Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Naanza kuamini hii safisha safisha ya backroom staffs ni Richard Arnold mwenyewe anaifanya kwa baraka za kina Glazers.

Rebuilding itaanzia kwake kuja uwanjani.

Nadhani anataka Man Utd iwe club ya mpira 100%, hayo ya biashara yatakuja badae.

Nampa 70% benefit of a doubt in this.
 
Ni aibu kubwa Sana man utd kucheza CL ,Mimi binafsi siamini kabisa mpaka hapo makundi yatakapopangwa ...!


Uwezo ni mdogo Sana imagine timu inagogwa 4-0 na Brighton na Bado hata zingeongezwa dakika nyingine 90 huoni wanaweza pata wapi goli ,hio hio timu wanaiaminisha dunia kuwa inaweza kucheza CL
....!
 
Hata Rangnick hakuletwa ili awe kocha kwa muda uliobaki.

Aliletwa ili aisuke upya Man Utd toka January. Aangalie wapi pa kurekebisha mpaka mwisho wa msimu.

Kama tulikuwa tunataka kuingia top 4, wangechukuliwa makocha wa kutupeleka hapo.
 
Ni mpaka msimu wa 2024/25 kwa kifupi kuanzia mwaka 2024 Man. United hatakosa Champions League msimu wowote ule au mpaka sheria zibadilishwe kutokana na historia yao kubwa kwenye michuano ya UCL.

Mimi nilitamani ianze msimu ujao maana mshaanza kulialia.
 
Ngoja leo tuamie kwa watoto labda watatufurahisha maana hawa wakubwa sasa ni homa tu..

Leo kuna Final ya FA ya under18 kati ya Manchester United na Nottingham forest .

Wenzetu mpaka vimechi vya watoto vina mashabiki wa kutosha maana hii mechi watu 65000 wamenunua ticket kwaiyo tutegemee uwanja kujaa kama kawaida.
 
Sasa huo msimu wa 2024/2025 si mtakuwa mnamaliza top 4 au mtakuwa Bado mnachezea vichapo
 
Kuna rumours za Jim Ratcliffe anataka kuinunua Man Utd.

Mnauonaje huo utaratibu?
 

Ondosha neno Man United hapo badala yake weka Timu zenye Rekodi kubwa/Nzuri ya Michuano ya Ulaya kwasababu nafasi mbili zilizopendekezwa sio za United bali ni bara zima la Ulaya.

Imagine Hawa wakose nafasi ya kushiriki
AC Milan
Liverpool
Barcelona
Man United

Hapo Manchester United hawezi kupata nafasi ya kushiriki kwani hao wengine wote wanamzidi kwa kila Kitu kwenye Mashindano ya Ulaya.
 
Chonde chonde kuweni wapole dhidi ya sifa kedekede munazomtupia ETH asijekuwa kama mwalimu wa Klopp na Tuchel.

Huyo nae hakuna kitu hapo ni swala la muda tu kama huyo mwalimu wa Klopp na tuchel tuliwaambia kwamba huyo theory nyingi sana kwenye vitendo ni zero kabisa,Epl hapo kugumu sana wachezaji lazima wachangamke.

Na huyo nae watamfukuza tu.
 

Hivi unauhakika gani kama atafiti hapo Epl, maana Epl hapo ni kugumu sana kwa Sasa makocha kila wakati wanatimuliwa. Ni vizuri tusubirie kwanza baada ya mechi kadhaa ndio tunamjua tu huyo hakuna kocha hapo au la.
 
Ndiyo maana nikasema United anaweza asikose msimu wowote ule wa UCL kuanzia 2024 kwasababu kama itafikia mwaka Liverpool atakuwa hayupo top 4 basi ujue United lazima atakuwepo top 4. Pia sheria inaangalia ligi mbili zilizofanya vizuri msimu uliopita ndiyo inatoa timu 2 zenye historia nzuri kama ingeanza kutumika next season United angefuzu kwasababu EPL ilifanya vizuri msimu uliopita na timu yenye mafanikio zaidi ya United kwenye UCL pale EPL ni Liverpool ambao tayari wamefuzu. Nimesema United kwasababu kwa rebuild inayofanyika automatically United wataanza kurudi nafasi za juu kwenye msimamo na the likes of Barcelona, Real Madrid, AC Milan ni vilabu ambavyo ni mara chache inatokea wamemaliza nje ya top na katika UCL ni La Liga na EPL ndiyo zina rekodi nzuri recently so kama sheria ingetumika miaka hii kivyovyote vile ingei-favor hii United inayosuasua kwasababu giants wengi wa UCL wanafuzu moja kwa moja, timu pekee ambayo ina-struggle ni United.
 

Nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…