurani ya Afrika Kusini kwa Nyerere? Tanzania tunaonekana kumuenzi Mandela mara nyingi zaidi ya South Afrika wanavyomuenzi Nyerere, tumetoa majina ya Mandela kwa barabara muhimu, viwanja nk, kama vile wao ndio waliotusaidia sisi. Kwa nini? Nasikitika sana. Kweli tenda wema uende zako.