Manchester United (Red Devils) | Special Thread

RR alilalamika kuwa board miyeyusho, mpka Luiz Dias pia akaenda liverpool.. naona liverpool tena wameingilia hii deal hapa, Man U wao bado wali contact agent wake tu, hakuna kinachoendelea utaona huyu nae kasepa kwengine sisi tupo tu
 
Mchezaji kashasema anataka kucheza chini ya Klopp + hampo UCL next season, punguza makasiriko utajipa ugonjwa wa moyo bure.
 
Unajua tuna kulewa sana chief lakn shida ipo kwako kutaka kutuaminisha watu waliopo ni wazuri na wanatosheleza wakati kimsing hawana performance tunayoitegema kupata nafasi nzuri kwenye ligi...sipend kufananisha wachezaj wetu na timu zingine lakn ss Manchester tuna viungo wabovu sana Fred na mac...in fact wamepewa nafasi misimu zaid ya miwili lakn hawaja ongezeka kiwango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na inavyoonekana kocha wetu atakuja kuwa kipenzi cha board maana alisema team yetu bado ina wachezaji potential sana akasisitiza wachezaji hao ndio walifanya tukamaliza nafasi ya 2 msimu uliopita

Tofauti na RR aliyesema tunahitaji wachezaji wapya at least 7
Ralf pia aliikosoa board kuhusu kuwakosa Diaz na Alvarez
 
Ten Hag anaamini team yetu bado nzuri sababu tulishika nafasi ya 2 na wachezaji haohao
 
Sawa, tupo hapa.. ngoja tumuone bwana ETH na hiki kikosi anachosema kipo vizuri
 
Tukubali tukatae mpira sasa hivi ni biashara, utawaona Madrid wajinga kutoa £100 kwa dogo wa miaka 22, au Liver kutanguliza hiyo £80 kwa Nunez, basi tusiwashangae wakinyanyua kwapa mwisho wa msimu au mashindano makubwa Uefa n.k anyway ngoja tuone maana kocha ashasema kikosi ni kizuri
 
Sasa Chief-Mkwawa hebu nipe option ya upande wa striker tukimkosa Nunez kwa bei rahisi unayosemea? Yupi / wapi tunapata?
Mkuu sisi hatuhitaji striker anayekuja kuanza, vyovyote vile Ronaldo ndio atalead timu msimu ujao, striker anayetakiwa ni Either mtoto msimu ujao akue na sisi ama sub ya Ronaldo incase anaumia.

Nunez ni mchezaji mzuri ila kwa 85M ni risk kubwa, liverpool wapo Vizuri kila idara wanaweza kurisk hata akizingua si watamuuza tu.

Sijui kama Belloti anafit Mfumo wa ETH ila jamaa anapatikana Bure, kuwa Rotational si mbaya.
 
Kwa sasa Man Utd inabidi ifanye sajili zake za msingi kipindi cha dirisha dogo ambapo ushindani ni mdogo.
Tukifika dirisha kubwa wachezaji wanatukataa,sijui tumepotezaje mvuto ghafla hivi!
 
Mkuu Issue ya Alvarez ilikuwa nje ya Uwezo wetu, Man City wanamtangaza Leo Alvarez haikuchukua Siku nyingi yule Pimbi Greenwood anafanya yake.

Kwa Greenwood tulikuwa Tayari tuna future Top striker tunamkuza Taratibu, ndio maana Hatukuwa na Umuhimu wa kutafuta Striker wakati una Ronaldo, Cavani na Greenwood.

Pia mimi naungana na ETH, kikosi chetu si kibaya kama watu wanavyotaka kutuaminisha, yazibwe tu Mapengo, priority iwe midfielder, Board ikinunua Midfielder 2 za kazi, beki wa pembeni, na Backup striker Tunaanza vizuri tu Msimu wetu, then kuanzia hapo ndio tutajua mbivu na mbichi, ambaye hatajituma na kumsikiliza mwalimu safari yake ndio itaishia hapo.
 
Jamaa nakuelewa sana. Shida ya mashabiki wa united wanataka ETH alete wachezaji wapya karibia kikosi kizima kama walivyo aminishwa na RR. Yani wachezaji karibia 7 wasajiliwe Kwa pamoja
 
Kwa sasa Man Utd inabidi ifanye sajili zake za msingi kipindi cha dirisha dogo ambapo ushindani ni mdogo.
Tukifika dirisha kubwa wachezaji wanatukataa,sijui tumepotezaje mvuto ghafla hivi!
Vyombo tu vya Habari vinakuza mambo na Ma Agent wanaitumia Man U kuongeza thamani ya wachezaji wao. just miaka ya Karibuni Sanchez, Fred, Maguire na Ronaldo wote walikuwa wanaenda City na Tumewapokonya.

Bastian, Ibrahimovic, Pogba, Cavani, Varane, Sancho wote ni Majina makubwa wameacha timu Kibao kuja Man U.

Mtu kama Varane why aache timu zote, angeenda tu PSG kama Ramos kula bata.

Bado tuna Mvuto mkuu, mishahara mikubwa, Jina Kubwa, ni wachezaji wachache sana watakataa kuja UTD.

Ninachomuelewa ETH anataka watu wa mfumo wake, hatasajili tu ilimradi aongeze watu, unless Board imuingilie.
 
Kabisaa na ndo plan nzima ndo maana ETH alisema anahitaji wachezaji wasio zidi watano kuziba mapungufu yaliyopo huku rebuild ikizidi kuendelea mdogomdogo
 
R
RR Austria Iko ina mshinda huko,Sijui kule atamlalamikia nani,theory kibao, practical zero
 
Jamaa nakuelewa sana. Shida ya mashabiki wa united wanataka ETH alete wachezaji wapya karibia kikosi kizima kama walivyo aminishwa na RR. Yani wachezaji karibia 7 wasajiliwe Kwa pamoja
Hii timu kocha mpya akija anaona inahitaji marekebisho machache hata RR alisema hivyo lakini baada ya kufundisha ndio akajua kuwa kazi iliyopo ni ngumu sana na the way wachezaji walivyokuwa wancheza msimu uliopita kocha alikuwa sahihi kusema timu inahitaji kununua wachezaji wengi na kibaya zaidi ni kuwa tayari our main competitors(Liverpool & City) wako kwenye peak.Vikosi vyao vimeshakamilika na still wanaendelea kuboresha
 
Kama Klopp alivyo kuwa ana timua mmoja mmoja Kwa muda wake kina Mignolet,Cyle,Moreno,Lucas,Lallana,Sturrige,Kolo toure,Baloteli,skritel,Coutinho na wengine Wengi


Alianza kusogeza mmoja mmoja mpaka kikosi kikabadilika Mane,VVD,Salah,Becker,Fabinho mpaka Sasa Nunez na Kila mchezaji aliingia Kwa msimu wake
 
ronaldo asipocheza rashford anaanza mbele dah
 
Chief NUNEZ ni zaidi ya hatari kufeli pale hilo sahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…