Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Maana Kama kweli 10hag anaenda na onana Basi ahakikishe anagusa na engo nyingine kwa kuweka watu sahihi,isije kuwa Onana anacheza bado na mabeki ambao wachomaji au anapiga pass zake viungo wanaporwa

Ili umfaidi onana acheze na backline isiyo na uwoga wa kupiga pass ,viungo pia wasiwe waoga kupiga pass ,

Uchezaji wa onana Ni similar na Djigui Diara
 
Onana watu wengi wamemjulia fainali ya UCL ila amekuwa bora kitambo tangu akiwa Ajax tunaoangalia Eredivisie Fox Sports tunaelewa japo hatukumuweka akilini wala hatukutegemea siku moja atahusishwa nasi ukizingatia wakati huo tulikuwa addicted na vitu vya De Gea.

Mbali na ligi ya England ligi nyingi watu hawafuatilii sana hasa hizo Uholanzi na Italy sasa wangemjua vipi?
Unasema mbali na pasi zake anakosa vitu vingi vya kuwa kipa bora hebu vitaje,najua saves lazima ziwemo ndio kitu cha kwanza hicho anacho pia.Hebu leta vingine hapa ambavyo hana

Hebu nenda kaangalie skills zake ana kila kitu ama mnaona kisa Mwafrika

Kingine haruhusu bao 4-7 hovyo kama kipa wetu bora

Miaka michache nyuma sisi tulimsaka sana huyu mwamba ikashindikana. Mkimpata mmepata
 
Kwa msako ambao utd huwa tunafanyiwa na vitimu vidogo vidogo hasa Arsenal na Brighton kama tusipojirekebisha ipo siku tutamkumbuka De gea. De gea amekuwa akifanya save ambazo zimekuwa zikishangaza wengi hivyo kama tusipojirekebisha sioni kipa atayeweza himili misako ya namna ile.

Umeanza vizuri na ukaharibu hapo hapo. Msako unaofanywa na vitimu vidogo halafu unasema haswa Brighton na Arsenal? Aah bhana. Hakika unamaanisha vitimu vidogo vyenzenu kama Chelkenge na Liverkuku. Brighton na Arsenal ni timu kubwa sana kwenu
 
Arsenal ana Champions League ngapi?
 
wapo baadhi mfano mbappé.. alienda psg
kwa mkopo kutoka monaco kbla y psg
kumsajili mazima.
Huyo PSG waliogoga FFP ila walikuwa na uwezo wa kulipa zile €150m fasta.

Nazungumzia hawa ambao wanasajiliwa kwa mkopo ambao hauna uhakika wa kununuliwa fuatilia EPL kama kuna aliyetamba wengi ni za uso.
 
Kwa msako ambao utd huwa tunafanyiwa na vitimu vidogo vidogo hasa Arsenal na Brighton kama tusipojirekebisha ipo siku tutamkumbuka De gea. De gea amekuwa akifanya save ambazo zimekuwa zikishangaza wengi hivyo kama tusipojirekebisha sioni kipa atayeweza himili misako ya namna ile.
Hao Brighton sio kwetu tu wanajua kuzitesa timu zote za top 6 halafu pia kuhusu sisi kufanyiwa msako na timu ndogo ni ishara ya udhaifu,huwezi kuona timu zinazojua kucontrol mchezo kama City na Liverpool zinafanywa hivyo.

Njia pekee ya kujilinda ni kuumiliki mpira haswa na kutoupoteza hovyo ukifanya hivyo utamfanya mpinzani wako akose pa kuanzia kukushambulia.

Hicho kitu hakipo kwenye timu yetu wachezaji hawawezi kupiga pasi 10 bila kupoteza mpira na wakiupoteza hawajui kuurudisha kitu ambacho opponents huwa wanakitumia kama silaha wanatupress na tunafanya sana makosa ndio maana tukikurana na timu iliyo serious inatutandika sana haijalishi De Gea yupo vyema kiasi gani kama ile siku Brentford.

Eneo la kiungo hadi sasa nna wasiwasi nalo Bruno na Mount ni watu wa kutake risk pasi zao nyingi katika eneo la kati wanatoa sana maboko,ndio maana kocha alikuwa anamtaka sana De Jong,tukifika level za kuuchapa mpira kama wa Arsenal,City ama Liverpool hutaona vitimu vidogo vinatushambulia badala yake tukakuwa tunavitesa sana.
 
