Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mnaandika upumbavu Gani, hemb jisikilizishe.
 
Inawezekana labda mimi huwa namuangalia kwa makengeza ila toka kitambo sijawahi kumuelewa.
Mkuu mwaka jana Wewe, 007, na wengineo humu mulikuwa mkinipinga sana Kuhusu Ole na mkasema anabebwa na "individual Brilliance" kwamba hakuwa na Tactics ila uwezo wa mchezaji mmoja mmoja unambeba.

Leo wachezaji wale wale, mashabiki wale wale mnawakataa tena kwamba hawana Kitu. Kauli ambazo zinakinzana.

Kifupi mkuu Mpe Pep kikosi cha Dunia cha Chelsea Kina Essien, Pogba, Makelele, Lampard etc atachemka, na ukampa Mourinho Xavi, Bosquet, Iniesta, Messi etc naye pia Atachemka.

Kila mchezaji anafit kwenye Mfumo fulani, Wachezaji wetu wengi wamesajiliwa na kuwa Trained kwenye Mfumo wa Ku himili Pressure na Ku counter, linapokuja mfumo kama Wa RR tena katikati ya Msimu hilo kwao ni suala Geni.

Cha muhimu ni kuomba tu ETH apate wachezaji wake anaoawataka, wanaofit mfumo wake, hata kama akiwa ni wa sasa.
 
Mkuu suala la kukaba Kipindi cha Ole lilikuwa fixed, as of Msimu uliopita tulikuwa nafasi ya 3 (kipindi cha mou tulikuwa bottom 3 kama sijakosea) tulipitwa na Leeds na Southampton tu, kwa top 6 sisi tulikuwa juu.


Issue kwangu ninayoiona ni Tunakabia wapi, kipindi Cha ole ama Timu ya Taifa uingereza timu inakaa Nyuma, unasubiri adui umkabie langoni mwako, hapa ngumu kukuta nafasi na kuna wachezaji wakiwa compact hawawi exposed sana mfano Maguire. Japo kuna match hizo nafasi zilikuwepo midfield na tulifungwa mashuti ya mbali ya kutosha.

RR yeye ama Klop na makocha wengine wa kisasa wao wana High line pressing, ambao ni mfumo mpya kwetu, even ole alijaribu mwanzo wa msimu, kifupi wachezaji wetu wengi wamefeli huu mfumo, sababu inahitaji mukabe kwa mstari na sio mtu mmoja azunguke uwanja mzima, akitoka mmoja kukaba ndio pale unakuta bonge la nafasi linaachwa.
 
Huyu James Garner msimu ujao asitolewe tena kwa mkopo.
Huyo dogo wanapanda na timu yake. Kapiga mpira mkubwa sana msimu huu, Daemushin aliwahi kumchambua kipindi cha nyuma nilihisi labda anaweka mahaba ila kiukweli anajua.
 
Hii United inawezekana hasa ETH akipewa full control
Nakumbuka kocha alimuwekea bit martial. Si unajua tabia za Moriinho, matajiri sijui bodi ikadai sijui Hawa wachezaji ndio nyota wa timu akaja Pogba wote wakapewa throne, kocha wa watu akaanza kupata tabu, nakumbuka ndio akawaambia Pogba ni virus, Hapo hamjajua tu tatizo liko wapi?? ETH anamaanisha kuomba full control na mkataba miongo mitatu just like Moriinho bodi ikizingua anaondoka..

Wazungu hawaingii uwanjani mechi za hivi karibuni wamegoma, Ili tajiri aachie timu. Wkt wa Moriinho samani ya UTD ilikuwa 4bil Sasa sidhani kama hata wakiuza bil2 atanunua MTU.

Bodi na glazers ni wapuuzi Sana wkt mwingine nilikuwa nadhani wametumwa au wamehongwa Ili Chelsea na au riverpool nao wachukuechukue vikombe maana nilimhisi Pogba na wakina martial kama wametumwa vile! United hata siku Moja pamoja na kushika no 6 kwenye mabaa, mahoteli majumbani ndio inatazamwa. Kwa maana kwamba sokoni UTD inabamba. Share hazijaporomoka kivileee ndio maana glazer wanaiona mambo si mabaya Sana.

I bet ETH akifanikiwa UTD jinalake tuuu ulaya itateseka Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…