Mandela anakuzwa kuliko anavyostahili?

Mandela anakuzwa kuliko anavyostahili?

In my opinion, soma kitabu cha "long walk to freedom" by Nelson Mandela!
Hapo utaona mchango wa mandela katika ukomboz wa S.A and kwa nn anaheshimika!...
On the other side, naamini kuwa nyerere alikua na mchango mkubwa sana katika ukomboz wa AFRICA, n kama unafuatilia mambo na kusoma articles mbalimbali huwez kataa hili!...
N sio kwamba MANDELA anaheshmika zaid ya nyerere BUT kwa sababu he is alive ni rahis kumzungumzia yeye kuliko NYERERE, NKURUMAH na wengne wenggi katka historia ambao wametangulia mbele ya haki!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Umesema yote mkuu Micka
 
Last edited by a moderator:
kila mtu ana aina yake ya umaarufu
watu kama nyerere, kwame nkrumah, amilcar capral (sina uhakika kama nimeandika jina lake kwa ufasaha), frantz fanon, kaunda, leopord sengho hawa ni maarufu sana miongoni mwa wasomi kwani walikuwa viongozi, wanaharakati na wasomi. hawa walikuwa na falsafa zao mfano socialism and self reliance ya mwalimu, humanism ya kaunda, consciosism ya nkrumah nk. niliowataja walikuwa na uwezo wa kuandika na hata kuwa wahadhiri wa vyuo vikuu. kwa upande wa mandela na kenyatta hawa walikuwa viongozi na wanaharakati tu lakini walikosa kipawa cha usomi/falsafa (intelectual capabilities)

hivyo basi kwa ufupi nyerere na nkrumah walikuwa viongozi, wanaharakati, wasomi na wanafalsafa, umaarufu wao ni mkubwa sana miongoni mwa wasomi. wakati mandela ye alikuwa kiongozi na mwanaharakati (hakuwa/si mwanafalsafa) na umaarufu wake upo kwa watu wa kawaida tu, si kwa wasomi
 
Hakuna kama Mandela wewe! Miaka 27 upo gerezani sio kwa kubaka wala ufisadi, Upo kutetea watu wako 27 years unaichukulia poa sio? Acheni Mahabba jamani!
 
A Person who was Jailed in Prison for 25yrs kwa ajili yakutetea haki ya ndugu zake, sidhani kama anastahili kulinganishwa na yeyote duniani na si Africa tu. ikumbukwe alikuwa na uwezo wakukubali vishawishi vya makaburu wampe maisha mazuri na familia yake but aliona vyote ni batili kwake ila haki na ukombozi wa waafrica wenzake tu, Mandela alikuwa tayari kwa lolote hata kugharimu maisha yake, He sacrificed everything including his Prety and beutful Wife(Winie). Baada ya Jela miaka 25 akawa Rais kisha kufanya kampeni ya maridhiano hasa kwa watu wake ambao walikuwa na machungu na hasira za mateso kutoka kwa wazungu. Nadhani kwa karne hizi ni wachache wa Aina yake labda karne za mitume.

Kwa hulka ya mtu mweusi ANGEWATOSA TU WENZAKE,asingekubali mateso kukaa Jela miaka yote hiyo hali ameshaahidiwa Neema na wazungu. Mandela ni aina ya viongozi ambao hata kama nchi yake itabidi kuingia vitani basi angekuwa tayari kupigana bega kwa bega na watu wake hadi mwisho, sio kama viongozi wetu wengi ambao ikitokea nchi inapata migogoro basi si ajabu hata kabla ya KIPENGA/FILIMBI kupigwa utashangaa nchi nzima viongozi wamelala mbele hadi wabunge na familia zao wapo UGHAIBUNI.
 
Ukiwa Nchi tajiri kama USA hata mtoto mdogo anamjua Mandela lakini sio The Legend him self JK Nyerere!!! Nadhani jina la South Africa linachangia.

Bila Nyerere historia ya Africa ingekuwa nyingine!!!
 
A Person who was Jailed in Prison for 25yrs kwa ajili yakutetea haki ya ndugu zake, sidhani kama anastahili kulinganishwa na yeyote duniani na si Africa tu. ikumbukwe alikuwa na uwezo wakukubali vishawishi vya makaburu wampe maisha mazuri na familia yake but aliona vyote ni batili kwake ila haki na ukombozi wa waafrica wenzake tu, Mandela alikuwa tayari kwa lolote hata kugharimu maisha yake, He sacrificed everything including his Prety and beutful Wife(Winie). Baada ya Jela miaka 25 akawa Rais kisha kufanya kampeni ya maridhiano hasa kwa watu wake ambao walikuwa na machungu na hasira za mateso kutoka kwa wazungu. Nadhani kwa karne hizi ni wachache wa Aina yake labda karne za mitume.

