Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Rashford ni mchezaji hatari sana ila alikosa consistence nadhani pia ni kutokana na ubovu wa timu misimu kadhaa iliyopita. Akipunguza uchoyo na kaufather atakwenda kuweka historia kubwa kwenye soka.
Rashford hajaacha kuwa mchoyo.

Tunahitaji mchezaji wa kumpa changamoto.
 
Hivi hii Liverpool imetufungaje 7?
Mpira ni mchezo wa makosa na ufundi mwingi sana wa kimbinu. Unapoingia uwanjani ukiwa unafanya makosa mengi ya kiufundi na mpinzani wako akiwa clinical kutumia nafasi anazopata utaadhibiwa goli nyingi sana.

Leo Bournermouth kamfunga L'pool ila mchezo wa kwanza Bou walifungwa goli 9 - 0. Jinsi walivyocheza leo wamebadilika kabisa walikuwa na nidhamu ya hali ya juu bila kufanya fanya makosa ya kizembe.
 
Kwaiyo unakubali nawewe ulifungwa na timu mbovu?View attachment 2546257
7-0?

Hapa hamna Cha kujitetea ,nyie ni wabovu tu ,

Shida yenu mnafichama kwenye matokeo ,angalia mmeshindaje ,sio kubahatisha

Mfano hiyo mechi mliyoshinda 3-1 vs Arsenal ,hakuna mpira wa maana au performance ambayo ilikuwa guarantee mna timu Bora
 
L'pool ule upepo wa kutufunga goli 7 naona ulianza kuwadanganya wakajiona matatizo yao yameisha.
Liverpool inajulikana msimu huu ni wabovu , ila siokweli waliwafunga 7-0 kwa kubahatisha ,ni sababu timu yenu bado Sana ina matobo ,

Huu mpira wa janja janja hata Conte aliucheza Sana msimu uliopita ukampeleka had UCL, na akapambwa Sana atabeba EPL msimu huu, lakini tulisimama tukasema mpira wa Sasa EPL sio ule wa miaka 2015 kurudi nyuma

Kwasasa Conte anataka kukimbia Epl baada ya kuona Hali ngumu
 
7-0?

Hapa hamna Cha kujitetea ,nyie ni wabovu tu ,

Shida yenu mnafichama kwenye matokeo ,angalia mmeshindaje ,sio kubahatisha

Mfano hiyo mechi mliyoshinda 3-1 vs Arsenal ,hakuna mpira wa maana au performance ambayo ilikuwa guarantee mna timu Bora
Kinachoamua mwisho wa mashindano ni kitu gani? Jaribu kufanya comparison ya United vs English premier league teams msimu huu ktk mashindano yote. (EPL, EFL, FA pamoja na European cups)

Unasemaje timu mbovu imeshinda michezo 31 kati 43 msimu huu idadi kubwa kuliko timu yoyote ile barani ulaya ktk ligi 5 kubwa (EPL, Serie A, Bundesliga, La Liga na Ligue 1) na ni timu pekee inayoshiki michuano yote ktk vilabu vya Uingereza. Ubora wa timu unapimwa kwa kitu gani? (72.1% - winning percentage, yaani ktk kila mechi 10 United msimu huu tumeshinda mechi 7)
 
Wabovu wapo namba 3 na wazima wanafungwa na kibonde bornamouth
Hii performance ndio inawalaghai , Conte alikuwa na mpira wa ujinga ujinga Kama wenu akashinda mechi kibao na kufuzu UCL , na akaongezewa watu ,media zikasema anabeba EPL msimu huu

Sasa hivi anataka kukimbia kabisa


Nyie Kuna mechi zaidi ya 7 mnapata matokeo tu lakini hamna guarantee ya ku survive huko mbeleni ,ndio maana katika zile top 6 pale nadhani mna GD 6 , Mna viashiria vingi Sana vya middle teams ila kwakuwa hamtaki ukweli ,muda utaongea
 
Yani wewe kocha msimu wake wa kwanza Unataka aanze na kucheza soka Safi sisi sio arsenal tunataka kwenda uefa hatutaki ujinga kama wa arteta.
 
Conte na mpira wake wa ujanja ujanja ila ana kombe la juzi juzi tu hapo nyie arsenal miaka 18 Sasa no EPL CUP sasa sio Bora hata Conte kama unaona ni rahisi na nyie chezeni mpira wa ujanja ujanja uwape hata ka UEFA basi
 
Unacheza na kina reading , chalton , na timu nyingi zenye kariba hiyo unasifia ,

Mimi nipo hapa muda utaongea ,hata Conte wakati anashinda hivi nilibishiwa Sana na ule mpira wake wa ovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…