Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Huyu jamaa 10hag alikuwa anamuhitaji kwani maana naona ni kama ametokea tu out of nowhere
 

Kwaiyo maguire anakiwasha sio?
 

Kwa sababu sisi tuna kroenke, sipendi tabia za matajiri kumnunua timu Kwa mapenzi na kumwaga mihela hovyo. Inaleta unfair advantage flani kwao Kwa sababu timu zingine zinajitahidi kutumia mbinu na akili na kulazimika kuwa wachumi...yeye ana mbinu na akili halafu na mahela kibao ya ziada pia. Nataka timu zote ziwe na mfumo wa kina Glazers na Kroenke, au zote zimilikiwe na Hawa matajiri vichaa . Wewe mwaga Hela na Mimi nimwage Hela tuone mwishowe
 
Bissaka namkubali sana anaweza kua press resistant mzuri kuliko wachezaji wetu wote, ila kama unamfatilia vizuri kwenye kutoa pasi hua anazingua sana, pasi zake nyingi hua zinaishia kwa opponent's.
Sasa huyu sio press resistant

Press resistant Ni yule anaweza kufatwa /kupressiwa na maadui hata watatu akatoa pass Moja tu ikawaacha hapo hapo

Ukiona mchezaji ana presiwa halafu anatoa pass kwa adui au mbovu Huyo Ni muoga au passing ability yake Ni mbovu ,

Ndio maana makocha wanaotaka kucheza kuanzia nyuma wanawasajili wachezaji wenye passing ability kubwa tu
 
Game ya Arsenal na Sporting CP ndio kati ya game zangu bora kabisa kuziona last season uwanja ulijaa wachezaji wa aina hiyo zilikuwa zinapigwa press ila kinachofanyika sasa ni ufundi mtupu hadi nikatamani siku moja nione Man United wakiupiga mpira kama ule.
 
Ok nimekupata mkuu hamis77
Bissaka tuseme ni Best Tackler kwenye squad yetu au Epl kwa ujumla.
Hua anafanya Tackling za kuogofya ndani ya box na anafanikiwa, ila kwenye Passing accuracy binafsi hua simkubali, mara kibao pasi zake hua zinaishia kwa maadui.
 
Bissaka ndiye beki ambaye hakuna winger dunian anataman kucheza nae ,

Ndio maana Mimi bado simuelewi 10hag , Huyo bissaka angeweza kumtumia vzr Sana zaidi ya hapo,

Pep anasema alipogundua anafungika Sana aliamua kutafuta wachezaji mabeki wanaowin duel na kukaba vzr ,ndio maana ukuta wake hauna natural Fullback wote wale Ni ma CB,

Bissaka muwekee kipa mzuri mguuni na mabeki wengine watatu wazuri mguuni , halafu usimpe majukumu ya kupanda mbele, angalia Akanji na Ake hawana majukumu ya kupanda ovyo, ila mkiwafikia hampiti
 
Yule Kocha wa Sporting anajua sana , soon ataenda timu kubwa

Alicheza na Spurs ya Conte , Conte alidhalilishwa Sana .
 
Sina imani na Onana kuwa kipa namba moja kiukweli labda aje awe chaguo la pili

Huwa namuona kama John Mwanda tu
Tupo wengi. Pale hamna kipa ila watu wabishi kwasababu ya ile fainali tu.

Hata Uzoho aliwahi kucheza mechi yake vizuri sana pale OT na alikuwa ni backup GK wa Omonia.

Onana ukitoa pasi zake zile anakosa vitu vingi vya kumfanya kuwa kipa bora.
 
Sina imani na Onana kuwa kipa namba moja kiukweli labda aje awe chaguo la pili

Huwa namuona kama John Mwanda tu
Acha ujinga kigezo cha kuwa namba 1 ni kipi?

Hata De Gea wakati anafika alikuwa pazia.

Tusiwe brainwashed kiasi hicho hata kabla yake tulikuwa na Van Der Sar watu wanakuja na kuondoka hakuna cha daima
 
Tupo wengi. Pale hamna kipa ila watu wabishi kwasababu ya ile fainali tu.

Hata Uzoho aliwahi kucheza mechi yake vizuri sana pale OT na alikuwa ni backup GK wa Omonia.

Onana ukitoa pasi zake zile anakosa vitu vingi vya kumfanya kuwa kipa bora.
Onana watu wengi wamemjulia fainali ya UCL ila amekuwa bora kitambo tangu akiwa Ajax tunaoangalia Eredivisie Fox Sports tunaelewa japo hatukumuweka akilini wala hatukutegemea siku moja atahusishwa nasi ukizingatia wakati huo tulikuwa addicted na vitu vya De Gea.

Mbali na ligi ya England ligi nyingi watu hawafuatilii sana hasa hizo Uholanzi na Italy sasa wangemjua vipi?
Unasema mbali na pasi zake anakosa vitu vingi vya kuwa kipa bora hebu vitaje,najua saves lazima ziwemo ndio kitu cha kwanza hicho anacho pia.Hebu leta vingine hapa ambavyo hana

Hebu nenda kaangalie skills zake ana kila kitu ama mnaona kisa Mwafrika


Kingine haruhusu bao 4-7 hovyo kama kipa wetu bora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…