Kwa hulka ya mtu mweusi ANGEWATOSA TU WENZAKE,asingekubali mateso kukaa Jela miaka yote hiyo hali ameshaahidiwa Neema na wazungu. Mandela ni aina ya viongozi ambao hata kama nchi yake itabidi kuingia vitani basi angekuwa tayari kupigana bega kwa bega na watu wake hadi mwisho, sio kama viongozi wetu wengi ambao ikitokea nchi inapata migogoro basi si ajabu hata kabla ya KIPENGA/FILIMBI kupigwa utashangaa nchi nzima viongozi wamelala mbele hadi wabunge na familia zao wapo UGHAIBUNI.
 
Namheshimu sana Mandela, lakini nimekuwa nikijiuliza sana, hivi ni nini hasa kinachofanya Mandela akuzwe sana duniani? Mara nyingi naona Mandela amekuzwa kulikoanavyostahili. Hivi ni lipi hasa la ajabu sana alilowafanyia Wa-South Africa,kuwapa uraisi wa mtu mweusi? Kwanza hata hayo mazungumzo ya kupata raisi mweusiAfrika Kusini Mandela hakushiriki kiasi hicho, walishiriki wengine.

Hebu linganisha Nyerere na Mandela katika kuchangia ukombozi wa demokrasia Afrika Kusini. Maoni yangu ni kwamba Nyerere alikuwa na mchango mkubwa kwa ukombozi wa Afrika Kusini kuliko hataMandela. Kumbuka Nyerere ndie aliyewashawishi ANC na wengineo AfrikaKusini wafanye mazungumzo na Makaburu, mazungumzo yaliyozaa demokrasia Afrika Kusini.In fact baadhi ya ANC walimtukana Nyerere alipowaambia wakae na kuzungumza naMakaburu. Kumbuka pia Nyerere ndiye alieanzisha kampeni iliyoitwa "boycottSouth Africa" kwa kampuni za kimataifa kutofanya biashara na Afrika kusiniya Makaburu.

Nyerere huyo huyo ndie aliyesababisha Afrika Kusini iondolewe kwenyeCommonwealth, jambo ambalo Makaburu waliona ni pigo kubwa sana. Nyerere ndiealiyetoa ardhi kwa kambi za ukombozi wa kusini mwa Afrika ili eneo lote lakusini likombolewe, kutia ndani kambi za wapigania uhuru za ANC, PAC (SouthAfrica), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZAPU, ZANU-PF (Zimbabwe) na MPLA(Angola). Nyerere alikuwa akitoa ndege kwenda kuwatorosha wapigania uhuru tokaSouth Afrika, ambapo kuna ndege moja ya East African Airways ililipuliwa ikiwakwenye hiyo mission. Nyerere ndiye alikuwa mstari wa mbele kuzuia mataifa ya nje kuwauzia Makaburu silaha akisema silaha hizo zilitumika dhidi ya watu weusi.

Halafu Mandela huyu, ziara zake za kwanza baada ya Afrika kusini kupata uhuruhaikuwa kuzitembelea nchi zilizoisaidia Afrika Kusini kupata demokrasia, balialienda Ulaya. Alipotaka kufanya ziara ya pili Ulaya kabla ya kuzitembelea nchizilizowasaidia alikataliwa na baadhi ya watu ndani ya ANC. Mandela alidai etianaenda Ulaya kuwaelimisha kwa nini ilikuwa muhimu yeye aachiwe kwa sababu nchikama Uingereza na Marekani waliwashauri Makaburu wasimwachie huru.

Suala la msamaha kwa yale Makaburu waliyowafanyia Wazalendo halikuwa laMandela, bali sehemu ya makubaliano katika mazungumzo kati ya Makaburu na ANC.

Basi hadi leo nashindwa kuelewa ni nini hasa kinachofanya Mandela akuzwe kiasihiki. Kwa sababu alifungwa? Mbona wapo wengi tu waliofungwa nae hatusikiiwakivuma kama Mandela?

Binafsi hata huwa inanisikitisha na kuniuma sana kwamba South Afrika huwa haionyeshi appreciation kamili kwa mchango alioufanya Nyerere kwa ukombozi wa nchi yao. Leo hii vijana wa South Afrika hawamjui Nyerere, wanajua uhuru wao uliletwa na Mandela tu. Nasikia kuna barabara pale Durban inaitwa Nyerere, kweli hiyo ndiyo shukurani ya Afrika Kusini kwa Nyerere? Tanzania tunaonekana kumuenzi Mandela mara nyingi zaidi ya South Afrika wanavyomuenzi Nyerere, tumetoa majina ya Mandela kwa barabara muhimu, viwanja nk, kama vile wao ndio waliotusaidia sisi. Kwa nini? Nasikitika sana. Kweli tenda wema uende zako.

Ni kweli kaka ila jambo la msingi hapa is price that Mandela paid for his people. Huyu bwana aliteseka sana kwa kuwapigania watu wake tofauti na Nyerere aliyekuwa anapiga porojo lakini haendi front.
 
Back
Top Bottom