Hapa Anderson na Forster wanashangilia wenyewe.
Hii timu kuna
WAZZA, VAN DER SAR , J.S PARK, Hawapo ilikuwa na Ubora kila Mahali, Picha karibu wachezaji 8 ni "World Class"
Ukweli Mchungu ni kwamba
Tumeshuka sana kuanzia kiutendaji mpaka kiuchezaji. Nyakati za Nyuma timu nyingi UTD ndo ilikuwa mfano wao ndo walikuwa wanachukua Viongozi toka UTD, Wachezaji na kuiga Mpaka Uendeshwaji.
Leo Hii timu Yetu Nahodha ni
BRUNO, Jamaa anajilalamikia Mpaka yeye Mwenyewe! Tukimkosa Licha mfumo mzima unabadilika kiuchezaji.
Msimu ulopita tumecheza na kina Weghorst lakini una Uhakika na timu, ETH aliwaambia fans tukutane Wiki ijayo tunaitoa Barca, walianza pata goli ila kwa uchezaji wetu ulikuwa unajua tutawafunga tu na ndicho kilichotokea,
FRED, WEGHORST wanaeza wasiwe Madaraja ya wachezaji wa UTD lakini walikuwa na ile Ari ya Wachezaji asili wa UTD.
Rashy anapiga Mpira nje anatupa mikono juu anarudi anafanya Jogging.
WAZZA, TEVEZ walikuwa wanakuja kama MBOGO na kizuri wakiwa na Mpira wana Ubora, Rashy anaweza kokota Mpira akampelekea Beki mguuni!
Palace, Nottingham, W/ham, Everton, Luton, Sheffield, zinashindwa chukua Watu wao kwa sababu tumewafunga na Mikataba mikubwa.