Umeanza vizuri na ukaharibu hapo hapo. Msako unaofanywa na vitimu vidogo halafu unasema haswa Brighton na Arsenal? Aah bhana. Hakika unamaanisha vitimu vidogo vyenzenu kama Chelkenge na Liverkuku. Brighton na Arsenal ni timu kubwa sana kwenu
HENRY14 sasa na wewe unaamini kabisa kua Arsenyo ni timu kubwa?
Hebu nitajie wewe timu kubwa yoyote Ulaya ambayo haijawahi kushinda Uefa na ina miaka zaidi ya 20 haijawahi kuchukua kombe la ligi na ina miaka 8 mfululizo imeshindwa kuingia top4.
 
Hiyo sekta ya kushambuliwa kama nyuki inakuwa inaashiria timu bado mbovu ina viungo wasiojua kucontrol mchezo kuna muda inatokea vitu vipo nje ya uwezo wa kipa ndio tunapigwa zile 4 4 hata 6 kabisa.

Timu ikija kujua kucontrol mchezo eneo la kati hatutaexperience hivyo tutakuwa tunaruhusu mashambulizi machache sana na yasiyo na madhara

So kushambuliwa sana shida sio kipa ni ya timu nzima,kama Onana atakuwa pazia whatever ila anahitajika kipa mwingine hata kama asipokuwa yeye sawa.

Ten Hag game za mwisho za msimu ndio zimemchefua kiasi hata akaghairi kumsainisha mkataba mpya De Gea.
Onana Ni usajili mzuri , bado sijaona EPL kipa anayemfikia kwa footwork,ila Kama una onana lakin viungo bado waoga kupiga risk pass , Wana passing ability mbovu ,Basi onana mtamuona Kama Erik Johora
 
Miaka michache nyuma sisi tulimsaka sana huyu mwamba ikashindikana. Mkimpata mmepata
Onana ana footwork ambayo mkipress anaweza kupiga pass Moja ikaenda Hadi kwa Winga

Mkapigiwa pass Moja ,Goli ,kaangalie UCL wachezaji wa City wanasifika kwa pressing ila walifika muda wanaogopa kumfata

Shida inakuja hapo manjesta anacheza na viungo gani
 
HENRY14 sasa na wewe unaamini kabisa kua Arsenyo ni timu kubwa?
Hebu nitajie wewe timu kubwa yoyote Ulaya ambayo haijawahi kushinda Uefa na ina miaka zaidi ya 20 haijawahi kuchukua kombe la ligi na ina miaka 8 mfululizo imeshindwa kuingia top4.
Manjesta ana miaka mingap bila ligi? Siumekaa miaka mitano bila taji lolote ,au unajisahaulisha
 
Manjesta ana miaka mingap bila ligi? Siumekaa miaka mitano bila taji lolote ,au unajisahaulisha
Hatuzungumzii miaka 5 bila ya kombe lolote, nimeuliza timu gani kubwa unayoijua wewe haijawahi kubeba kombe la ulaya Uefa au Europa na pia ina miaka 20 haijawahi kuchukua kombe la ligi na ina miaka 8 mfululizo haijawahi kufuzu kuingia kwenye top4.
 
Mashabiki wa CR7 mjiheshimu ndio mnaongoza kwa huu upuuzi wa kumchukia kocha
Screenshot_20230630-003214.jpg
 
Onana ana footwork ambayo mkipress anaweza kupiga pass Moja ikaenda Hadi kwa Winga

Mkapigiwa pass Moja ,Goli ,kaangalie UCL wachezaji wa City wanasifika kwa pressing ila walifika muda wanaogopa kumfata

Shida inakuja hapo manjesta anacheza na viungo gani
Sema atajaribu kulifanyia kazi mazoezini na kwenye mechi ndio maana kaomba,friendlies nyingi pre season
 
Hatuzungumzii miaka 5 bila ya kombe lolote, nimeuliza timu gani kubwa unayoijua wewe haijawahi kubeba kombe la ulaya Uefa au Europa na pia ina miaka 20 haijawahi kuchukua kombe la ligi na ina miaka 8 mfululizo haijawahi kufuzu kuingia kwenye top4.
Leta list ya timu kubwa hapa kwa mujibu wa forbes au FIFA au UEFA , halafu tuanze kuangalia moja Moja ,Mimi najua hata Forrest ana UCL 2 ,ila Ni timu ndogo tu
 
Hao sio mashabiki wa Manchester United, ni mashabiki wa Arsenyeto wanaojifanya ni mashabiki wetu kumbe ni mamluki.
Tena inawezekana huyo aliyefanya uhaini huo akawa ni Carasco Putin au Bachelor ll
Hao sio mashabiki wa Manchester United, ni mashabiki wa Arsenyeto wanaojifanya ni mashabiki wetu kumbe ni mamluki.
Tena inawezekana huyo aliyefanya uhaini huo akawa ni Carasco Putin au Bachelor ll

Mbona hao kina Bachelor na Carasco ni watu wenu?
 
Back
Top Bottom