Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Kama ni project mpya niko tayari kabisa wacheze wale vijana wa pre season kila mechi nitavumilia misimu mitatu kuliko hawa wapuuzi.

Ni bora kina savage wacheze tu wapate experience hata tufungwe kila mechi niko tayari kuisubiri hiyo project ila hawa jamaa ni wameshindwa kufanya chochote

wachezaji ambao makocha zaidi ya wa4 wameshindwa kuwacoach unawategemea wa nini.
 
Kwa hiyo mnafungwa kwa sababu timu Ina madeni aliyekwambia kwamba hizo timu nyingine hazina madeni ni nan?

Kuhusu mfumo Siyo nyie mlisema kuwa yule directing manager wenu aondoke na akaondoka kwa kujiuzulu yaan kila kitu mtakachotaka mashabik mnafanyiwa iwe kuondoa mtu au kuleta mtu


Tangopori la Neville umelichukua zimazima bila kulifikiria
 
Huyo cocha sijui atamfunga nani hapo epl kwa mpira wanaocheza Man U,yaani hapo itakuwa kipigo mpaka wamfukuze hapo sijaona mechi ya kushinda huyo hapo epl,

Anauwezo mdogo sana,watu walimpamba tu lakini uwezo hana kabisa huyo epl haiwezi.

Mimi kwa mtazamo Wangu huyo kwa nanmna timu inavyocheza hawezi kushinda mechi yoyote hapo epl narudia tena hawezi kushinda mechi yoyote pale epl .
 
Umeongea kwa masikitiko makubwa sana. United kwa sasa mnapitia njia walizopita Liverpool na kina Milan. Mnahitaji muda kujenga timu itakayoweza kushinda na vilabu vikubwa barani ulaya. Na hii inahitaji muda. Lakini ile tabia ya kusainisha makocha afu muda mfupi mnawafukuza hamtaweza kuijenga timu yenu. Kwa mfano, huyu ETH tayari kaja na mfumo wake toka pale ajax. Na anaamini kwa % nyingi mchezaji aliyepitia pale ajax anaweza kumtumia na kupata mafanikio. Ndio maana anawajaza pale.
Mnapaswa kuendelea kumwamini hata kama timu inafanya vibaya, yaani mumpe muda. Angalao miaka 4, kama mafanikio yasipoonekana basi aonyeshwe mlango wa kutokea.

Liverpool wakati wanampa Klopp timu alikuta benteke ndio main striker, Kolo Toure na Momo Sakho ndio mabeki wa kati. Akawaambia kabisa. Makombe yataanza kupatikana ndani ya miaka mi4. Akaanza kuijenga timu. Kawaleta kina Mane, Salah, Alison Beker, Rob, vvd, Fab, kisha akampandisha TAA nk. Akaondoa magarasa kibao. Sakho, benteke, na wengine. Mpaka sasa mchezaji aliyebaki pale klopp aliyemkuta ni captain Heddo na msaidizi babu Milner. Waliobakia ni yeye kawaleta.
Kina Glazer wao wanaangali mkwanja tu. Watulie wamwamini ETH na wampe muda wa kutengeneza timu. Tofauti na hapo mtaendelea kupigwa tu.
 

Hawa viparangoto waliofanana kama matofali, akili zao pia zimefanana. Ila united mnajua kuchafua cv za makocha kweli. Conte ndio mtu aliyekuwa anawafaa. Mourinho mlimtimua, akaja Olesendeka mkamtimua. Akaja juke mjerumani akaonyeshwa mlango. Toka 2014 baada ya kustaafu mzee wa brown evelope mmeshaajiri makocha zaidi ya wa5
 
Mwanzo kabisa nimeanza kwa kuandika "Glazers ni moja ya matatizo ya United."
 
Mpeni team Yusuph bakharesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…