Ili kuweza kushindana unahitajika uwekezaji mkubwa, nafasi moja inapaswa kuwa na wachezaji wazuri zaidi ya wawili. Leo hii DM anategemewa Casemiro pekee na ndio huyo ameshakuwa babu, akiwa nje ni msala.
Huwa nawatazama wachezaji wetu, ni wazito sana, ni wazito kuanzia kichwani. Hawana uwezo wa kufanya maamuzi haraka, mchezaji anaweza kushangaa na mpira mpaka ukachukuliwa au anakaba kwa macho mpaka goli linafungwa.
Huko upande wa mabeki ndio tatizo kubwa, tuna beki nzito kimwili na kiakili. Bora Licha na Varane walikuwa kidogo wanawezana, Varane alichangamshwa na Licha.
Kichwa alichopiga Haaland akaokoa Onana alikipiga kama yupo mazoezini. Timu yetu bado inatakiwa kufanya uwekezaji kwa kununua wachezaji sahihi, nilikuwa nafikiri tuna wachezaji wazuri wengi lakini sikuwa sahihi.
Hii penati kwa kweli duuuh! ni kweli kashikwa ila jinsi alivyoanguka duu! Pamoja na kuwa timu yetu sio nzuri akichezesha Tylaor au Michael Oliver gemu yetu kutoboa huwa ni ngumu sana sijui ni maono yangu au wote tunaona hivyo.